Nguvu ya mitandao: Nimeokota handbag yenye pesa kabla vibaka hawajaiwahi na kumrudishia aliyeidondosha kupitia Instagram

Nguvu ya mitandao: Nimeokota handbag yenye pesa kabla vibaka hawajaiwahi na kumrudishia aliyeidondosha kupitia Instagram

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
MUHIMU: Tahadhari inabidi zichukuliwe, Wema wako unaweza kuku gharimu! kabla hujachukua uamuzi wa kumrejeshea mtu vitu vyake ni lazima upate taarifa zake (ni mzima?, kapata tukio lipi?, nk) lasivyo unaweza kuingia mtegoni au kuhusishwa na kesi.. kama huna taarifa ni bora utafute njia ya kukirudisha ulichokiokota kisiri siri bila kuacha alama wala kujulikana au ikibidi uvipeleka polisi japo hawaaminiki, Binafsi niliridhishwa na ushirikiano wa upande wa pili hivyo sikuwa na wasiwasi .

Leo hii wakati nimeamka kufanya mazoezi asubuhi, nilikikuta kipochi cha mkononi (hand bag) kwenye njia ambayo huwa nafanya jogging, Nilichunguza mazingira vizuri na nikakifungua, nilikuta noti 132 za elf 10 pamoja na noti nyingine chache, flash, na kitambulisho.

Well, nikaibeba, nikaendelea na mazoezi yangu. Nilipofika nyumbani niliingia facebook na kumtafuta huyo mtu nikamkosa, niliingia twitter nilimkosa, Bahati ilioje niliingia Instagram nikamkuta kwa picha ile ile kama ya kwenye kitambulisho. hakika ilikuwa ni bahati kwa aliidondosha maana ingeokotwa na teja au kibaka ingekuwa ni historia.

nilimtumia meseji kwa account yangu ya pili (akaunti rapa) aniambie kama kuna shida imempata na anitumie verificaton picture (hapa nilimwambia anitumie picha kashika kikombe ili nijiridhishe ni yeye na sio picha za galley au za kudownload), baada ya lisaa hivi wakati nikiwa nakunywa chai nilipokea meseji yake ambayo alilenga moja kwa moja kwa shida iliyompata kuhusu kupoteza hio hand bag, kuhusu picha alisita mara ya kwanza ila nilipomwambia bila picha sitoi ushirikiano, ilibidi apige picha kashikilia kikombe)

Basi nilimwambia aondoe shaka, ninayo hio wallet, Nilimwambia aje kupitia wallet yake chumba cha mapokezi sehemu napofanyia kazi kwasababu mimi huwa sipo ofisi kuu muda mwingi (niliscreen shot hizo chats na kuzitunza online zije kuwa msaada likitokea la kutokea)

alikaja kuichukua wallet yake saa nne lakini huwezi amini kanisubiri mpaka nimerudi saa nane mchana huku akiwa haamini amini kwamba niliiwahi hio wallet badala ya Teja au kibaka.

Najua wengi mtaniona mjinga lakini niwaambie tu kwamba maumivu ya mtu unaemwibia, unaemdhurumu, n.k huwa yanaziba baraka zako. huwezi kujifariji kwamba umeokota wallet ambayo ina kitambulisho chenye taarifa za kumpata huyo mtu na ukapuuzia kumtafuta kwa kisingizio cha "cha kuokota si cha kuiba mwenye mali ni..."

Anadai hio hand bag yawekezaka aliidondosha bila kujua akiwa kwenye chombo cha usafiri, Kanibembeleza sana kunipa kiasi flani kama shukrani lakini nilikataa, aliendelea kunibembeleza sana mpaka nikaanza kuona wazi wazi kukataa kwangu ni kama kunamuumiza hivi kwa kuona namdharau, ikabidi kishingo upande nichukue kiasi kidogo sana ili kumpooza roho.

Teknolojia inasaidia sana
 
Kwa hyo milioni 1 na laki 3 ukazirudisha kwa mwenyewe.
Mimi NI muislam lakini hapo kwenye hela pangekuwa mtihani.
Kuna watu wema duniani bado wapo. Nakumbuka September nilienda Arusha, jioni nikaenda kwenye restaurant moja nikala nikaondoka.

Kesho yake nilikuwa nasafiri kwenda dodoma, asubuhi nikajiandaa safari ikaanza. Sasa kufika maeneo ya karibu na uwanja wa ndege, sijui nilikuwa nataka kutoa nini naangalia sioni wallet.

Ikabidi kusimama na kuangalia kila mahali sioni. Ikabidi kurudi mjini maana ina kadi na vitambulisho vyote maana nilipiga simu nyumbani hamna.

Nikajisemea sehemu ya mwisho jana kwenda ni pale. Nilipofika tu bahati nzuri nikamkuta mhudumu aliyetuhudumia.

Aliponisalimia tu akaniambia dada jana ulisahau kitu nikamwambia ndio. Akaniletea wallet yangu na kila kitu kilikuwepo.

Daah sikuamini kabisa, nikampa pesa kama shukrani, nikaanza safari upya. Yaani sikuamini kabisa
 
Kua makini bro mm Dogo wangu aliokotaga handbag kama ww akamtqfuta mwenyewe kupitia anuani zilizomo baada ya kumpata kesi ilimgeukia kumbe mdada aliumizwa na alikua na majeraha alafu Ni mke wa mjeshi...
wanaangalia na aina ya mtu mkuu.

Mimi mtumishi wa umma, ninapokea mshahara wangu, nina biashara yangu nimeajiri mtu, n.k siwezi kuwa suspected kirahisi namna hio kwamba nianze kukaba watu ?

Ingekuwa sina ajira, sina shughuli maalum, n.k nisingejisumbua huko kote maana naijua vizuri hii system
 
Back
Top Bottom