Nguvu ya mitandao: Nimeokota handbag yenye pesa kabla vibaka hawajaiwahi na kumrudishia aliyeidondosha kupitia Instagram

Nguvu ya mitandao: Nimeokota handbag yenye pesa kabla vibaka hawajaiwahi na kumrudishia aliyeidondosha kupitia Instagram

Kuna siku utapewa kesi ya mauaji au ubakaji ndio utajua hujui,huyo mtu angekuwa kauawa sasa hivi ungekuwa segerea,usirudie ujinga huo
juzi nikiwa hospitali ameletwa dada mmoja ameuwawa tena kwa kuchomwa na bisibisi akatupwa kwenye manyasi.
 
Ni kweli mkuu ila kumbuka siku hizi walimwengu sio kabisa. Anaweza kukugeuka na hawa mahakimu wetu wakafuata maelekezo ukaozea jela. Tahadhari ni muhimu.

Angeziacha mwenye uhitaji akaokota.
Kuna shemeji yangu aliokota simu 2013 amekaa nayo asubiri atakayepiga smu ampe maelekezo jinsi ya kuipata!! Ilikua asubuhi kufika saa kumi jioni ikapigwa simu akatoa maelekezo waende ofisini kwake smu aliokota asubuhi wkt anaenda kazini!!mwaka 2017.

Akahukumiwa kunyongwa Hadi kufa Hadi Leo Yuko gerezani !!bahati nzuri ameitwa kwenye kikao Cha rufaa ya hukumu yake tareh 23 mwezi huu anasikiliza rufaa yako ,naamini Mungu atawaongoza majaji wampe haki yake.

Ile smu kumbe ilikua ya mjeshi kapigwa Hadi kafa na vibaka wkt wanakimbia ndio wakaidondosha na yeye akapita hapo akaiona na kuiokota
 
Kuna siku utapewa kesi ya mauaji au ubakaji ndio utajua hujui,huyo mtu angekuwa kauawa sasa hivi ungekuwa segerea,usirudie ujinga huo
Mazingira ya mauaji, ujambazi ama uvunjaji yanaeleweka.

Shaka na imani potofu zisituzuie kutenda mema kwa wengine!

Mfano mzuri ni huu huu wa hii simulizi, mbona hakuna mauaji, mbona hakuna ujambazi ni mtu tu alidondosha?

Sasa wewe unashauri angefanya nini baada ya kuokota?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuchukua kitu ambacho tayari kuna vitambulisho vya kumpata mwenyewe ni WIZI. PERIOD

Tahadhali ni kumtafuta ambaye wenzake wameuawa na yeye kubakwa halafu ukamwambia una vitu vyake. Dunia haieleweki huenda IKALA KWAKO
 
Leo hii wakati nimeamka kufanya mazoezi asubuhi, nilikikuta kipochi cha mkononi (hand bag) kwenye njia ambayo huwa nafanya jogging, Nilichunguza mazingira vizuri na nikakifungua, nilikuta noti 132 za elf 10 pamoja na noti nyingine chache, flash, na kitambulisho...
Vipi kuhusu kula tunda kimasihara mmefikia wapi?
 
Back
Top Bottom