Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 72,020
- 129,293
Mkuu, Kwanza nakupongeza Kwa kujikita kuzungumzia mapungufu mengi yaliyopo sasa na hata Mimi naungana na wewe katika hayo ingawa si yote
Binafsi siungi mkono unafki mkubwa uliokubuhu Kwa wengi wetu hapa, hasa mtu anapokumbuka ya utawala uliokuwepo kabla ya huu,
Mkuu, mtu anapojaribu kukumbuka nyuma maana yake inabidi atueleze pia yoote tuliyokuwa tukishinda hapa kuyaponda, Mkwere alidharilika Sana hapa na waliomdharilisha ni haohao ambao leo wanasema wamekumbuka Uongozi wake,
Na ndiyo maana nilihitimisha kusema, wake za lutu ni wengi na hawatakaa waishe
Je kipindi cha JK wanakumbuka pia kwamba Maskini wengi waliswekwa ndani Kwa makosa yasiyo Yao, Maskini wengi walikuwa wakinyang'anywa mashamba na viwanja na matajiri, tena usinikumbushe kabisa kuna ndugu yangu alinunua kiwanja alikuwa akikiendeleza kidogokidogo siku ya siku alikuta kiwanja kile kimepigwa fensi kwenda mahakani akafungwa yeye,
Wanakumbuka pia kwamba member wa hapa bwana BAK karibu Kila siku alikuwa analeta liwaya jinsi serikali ya kipindi hicho ilivyokuwa imeoza
Staki kukumbuka uozo wa nyuma, Tusemeni na tukaze kukemea uozo uliopo leo
JK hakuwa na lolote la maana, na ukiona watu wanamsifia basi ujue wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa lengo la kumnanga Magufuli. Yaani kama ni alama za uongozi JK na Magufuli hakuna anayekaribia 50%. Kama ni ubora au udhaifu wa wawili hao, inategemea na mtoa maoni yuko katika mazingira gani kwa wakati husika.