Nguvu ya Rais Magufuli sasa inajulikana ilipo. Ni hatari kwa uchumi wetu

Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.
Asante sana kwa kututhibitishia kiwango chako cha ufahamu kilivyo kwa kujificha kwenye "keyboard", maana maisha yako ndivyo yalivyo.
 
Mkuu nakusalimia Jumamosi ya leo. Nashukuru kwa mchango wako ila na mimi nina machache ambayo naweza kukuongezea katika ufahamu wako wa masuala ya viwanda.
Ujenzi wa viwanda una pata changamoto kama moja ya vifuatavyo vitakuwa havipo,
1) Nguvu kazi.
2) Mali ghafi.
3) Nishati.
4) Soko la bidhaa ambazo tayari zimekamilika.

Kwa kwetu hapa Tanzania kuweza kuanzisha kiwanda kikubwa ni taabu sana.Mahitaji ya viwanda vya saruji kama Kiwanda cha saruji cha wazo ni karibu asilimia kumi (10%) ya umeme wote nchi hii inazalisha. Kwa hiyo viwanda kama hivyo vikiwa kumi inabidi viwanda vingine vinavyo tengenneza bidha zingine visimane. Kwa hiyo kiwanda cha Dangote kama asinge tafuta nishati nyingine na kuzalisha umeme hapo kiwandani, basi kiwanda kingefungwa .
Kwa mahitaji hayo tunatakiwa tuwe na umeme wa kutosha na kwa bei ya asilimia mia nne (400%) chini ya bei ya umeme yaleo ili tuwe washindani Africa na sio Duniani.

Hili somo ni refu kidogo na halitaki ushabiki kwa sababu ni sayansi. Tunatakiwa tuwe na uzalishaji wa umeme MEGAWATI 15,000 ili tuweze kutumia vizuri nchi yetu kiviwanda na viwanda visambae nchi nzima, Tanzania ni kubwa kuliko Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda kwa pamoja.

Asante Mkuu nachangamsha uzi na wengine wataongezra.

NAWAKILISHA.
 
Inashangaza sana kuwa haya yanatendeka ,walio takiwa kukosoa wanashambuliwa! Hivi kina Mzee Butiku na wenzake wanajisikiaje namna walivomkomlia kumkosoa JK na BWM ,Leo hali ni mbaya wamekaa kimya utawala bora uanabakwa!
Mkuu wazee wanasoma nyakati:, UKIMYA WAKO NDIO UHAI WAKO!!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kwa kututhibitishia kiwango chako cha ufahamu kilivyo kwa kujificha kwenye "keyboard", maana maisha yako ndivyo yalivyo.
"---kuthibitisha kiwango chako cha ufahamu kilivyo kwa kujifcha kwenye 'keyboard"!
Kuna sababu zipi zinazokufanya udhani najificha kwenye 'keyboard', na kwa nini unaona najificha?

Mawazo yangu si hayo umeyapata, hata kama yamepitia kwenye 'keyboard'!

Wewe ulitaka iweje? Unatishia watu kwa mawazo yao? Mpuuzi mkubwa wewe!

Unajua jinsi gani maisha yangu yalivyo, na yanakuhusu nini wewe?
 
Kwa mahitaji hayo tunatakiwa tuwe na umeme wa kutosha na kwa bei ya asilimia mia nne (400%) chini ya bei ya umeme yaleo ili tuwe washindani Africa na sio Duniani.

Hili somo ni refu kidogo
Mkuu Gerald M Magembe, hapo hakuna somo refu lisiloeleweka na yeyote anayetaka kulielewa. Najihesabu kama mmoja wa wenye uelewa wa kutosha juu ya hilo.

Kwa hiyo hayo uliyoandika hapo sio sababu ya kujibu kwa nini juhudi zilizokwishaanza, na zilitegemewa ziendelee, kwa mfano kwenye hilo swala la pamba na viwanda vya nguo kutoendelea kupata msukumo ule ule au zaidi ya ule uliokuwepo mwanzo.

Hayo uliyoeleza hapo juu siyo jibu.
Tunatakiwa tuwe na uzalishaji wa umeme MEGAWATI 15,000 ili tuweze kutumia vizuri nchi yetu kiviwanda na viwanda visambae nchi nzima, Tanzania ni kubwa kuliko Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda kwa pamoja.
Jambo la kushangaza sana hili. Unasubiri upate 15,000 MW ndipo ujenge viwanda? Uliona wapi jambo kama hilo linafanyika?

Kwa hiyo, unakokuita "kuchangamsha uzi" sio kweli. Ni upotoshaji tu.

Ukitaka nikuorodheshee kiasi cha umeme wanachozalisha Kenya na Uganda ni rahisi sana kufanya hivyo. Hili ni tatizo letu la kujifanya tunajua sana mambo kumbe hatujui chochote. Kwa Afrika Mashariki, pamoja na kwamba Kenya ndio wazalishaji wakubwa wa umeme, zaidi ya 2,000MW kwa sasa, wao ndio pia wanaoongoza kwa umeme wao kuwa aghali zaidi. Hawajasitisha kufanya mipango yao ya uzalishaji wa viwanda kwa sababu hawana umeme wa kutosha au ulio nafuu zaidi.

Lililotegemewa lifanyike hapa kwetu, ni kuendelea na juhudi zetu zilezile ambazo tulishazipanga hata kabla ya huo umeme mwingi kuwepo, ziendelee. Unasitisha watu wasilime pamba eti bado unasubiri umeme?
 
Ni kweli, kama alivyosema mdau hapo juu, mods mme edit title. Mods mods, yaani nyie!
Anyways, watanzania hatuna shukrani, tumeambiwa kwa miaka hii michache vimejengwa viwanda zaidi ya 6600! Basi angalau tushukuru. Imagine all those jobs created by this surge of industries! Forever we are grateful.
 
"---kuthibitisha kiwango chako cha ufahamu kilivyo kwa kujifcha kwenye 'keyboard"!
Kuna sababu zipi zinazokufanya udhani najificha kwenye 'keyboard', na kwa nini unaona najificha?

Mawazo yangu si hayo umeyapata, hata kama yamepitia kwenye 'keyboard'!

Wewe ulitaka iweje? Unatishia watu kwa mawazo yao? Mpuuzi mkubwa wewe!

Unajua jinsi gani maisha yangu yalivyo, na yanakuhusu nini wewe?

Ungemwambia tu

Mwanaume hashindani na sidiria

Idadi ya vifo Italia imefikia 10000
 
Mbona hujaeleza nguvu ya Magufuli ipo wapi Kama kichwa Cha uzi kinavyojieleza?
Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao mnaowaita mabeberu ndio soko la mazao yenu, mnatukana weee ooh mabwanyenye, manyonyaji, makupe halafu mnawapelekea mazao yenu korosho, kahawa pamba, mnafikiri watanunua kwa sh ngapi, nini kazi za mabalozi wao kama si kufuatilia mitandao na hotuba za viongozi wenu?

Hapo ndio kahawa ya TZ inanunuliwa kwa robo bei ya kahawa ya Kenya. Waambieni wafalme wenu na wapambe wao wajifunze diplomasia, au wafunge domo.
 
Mkapa,Ukweli na Uwazi,sijui Kama huo Ukweli na Uwazi ulikwepo.
Kikwete Maisha Bora kwa Kila mtanzania,sijui kama hayo maisha Bora yalikwepo.
Magufuli,Tanzania ya Viwanda.Usitegemee Kama hivyo viwanda vitakwepo.Manifesto zote huwa zinafeli
 
Umeweka hapa mambo kadhaa yanayostahiri kupewa 'attension'

Sijatumwa, hili liwaze vizuri. Nadhani umelipachika tu hapo bila ya kutilia maanani. Kwa nini nitumwe?

Unasema "nakumbusha upuuzi ulioshamiri enzi ya awamu ya nne" Hebu nipe mfano tu wa niliyokumbusha ambalo ni upuuzi.

Mipango ya kuzalisha pamba kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya viwanda vyetu, ni upuuzi?

Kwa hiyo ndio sababu mkazo juu ya hilo ulisitishwa baada ya awamu ya tano kuingia madarakani?

Sijaandika mengine yoyote yaliyofanyika awamu ya nne, isipokuwa hili la viwanda. Hivyo viwanda vilivyofunguliwa mapema kwenye awamu ya tano, vilitokana na 'upuuzi'?

Kuonyesha jinsi usivyokuwa makini, uaneleza mambo ya Bwawa..., una maana baada ya uamzi wa kutengeneza bwawa, mipango iliyokuwepo inaendelea ililazimu isimamishwe kusubiri bwawa?

Hiyo ni serikali ya wapi, inayosimamisha shughuli zake ambazo tayari zipo kwenye utekelezaji kwa vile mipango mipya ndio imeanzishwa! Hili bwawa ni vita?

Kutokana na majibu yako, inaonekana umo serikalini. Ni mtumishi wa serikali kwa kutegemea fadhira. Watu kama nyinyi mnalirudisha nyuma taifa letu.
Nianze na la mwisho…hapana mimi sio mtumishi wa serikali,
Pili, sijasema shughuri za viwanda zimesimama, ukweli ni kwamba zinaendelea na zitashamiri zaidi kwa viwanda vingi zaidi kufunguliwa hasa baada ya umeme kupatikana kwa wingi na kwa gharama nafuu!
Kutotangaza kufunguliwa kwa viwanda kwa muda huu wa karibuni hakumanishi hakuna viwanda vinavyofunguliwa! Nilikushauri, kabla hujakurupuka na mihemko ya kuanza kukosoa, uende kwanza kwenye kitongo husika ktk wizara husika upate 'updates' kuhusu viwanda vilivyofunguliwa hivi karibuni bila ya kupigiwa mbiu, na upate 'trend' ya ufunguzi wa viwanda tangu awamu hii iingie madarakani!
Mwisho…awamu ya nne imefanya mambo mengi sana ambayo yamesababisha kumpaisha sana Magu kwa kuwa yeye anafanya kinyume! Ubwetefu, rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya, matumizi mabaya ya madaraka na mali ya umma, n.k. ndivyo viliipamba sana awamu ya nne. Awamu ya 4 iliingia madarakani kukiwa na fedha ya kutosha hazina na BK, lakini mchwa uliitafuna na kuacha ukata hazina na BK, na hivyo awamu ya tano kuanza 'from ground zero!
Sasa kwa watu kama ww, napata shida juu ya uwezo wa kutunza kumbukumbu ya wapi tulipotolewa na awamu ya tano na wapi tulipo na tuendako!
Nakuomba usikurupuke tena, fanyia kazi huo ushauri kwanza!
 
Back
Top Bottom