Nguvu ya Rais Magufuli sasa inajulikana ilipo. Ni hatari kwa uchumi wetu

Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.

Pamoja na Coronavirus duniani wewe unaleta uzi huu. My God. Ndo Hapo unaona Kuna Shida kubwa sana kwenye akili zetu watz.

But tell us Sasa una tatizo gani kubwa moyoni mwako. Wewe binafsi, mana siku Zote naamini Hakuna makundi katika maumivu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kiwanda cha kina pole pole na bashiri kinachozalisha upupu.Kipo active kweli,aina nyingine sijawahi sikia!
 
Ubabe hauwzi kudumu..... Amebaki peke yake alafu kazeeka vibaya sn mpaka huruma
 
Mkuu, Kwanza nakupongeza Kwa kujikita kuzungumzia mapungufu mengi yaliyopo sasa na hata Mimi naungana na wewe katika hayo ingawa si yote

Binafsi siungi mkono unafki mkubwa uliokubuhu Kwa wengi wetu hapa, hasa mtu anapokumbuka ya utawala uliokuwepo kabla ya huu,

Mkuu, mtu anapojaribu kukumbuka nyuma maana yake inabidi atueleze pia yoote tuliyokuwa tukishinda hapa kuyaponda, Mkwere alidharilika Sana hapa na waliomdharilisha ni haohao ambao leo wanasema wamekumbuka Uongozi wake,

Na ndiyo maana nilihitimisha kusema, wake za lutu ni wengi na hawatakaa waishe

Je kipindi cha JK wanakumbuka pia kwamba Maskini wengi waliswekwa ndani Kwa makosa yasiyo Yao, Maskini wengi walikuwa wakinyang'anywa mashamba na viwanja na matajiri, tena usinikumbushe kabisa kuna ndugu yangu alinunua kiwanja alikuwa akikiendeleza kidogokidogo siku ya siku alikuta kiwanja kile kimepigwa fensi kwenda mahakani akafungwa yeye,

Wanakumbuka pia kwamba member wa hapa bwana BAK karibu Kila siku alikuwa analeta liwaya jinsi serikali ya kipindi hicho ilivyokuwa imeoza

Staki kukumbuka uozo wa nyuma, Tusemeni na tukaze kukemea uozo uliopo leo
Mapungufu ya awamu iliyopita si mafanikio ya awamu ya sasa. Ajipambanue kwa kuboresha uchumi wa nchi,mtu mmoja mmoja na huduma za jamii na si kukamia watu waishi kama mashetani!
 
Mkuu Odhambo, ili uchumi wa wananchi urejee ni kitu gani kifanyike mkuu, ningependa kujifunza ktk hili, samahanimkuu
Mfano tu. Hivi kulikuwa na ulazima wa kuwanyang'anya wafugaji mifugo yao yote ?! Kwa kuwasomea tu sheria, kuwa ng'ombe moja anakula majani ya shs 5000 siku kwa miaka mitatu !! Unampigia hesabu mchungaji anachanganyikiwa kisha anashindwa kulipa faini. Halafu hao hao ng'ombe wanauzwa kwa wafanyabiashara kwa bei poa ?!!. Huyu mfugaji uchumi wake si umeuua ?!. Kwa nini wasiwekewe sera nzuri inayowezekana.

Mfano wa pili ni wavuvi. Walichofanyiwa na operations za Mpina ni kuua uchumi wa kila mvuvi, bila kuangalia ni haramu au halali . Tembelea maeneo waliko watu hao uniambie wana hali gani. Na ulete mrejesho.

Kukua kwa uchumi ni kuwawekea watu sera na sheria rafiki ili wamudu kujikwamua. Siyo hii ya kufurahia kuongoza maskini na ombaomba [emoji120][emoji40]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na Coronavirus duniani wewe unaleta uzi huu. My God. Ndo Hapo unaona Kuna Shida kubwa sana kwenye akili zetu watz.

But tell us Sasa una tatizo gani kubwa moyoni mwako. Wewe binafsi, mana siku Zote naamini Hakuna makundi katika maumivu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu 'unprejudised'
Mbona unalisaliti jina lako? Ni kitu gani kwenye mada hiyo kilichokuumiza roho kiasi hivho!

Uansema "---pamoja na coronavirus duniani..."; una maana mengine yote yamesimama imebaki corona peke yake?

Na hata kama maisha yetu yangebaki kuendeshwa na corona pekee, wewe huoni mada inazungumzia mambo kabla ya corona, au akili ni ndogo haitoshi kukuelekeza hivyo?

Kuonyesha usivyokuwa makini na unayoandika, tazama haya maneno yako yafuatayo:

"....Wewe binafsi, maana siku zote naamini hakuna makundi katika maumivu".

Unaelewa maana ya maneno haya, au unajiandikia tu mradi uonekane unajua kitu? Kama kuna corona unayotaka tuiweke mbele zaidi ya mengine yooote, kwa maana yako, kila mtu ashughulike kivyake, na sio kama kundi la watu/nchi.

Kwa haya uliyoweka hapa, nakuona kwamba huna ujualo.

Samahani sana lakini mkuu.
 
Wengi waoo (Lumumba People) wanajitoa ufahamu tu siyo kwamba hawajui hali halisi. Mm binafsi nilikuwa na mtumbwi mmoja kwa ajiri ya uvuvi wa dagaa. Nilikuwa nimeajiri watu 5 katika mtumbwi huo, lakini bila huruma: mtumbwi, machine, nyavu za kuvulia (mitego) na makalabai, vyote vilitaifishwa (vilichukuliwa na kuharibiwa) na bado nikawa na kesi ya kujibu, ya kwa nini natumia nyavu zisizoruhusiwa, wakati kwa kipindi hicho hapakuwa na nyavu zingine walizokuwa wanadai ndizo zinafaa.
Kutokana na hayo, sasa hivi nimebaki msaka tonge, wakati nilikuwa nimeajiri watu 5. Watu hawa kwa sasa nao wanalia njaa kali. Sasa, huyu ni mimi wa mtumbwi mmoja. Je aliyekuwa na mitumbwi 5-10, alipata hasara gani?
Kuna jamaa mmoja alinyang'anywa mitumbwi 5 na vifaa vyake, akawa kama mwehu kabisa. Mwanzo alikuwa kada mtiifu wa CCM kwa sasa ni mpinzani zaidi ya hao wewe unaowajua kuwa ni wapinzani wa kweli.

Lakini pia mm nilikuwa nina mabwawa ya samaki kando ya ziwa Victoria, kwa kipindi cha nyuma kabla ya 2015 tulikuwa tumeruhusiwa kufuga samaki sehemu hizo, lakini miaka ya 2016/2017 bila kutaarifiwa walitumwa maaskari wakayabomoa na kuharibu kabisa mabwawa hayo. Mpaka watu wengine walikufa kwa Presha. Haya huwezi kuyajua kama siyo mhusika.

Ebu sasa fikiria mtu alikuwa ana mabwawa 2 yenye samaki 1000 kila moja, na samaki hao wana umri wa miezi 5. Then kufumba na kufumbua yametoweka, hivi unahisi alijikuta ktk hali gani?

Mfikirie mzee wangu pale Kagera anayelima KAHAWA ambaye kipindi cha nyuma aliruhusiwa kuuza kahawa yake kwenye soko huria, kulingana na soko lililozuri ( penye bei kubwa zaidi). Sasa leo analazimishwa kuuza sehemu moja, kwny vyama vya USHIRIKA kwa bei iliyopangwa na serikali tena kwa mkopo. Unahisi anajisikiaje sasa?

Mfano: bei ya kahawa kwenye vyama vya ushirika ni 1000/= kwa kilo hapa Tanzania. Ukivuka Rwanda au Uganda bei ni nzuri zaidi labda 2500/= kwa kilo #thaman y tsh#. Halafu huko kumbuka ni tasilimu. Na huku kwetu ni mkopo na kuzurumiwa kukiwemo. Ukimwuliza waziri utasikia TUNATAKA KUMKOMBOA MKULIMA.
1. Je huo ndo ukombozi kweli?
2. Je Kuna dhamira ya dhati ya kumkomboa mkulima?
3. Je ndo maisha ya wanyonge yameimarika kama tunavyoelezwa?

Yapo mengi sana ya kusema, sema tu hata tukisema bado tuanaonekana ni wachichezi hata kwenye haki zetu.

Maandalizi ya KAWAHA mpaka mtu anavuana kahawa hiyo ni takribani mwaka mzima, bado pembejeo, wafanyakazi (wasaidizi) maana kama una shamba kubwa lazima utoe ajira. Lakini kwa sasa malipo yanayotolewa, MKULIMA hawezi toboa.

Lakini, aidha kwa kujua, kwa makusudi ama kwa kutojua, walioko kwenye mfumo wakiongozwa na MKUU WA MALAIKA hawajali. Wamebaki wanapambana na WAPINZANI, kana kwamba ndo walioharibu UCHUMI wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini, aidha kwa kujua, kwa makusudi ama kwa kutojua, walioko kwenye mfumo wakiongozwa na MKUU WA MALAIKA hawajali. Wamebaki wanapambana na WAPINZANI, kana kwamba ndo walioharibu UCHUMI wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Mkuu 'Gitah'
Nilitaka kuanza na samahani ya kukuuliza asili ya jina lako; lakini, ah, ndio hivyo nimekwishauliza.

Nimekusoma vyema mkuu, na kukuelewa barabara. Wengi tumeathirika na 'operesheni' hiyo hata kama sio moja kwa moja. Ndugu waliokuwa wameanza kujitegemea badala ya kututegemea kwa vimisaada, sasa wamerudi kuwa omba omba kwetu tena.

Katika yooote uliyoandika, kuna mambo yalifanywa/tekelezwa vibaya. Pengine utekelezaji wake usingekuwa mbaya kiasi kile, hali isingekuwa mbaya sana.

Mtazamo wangu: 'operation' ile ilikuwa ni 'overdue'.

Kuna mambo hayakustahiri yafanyike yalivyokuwa yanafanyika kabla ya operesheni. Siwezi kamwe kumlaumu moja kwa moja muathirika nikamwacha pia kulaumu aliyeruhusu hali ikawa mbaya kiasi kile.

Chukulia hilo la kahawa huko Kagera. Hata kama ni swala la soko huria, ni nchi gani ilisinzia usingizi wa pono mali yake ikiuzwa kunufaisha nchi nyingine? Huo ulikuwa uzembe wa serikali yetu kusimamia zao hilo na kuhakikisha kwamba wakulima wake hawalazimiki kuvusha mazao yao nje.

Hilo moja.

Huu uvuvi wenu, serikali iliwaacha mkawa mnatumia zana zisizokuwa nzuri kwa uendelevu wa kazi yenu. Sheria zipo, zilishatungwa kuhakikisha nyavu fulani haziruhusiwi. Serikali/watendaji wakaona sheria hazina maana, au wakaamua kuzitumia kujipatia chochote, nanyi mkaona ndio kawaida.

Mara paaa, akaja Magufuli. Pamoja na yeye kuwa mkiukaji wa sheria zisizomfaa, akaona asimamie sheria zilizopo kupitia kwa kichaa mwenzie. Mpina. Mpina na ukichaa wake hakuwa na mda wa kutizama operesheni ifanyike vipi ili isilete maumivu makubwa kwa hawa walioikiuka.
Kachoma nyavu na mengi mengine ambayo hayakupendeza.

Sasa tupo hapa, baada ya yote hayo. Watu wanalia maumivu, lakini sheria imetekelezwa kihovyohovyo.

Lililopo sasa, ni kutorudia makosa.
Kama wewe ni mvuvi, fuata maelekezo. Fanya kazi zako ndani ya sheria.

Kila mara kumbuka, gharama ya kukiuka sheria ni kubwa zaidi kuliko kubaki ndani ya sheria.

Huo ndio mtizamo wangu juu ya hayo uliyoandika hapo juu. Pole kwa maumivu; lakini pia, jifunze, usikiuke taratibu zilizowekwa katika jambo jingine lolote tena.
 
Ndugu, hatujifanyi, bali tunasema kwa capital letters kuwa "HATUONI" kabisa kwa miaka mi5 (2015 - 2020)

Wewe unayeona kanusha kutokuona kwetu kwa ushahidi thabiti usio na shaka...!!
Maendeleo niliyoyaona kwenye Serikali ya JPM ni Kasi ya kutengua na kuteua kwa kuzingatia sifa ya kuimba mapambio.
 
Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.
unapoandika kitu kama hiki namba na evidence uwe unawek, mifano na kulinganisha takwimu, otherwise ni vacuum talk.

magufuli ni dikteta lakini kwenye kazi huwezi kumlinganisha na mwizi Jakaya.

Really, JPM ni dictator ila yule congenital corrupt Jakaya, no. We can correct JPM by pushing him
 
Ngoma ya kitoto haikeshi mkuu. Mwijage sijui yuko wapi maana yeye angalau alikuwa ana guts za kutamka maana ya neno viwanda bila kupepesa macho
Kweli kabisa mwijage pa1 na usanii wake ila aliimudu wizara.
 
Nafikiri wewe hujaelewa au kumuelewa Lengo la awamu ya tano.
Na suala la maendeleo ya kiuchumi na mengineyo ni la majumuisho ya vitu vingi.
La viwanda ni juhudi za watu binafsi au tuseme private sector kuifanya, njia nyingine ni watu wenyewe waji organise waanzishe hivyo viwanda, kuna partnership, joint venture, cooperatives, companies nk nk kama ilivyokuwa somaigroup, jv group, a to z, sunflag , la hilo likishindikana ndio serikali inaweza ku prop up kwa kuanzisha hivyo viwanda au kuomba mashirika yake yafanye hivyo , na juhudi hizo zimeanza ktk sugar industry.

Sasa wakati huo huo unapozungumzia viwanda, pia kunatakiwa kuwepo na source of raw material ambayo ita tokens na uzalishaji toka kwa wakulima binafsi usafiri, bank , maghala nk.
 
Busara zilikuwa ziaze ktk kufufua mazo ya biashara kwanza ili kuvutia uwekezaji ktk viwanda, Pia tuanze kufufua viwanda vyote alivyoanzisha Mwalimu. Badala yake tukaanza mkakati wa kujenga viwanda vipya bila dira ya aina yoyote! Tumeishia kuhesabu vyerehani na machine za kufyatulia matofali kama viwanda! Shame!
Kanuni bora katika maisha unapokuta mke wa mtu hajafanikiwa kupata mtoto usimseme hovyo. Hata wewe uliyepata watoto kumi, wote kumi wanaweza kutwaliwa na Mungu kama wale watoto wa Ayubu.

Usibeze kazi waliofanya kaka na dada zako kukulea. Ni kazi nzuri na yenye kheri. Mtu atuvuna alichopanda. Ukipanda upole utavuna huruma. Ukipanda ubabe na dharau utavuna fedheha.
 
Nafikiri wewe hujaelewa au kumuelewa Lengo la awamu ya tano.
Na suala la maendeleo ya kiuchumi na mengineyo ni la majumuisho ya vitu vingi.
La viwanda ni juhudi za watu binafsi au tuseme private sector kuifanya, njia nyingine ni watu wenyewe waji organise waanzishe hivyo viwanda, kuna partnership, joint venture, cooperatives, companies nk nk kama ilivyokuwa somaigroup, jv group, a to z, sunflag , la hilo likishindikana ndio serikali inaweza ku prop up kwa kuanzisha hivyo viwanda au kuomba mashirika yake yafanye hivyo , na juhudi hizo zimeanza ktk sugar industry.

Sasa wakati huo huo unapozungumzia viwanda, pia kunatakiwa kuwepo na source of raw material ambayo ita tokens na uzalishaji toka kwa wakulima binafsi usafiri, bank , maghala nk.
This is a broad daylight lie. Give us a rest!
 
Nakumbuka zile mbwembwe nyingi za kufungua viwanda karibu kila wiki kwa wakati fulani mwanzoni mwa awamu yake. Viwanda vingi alivyovifungua, vyote vilikuwa ni juhudi za Rais Kikwete.

Siku hizi hata kusikia tu lile neno la viwanda ni nadra kabisa, na baadhi yetu hatujui kama wizara hiyo bado ipo au ilifutwa, maanake hata waziri mwenyewe hajulikani kama yupo au hayupo.

Zao la pamba, wakati wa Kikwete, lilikuwa limewekewa nguvu sana kiasi kwamba maeneo yote panapolimwa zao hilo palianza kuonekana kuwa shughuli ya kulifufua zao inafanyika. Simiyu ilianza kuonekana kama mkoa maalum wa kulima zao hili.

Juhudi za kulifufua zao hilo, ulikuwa ni mkakati wa kufufua viwanda vya nguo, ili pamba tunayozalisha isindikwe hapa hapa kwetu, na kulisha viwanda hivyo. Hali hii ilitia matumaini makubwa.

Sasa sikumbuki ni lini nimesikia habari zinazohusiana na mikakati hiyo, badala yake, inaelekea hata hiyo pamba kidogo itakayoendelea kuzalishwa, tegemeo letu ni kuwauzia wenye viwanda nchi jirani yetu hasa pale Kaskazini.

Hili litakuwa ni jambo la kusikitisha sana, kwa sababu tunapoteza fursa za waTanzania katika mnyororo mzima wa zao hili muhimu.

Na kwa uhakika, wenzetu hawa wamepania hasa na mikakati yao ya kushika soko zima la ukanda huu katika swala la nguo. Wamefufua viwanda vyao, na hata zao la pamba wakaamua kulima lile la aina mpya, lisiloshambuliwa na wadudu (genetically modified), bila shaka lengo lao likiwa kujitosheleza zaidi kwenye viwanda vyao.

Hata mitumba wameamua kuipiga marufuku, ingawa ndio waliotulazimisha tusalimu amri tulipotishiwa AGOA. Ni wajanja sana hawa watu!

Hili ni eneo moja tu la viwanda, ambalo limemshinda wazi wazi Rais Magufuli kulitilia mkazo unaostahili. Miaka mitano yake yote, mbali ya kuimba kwa nguvu sana hapo mwanzo kuhusu umhimu wa viwanda, mwisho wake, kama ni alama, anastahili F kubwa kabisa.

Rais Magufuli hatatuvusha kabisaa, katika maswala ya viwanda. Labda tutegemee hayo mengine, kama ya Miundombinu, sio viwanda.

Najua kuna maeneo mengine mengi yaliyomshinda, lakini hili la viwanda lipo dhahiri.
Inaitwa ugeni wa ofisi au nguvu ya soda ngoma ya kitoto haikeshi
 
unapoandika kitu kama hiki namba na evidence uwe unawek, mifano na kulinganisha takwimu, otherwise ni vacuum talk.

magufuli ni dikteta lakini kwenye kazi huwezi kumlinganisha na mwizi Jakaya.

Really, JPM ni dictator ila yule congenital corrupt Jakaya, no. We can correct JPM by pushing him
Mkuu, hii sio 'publication paper'.

Ukitaka hiyo nitakupa vizuri bila ya taabu yoyote.
 
Back
Top Bottom