Nguvu ya Rais Magufuli sasa inajulikana ilipo. Ni hatari kwa uchumi wetu

Hata sielewi unaandika kitu gani hapa kilicho tofauti na mada iliyopo.

Mada haijasema viwanda lazima viwe vya serikali.

Mada haijasema 'source of raw material' isiwe ya wakulima binafsi.

Usichoelewa au hutaki kukiandika ni kwamba serikali inatoa sera na kuzisimamia katika maeneo kama haya ya viwanda.

Sera hizi ziwe ni endelevu, sio kila awamu inayoingia madarakani wanachora za kwao na kubadili mwelekeo wa nchi. Katika hali hiyo hutapata maendeleo ya aina yoyote.
 
Kwa private sector ni ngumu kuwekeza kwenye Sera zisizotabirika ni sawa na kuchezea shillings
 
magufuli ni dikteta lakini kwenye kazi huwezi kumlinganisha na mwizi Jakaya.

Really, JPM ni dictator ila yule congenital corrupt Jakaya, no. We can correct JPM by pushing him
Mkuu 'Interested Observer'

Imenibidi nirudi kuiangalia hii mistari miwili uliyoweka hapo juu na kukusahihisha uelewe maana niliyonuia katika kumtaji Rais Kikwete.

Nimeandika alichofanya Kikwete katika eneo la viwanda, hasa sera ya kuvifufua viwanda vya nguo na kuimarisha upatikanaji wa mali ghafi kwa ajiri ya viwanda hivyo.

Hili mimi niliona Rais Kikwete aliliweka sawa; na lilistahiri kuwekewa mkazo na kuendelezwa na aliyerithi nafasi yake.

Sijalinganisha Rais Magufuli katika eneo jingine lolote na Rais Kikwete.

Kwa hiyo ukitaka kuchambua niliyoandika hapo juu, jizuie kuwa na tamaa ya kuangalia ujumla wa hawa viongozi kama unavyoshawishika kufanya hapa.
 
Hujakutwa na dhahma wewe.
 
Mleta mada kama sio diaspora,

Basi ni korona ndio itakuwa imemfanya asahau yale yote awamu hii iliyoyafanya katika sekta ya viwanda.

Sote tulikuwa mashuhuda wa ufunguzi wa viwanda kadhaa na pia tunaendelea kushuhudia viwanda vingine vikifunguliwa.

Mleta mada aende wizara apewe takwimu za idadi ya viwanda vipya vilivyofunguliwa toka awamu hii imeingia madarakani.

Nilitegemea kuona data hapa zikizungumza lakini kwa bahati mbaya tunalishwa maneno matupu tu ya mleta mada ambayo ki msingi ni hisia, kwa mtu yeyote makini , huwezi kuongozwa kwa hisia pekee, tunahitaji data.
 

Muhimu uje na takwimu ya idadi ya viwanda vilivofunguliwa
 
Moderator ume edit heading ya uzi huu kwa kuogopa nini ? umeharibu maana nzima , kama umetishwa au haukupendezwa na nondo zilizomo kwanini usiufute tu ili tujue moja ? Kalamu1
Hilo si tatizo mkuu Erythrocyte, ni lazima ujue mazingira wanayofanyia kazi. Usiwalaumu.

Lililo mhimu ni kama mada inaeleweka. Wakibadili na hiyo, hapo ni bora kuifuta yote.
 
Unategemea nn kama washaur wakuu ni bashite na mganga wake kienyeji
 
Tanzania ya Viwonder,

Wenye akili walipata kuponda!
 
Hilo si tatizo mkuu Erythrocyte, ni lazima ujue mazingira wanayofanyia kazi. Usiwalaumu.

Lililo mhimu ni kama mada inaeleweka. Wakibadili na hiyo, hapo ni bora kuifuta yote.
Ni vema wakawa wanatoa taarifa kama wana edit basi ili tujue , sikuona shida ya ile heading ya mwanzo
 
Eti limemshinda! Umetumwa kujaribu kukumbusha upuuzi mwingi ulioshamiri enzi ya awamu ya nne eeh! Watu wenye mtazamo finyu kama wewe ni wepesi sana kurukia hitimisho! Kwa kifupi, maswala ya viwanda mpaka sasa ni mvua za rasharasha! Ngoja bwawa la kufua umeme wa maji la Nyerere likamirike ndio mvua za mafuriko ya viwanda utaiona! Kwa sasa hali ya gharama ya umeme bado haijawa rafiki kiasi hicho ktk uanzishaji viwanda! Lakini hata hivyo vlivyoanzishwa vinaendelea na uzalishaji! Ustake kula vitu vilivyopo chunguni vikichemka, subiri viipuliwe na uandaliwe meza ndio utafaidi kwa utulivu, sio kwa kukurupuka ki hivi!
Na isitoshe, kuna mambo mengi yanaendelea ktk sector ya viwanda Tz ambayo hayatangazi! Kama unataka kufwatuka na uzi wenye tija, pita wizari husika utapata taarifa zenye uhakika sio hizi za kujiokoteza okoteza tu…kisa chuki binafsi cha jemedari raia namba 1, baba lao, rais mpendwa Mh. Daktari John Joseph Pombe Magufuli!
 
SGR waliishiwa hela kabla haijafika Moro, mkandarasi alishaondoka site na vifaa vyake!
Kuna watu naona mmechoka kuishi uraiani kwa kuamua kufanya kwa makusudi makosa ya kimtandao! Mbona unaleta uchuro? Na kwa taarifa yako hilo halitatokea, we subiri very soon uzinduzi wa safari za Dar-Mora kwa speed ya 5G utafanyika mbaki na aibu yenu wenye viroho vya kwanini!
 
Ngoma ya kitoto haikeshi mkuu. Mwijage sijui yuko wapi maana yeye angalau alikuwa ana guts za kutamka maana ya neno viwanda bila kupepesa macho
Aisee kweli hii ni Tanzania, mimi nilishasahau kama kuna mtu anaitwa Mwijage kwa kweli
 
Ndugu, hatujifanyi, bali tunasema kwa capital letters kuwa "HATUONI" kabisa kwa miaka mi5 (2015 - 2020)

Wewe unayeona kanusha kutokuona kwetu kwa ushahidi thabiti usio na shaka...!!
Maandishi yangu ndio utayaona!!?



MAGUFULI4
 
Hujakutwa na dhahma wewe.
Ikinikumba kwa sababu za kutofuata taratibu na sheria zilizopo, na bila ya uonevu wa hiana wa hao wanaofanya inikumbe; nitajilaumu mwenyewe.
 
Zipo jamii si wazuri kwenye reasoning bali Kwa matumizi ya nguvu hata ukisoma colonial history it is nature, Sasa ukizimix lzm uende mtaroni,wa nguvu abakie kwenye nguvu Na wa reasoning hivo hivo
 
Umeweka hapa mambo kadhaa yanayostahiri kupewa 'attension'

Sijatumwa, hili liwaze vizuri. Nadhani umelipachika tu hapo bila ya kutilia maanani. Kwa nini nitumwe?

Unasema "nakumbusha upuuzi ulioshamiri enzi ya awamu ya nne" Hebu nipe mfano tu wa niliyokumbusha ambalo ni upuuzi.

Mipango ya kuzalisha pamba kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya viwanda vyetu, ni upuuzi?

Kwa hiyo ndio sababu mkazo juu ya hilo ulisitishwa baada ya awamu ya tano kuingia madarakani?

Sijaandika mengine yoyote yaliyofanyika awamu ya nne, isipokuwa hili la viwanda. Hivyo viwanda vilivyofunguliwa mapema kwenye awamu ya tano, vilitokana na 'upuuzi'?

Kuonyesha jinsi usivyokuwa makini, uaneleza mambo ya Bwawa..., una maana baada ya uamzi wa kutengeneza bwawa, mipango iliyokuwepo inaendelea ililazimu isimamishwe kusubiri bwawa?

Hiyo ni serikali ya wapi, inayosimamisha shughuli zake ambazo tayari zipo kwenye utekelezaji kwa vile mipango mipya ndio imeanzishwa! Hili bwawa ni vita?

Kutokana na majibu yako, inaonekana umo serikalini. Ni mtumishi wa serikali kwa kutegemea fadhira. Watu kama nyinyi mnalirudisha nyuma taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…