Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
maskini wafuasi wa Amollo humtukuza odinga kiwango hata ikiwa odinga atawaibia fulusi wazi-wazi mchana, watasema si mwizi bali ni Agwambo yaani Simba.
nakushukuru mkuu @Rutashubanyuma kwa kututembelea. very nice of you, we appreciate it. Those who labor for the truth are few but they that harvest thereof are many.
kama umegundua kitu uhuru he is not serious enough as if anajua iko kitu inakuja hii inatokana na ICC Case imewaumiza sana kisiasa ila kwa kwa kuwa ni mwanasiasa hana jinsi anajitahidi awepo kwenye historia the only guy who is serious enough ni odinga raila .kuelekea huku mwishoni ukabila hauna nafasi tena ,kwani hii turufu hutumiwa na wanasiasa wanapoona maji yamezidi unga .mkuu ruta tayarisha champagne aina ya chandoon siku ikifika raila sworn as a kenya president .HUGO CHAVES siku Uhuru anatangazwa mshindi usikose jamvini kunipongeza kwa kuwa na kionambali...........
Kabaridi baada ya uchaguzi huu kuna wengi wanamwombea mema Amollo wataingia mitini......
RUTA unaweza kuwa mkubwa ki umri lakini ukawa bogus in thinking. Nakala yako umeiandika tarehe 29 Dec.lakini acording to the current political trend in kenya,inaonyesha huna updates whats going on.mudavadi alipokimbia Odm sababu kuu ilikuwa njia itakayotumika kumpata odm flag bearer,huko alipohamia kapakimbia tena,akipingana na njia ya wajumbe aliyokuwa akiidemand odm,je una lolote la kusema abt mm tena?.....RUTA kalonzo na odinga sasa wapo pamoja chini ya mwamvuli wa Cord na wanafanya kampeni zao pamoja.je watambwa hilo? In politics siku zote hakuna rafiki wala adui wakudumu.....RUTA uhuru na ruto ni watoto waliokulia kanu na kulelewa kisiasa na mzee moi,kumbuka moi ndio alimnominate uhuru kuwa mbunge kwa mara ya kwanza na kumpa uawaziri wa local gov,hapo tunaweza sema kanu imerudi kwa njia nyingine,(uhuruto)....RUTA uhuru na ruto wanatumia icc kama njia ya kupata kura za huruma na ndio maana muungano wao ni maarufu sehemu wanapotoka tu.RUTA epuka kucopy na kupaste nakala kutoka kwenye blogs za watu wenye chuki na raila.umekuwa mtu anae eshimika sana humu jf lakini kwa ili umechemsha mkuu.
wewe baridi nimegundua ni wale wale,ebu nitajie nchi ipi ya kiafrica ambayo aishirikiani na nchi za nje.rao kushirikiana na mataifa mengine sio kwamba anatafuta kungwa mkono ili apate urais lakini anajenga mausiano mazuri na mataifa yaliyoendelea for the benefit of the kenya.unakumbuka moi alivyoshindwa kujibu maswali walipoenda ziarani ulaya.bila marehemu Robert ouko (Rip) kumsaidia kujibu maswali it waz a big shame to the nation.mpaka akamuacha kwa asira baadae wakamua yeye na total man wake. wakikuyu ndio walimuua Tom mbuya(RIP) kijana wa watu alikuwa so briliant and up coming politician.kikuyu mafias wakawa na hofu kwamba mboya waz becoming darling wa watu na western countries.uhuru hawezi kuongoza nchi kwa sababu kuu zifuatazo. 1 wakenya hawapo tayari kuongozwa fugitive president and vp.2 familia ya kenyata imegrab land na mali nyingi sana za wakenya.uhuru na ruto wameshindwa kueshimu pact kati yao na mudavadi je watawaeshimu wakenya?.uhuru anasumbuliwa na mashetani dark forces labda msuba.
MKUU KIBARIDI Uliponiacha hoi ni pale unasema raila aelewani na Kikwete,mseveni,nkurunzinza. Sasa Kikwete atamsaidia nini raila,wakati yake yanamshinda,nchi tajiri lakini wananchi maskin,anaulizwa anasema eti ajui sababug. Mtoto wake ndio one of the tycoons wa hapa bongo,wanagrab kila kilichopo,serikali imejaa rushwa kikwete anawaangalia tu. kumbukeni uchumi wenu unategemea maua na utalii.sasa sijui mtauza wapi maua,au watalii mtawatoa wapi,chai mtauza wapi,kumbukeni zimbabwe walinunua hadi mkate milioni moja per loaf of bread.wakati huo uhuru atakuwa anaenjoy maisha.
Akilala akiamka kwa takribani miaka 20 hivi, Raila Amollo Odinga amekuwa hafikirii kazi nyingine ila kuwa Raisi wa Kenya na kuhitimisha lile ambalo baba yake Odinga Oginga alishindwa kulifanya.........kuwa mjaluo wa kwanza kutawala Kenya.
Lakini wazungu wana msemo usemao........................"like father like son"...........................nasi bila ya kuachwa mbali hulonga................."mtoto wa nyoka ni nyoka tu"....................sababu zilizomzuia baba yake Raila kuongoza kenya sasa zimeshamiri na baada ya uchaguzi wa 2013 nguvu ya umma itatimiza uhaja huu ambao umekuwa unahitajika ili kuinusuru kenya kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Hapa ninaambatanisha sababu 10 kuthibitisha mtazamo huu:-
1) Historia hujirudiarudia yenyewe.
Baba yake Raila aliombwa na Mkoloni mwingereza aongoze Kenya mpya lakini kwa kuelewa ya kuwa waliopigania uhuru wa Kenya ni wakikuyu kupitia Maumau na akina Jomo Kenyatta, Oginga alikataa na kudai hakuna kuongelea uhuru hadi Kenyatta afunguliwe kutoka jela. Kauli hiyo ndiyo iliyomsaidia Oginga kuukwaa umakamu wa uraisi na sababu yake kuu hakuwa na mikwaruzano na wakikuyu bali aliwaunga mkono kwenye azma yao ya kukamata dola. Oginga alipokosana na kenyatta basi hata hicho cheo alipokonywa mchana kweupe.
Fundisho hapo ni kuwa kama Raila angelikuwa ana mkakati madhubuti wa kuwa Raisi wa kenya alipaswa kujenga miundo mbinu za nguvu na wakikuyu badala ya kuwabeza kuwa ni wakabila kwa kudai huwa hawachagui mtu yeyote isipokuwa wa kabila lao................na kubeza michango ya wakikuyu kwa kudai katiba mpya ifute kenyatta day na kuiita mashujaa Day...............jingine ni kudai hela ya kenya inamuenzi Kenyatta kwa sababu ni mkikuyu au hata kutohudhuria siku ya kumbukumbu ya kifo cha kenyatta.........
2) Kuunguza madaraja ya kisiasa
Raila alikuwa kinara wa kumkataa Uhuru Kenyatta mwaka 2002 na hata kushawishi baadhi ya viongozi wa Kanu akiwemo Kalonzo Musyoka kuikimbia Kanu na kuisababishia maumivu makali. Pamoja na kufanikiwa kupata kuungwa mkono na wakalenjini katika chaguzi ya 2007 lakini aligombana na William Rutto na hivyo kushindwa kulinda muungano wao na sasa kumgharimu.
Hata akina Rafael Tuju ambao wanatoka kabila lake, Raila amekuwa akiwabughudhi kwa kisa hawamwuungi mkono yeye!
Machafuko ya kujaribu kumpindua Moi mwaka 1982 kwa kiasi kikubwa yalichochewa na Raila na wapo wanajeshi wengi nchini Kenya ambao amejenga nao uhasama kwa tukio hilo na kufanya kuwa ni vigumu kuungwa mkono na majeshi ya Kenya hususani vinara wajeshini...............
3) Kumuunga mkono Kibaki mwaka 2002 bila ya MOU inayoeleweka.
Hata juzi kwenye hafla ya kutangaza muungano wao, Kalonzo Musyoka alimlaumu Raila kwa kuingia makubaliano na kibaki bila ya MOU inayoeleweka na matokeo yake kibaki aliwatimua kazi pale walipokosana naye. Kama wangelikuwa na MOU Kibaki asingeligombea muhula wa pili kama alivyokuwa kawaahidi hapo awali na baada ya kipindi kimoja tajwa, umaarufu wa Raila mwaka 2007 ungelimwezesha kuwa Raisi.
4) Kumsaliti William Rutto Uwaziri mkuu.
Katika makubaliano ya Raila na Rutto mwaka 2007 yalikuwa Rutto lazima awe Waziri Mkuu. Sasa alipoona kaukosa uraisi badala ya kuheshimu makubalino yake na Rutto akamnyang'anya Rutto ugali wake......................kama Rutto angelikuwa waziri mkuu leo Raila angelikuwa ana nafasi nzuri ya kuwa Raisi kwa sababu kura zote za wakalenjini zingelikuwa za kwake..........na kwa kuwa waziri mkuu Raila kawapa nafasi wapiga kura kumpima na utendaji wake haujawafurahisha wengi........................angelijifunza hapa TZ ukimwondoa J.K Nyerere hakuna Waziri Mkuu ambaye aliwahi kuwa Raisi na sababu alitusaidia Sumaye pale alipokuwa anatoa hotuba yake ya mwisho kama Waziri Mkuu na kuwalaumu wabunge kumchukia wakidhani yeye ndiye anawasumbua kwenye majimbo yao..............................somo hapo ni kuwa uwaziri mkuu na mahali pa kumsaidia Raisi siyo mahali pa kujijengea umaarufu wa bei poa wa kuwa Raisi...................Lowassa angelijifunza hapo kama Kawawa alivyojifunza
5) Upendeleo wa ajira kwa ndugu zake (nepotism)
Moja ya mapungufu makubwa ya Raila ni kuwa bunge la Kenya limekuwa likihoji juu ya teuzi nyingi ambazo Raila amekuwa akizifanya serikalini ambazo zimekuwa za kupendelea ndugu zake wa karibu ambayo ni mbaya zaidi ya hata ya ukabila........................yaani hii ya Raila ni "nepotism".
Tatizo ni kuwa watu wanapokuhusisha na kuwabagua ujue kukuchagua wakati wakijua fika huna mpango wa kuwasaidia bali wewe sera yako ni kubeba ndugu zako tu, kukuchagua inakuwa vigumu sana........
6) Kumtegemea Obama na ICC kumpa Uraisi!
Huu ni sehemu ya upumbavu mkubwa kichwani mwa Odinga..........mara nyingi amekuwa akijifananisha na Obama wakati Obama hakulelewa kwenye misingi ya ukabila wa hapa Afrika...........amekuwa akihoji kwanini iwe rahisi kwa wazungu kumchagua mjaluo na Kenya inakuwa shida aisichojua wazungu hawakumchagua Obama kwa sababu ya Ujaluo wake bali kwa kukidhi vigezo vya mahitaji ya siasa za marekani..........period!
ICC imetumika kuwachafua Uhuru na Rutto kwa tuhuma ambazo zilipikwa na wafuasi wa Raila waliomo kwenye NGOs na KNHRC.................na wengineo tunawaona sasa wamekuwa wasemaji wakuu wa kampeni ya Raila na ODM............................tatizo la ICC ni kushindwa kuwafungulia mashitaka Kibaki na Raila. Vilevile ICC wameshindwa kutoa maelezo ya kina kwanini vurugu za Kibera ambako Raila ni mbunge na kisumu hazikufunguliwa mashitaka ICC pamoja na watu wengi kufa na kupoteza mali zao kwenye maeneo hayo? Koffi Annan na fisadi Ken Mkapa wanafikiri ya kuwa wanaweza kutumiwa na Marekani na Ulaya kuishinikiza Kenya kumchagua Raia kuwa Raisi na hivyo kibaraka wa nchi matajiri duniani ziendelee kulinyonya taifa hilo......................wasichojua walinzi wa mwisho wa utaifa wa Kenya ni wakikuyu kama vita vya maumau vinavyotufunza.......................makabila mengineyo aidha yalikaa kimya au yalimsaidia mwingereza kuzima vuguvugu la uhuru nchini humo.
Jana usiku kwenye taarifa ya habari ya saa 3 usiku kwenye luninga ya the CITIZEN, mbunge wa kuteuliwa mwanamama Shebeesh aligusia masuala haya ingawaje alikuwa akiilaumu Ikulu na kibaki kwa kutaka kushinikiza Uhuru aachie ngazi kwa Musalia Mudavadi...............
Uchaguzi huu utamkataa Amollo kwa kuwa ni kipenzi cha ukoloni mamboleo...........
7) Kumnyanyasa Makamu wa Raisi Kalonzo Musyoka.
Raila Odinga katika khali isiyo ya kawaida amekuwa akitumia muda mwingi kupigania "seniority" kati yake na Musyoka.......................akidai baada ya Kibaki ni yeye............nilimshangaa jana kwa mara ya kwanza tangia awe Waziri Mkuu alikwenda kumtembelea Kalonzo ofisini kwake......................siyo kwa sababu anamheshimu bali kumshinikiza awe namba mbili wake kwenye uchaguzi ujao!.............How pathetic!
Unapojikuza ujue Muumba atakushusha tu..........................na Raila katika kudai makuu sasa inabidi aoshe unyayo wa Kalonzo ambaye amekuwa akimdharau sana........................katika miaka 5 iliyopita................na uzoefu unaonyesha mwisho wa yote muungano wao utaishia pabaya kabla ya uchaguzi..................
8) Kuizuia demokrasia kufanya kazi yake ndani ya ODM
Hili linashangaza lakini ni ukweli. Musalia Mudavadi kisa ya kuikimbia ODM ni pale alipobaini katiba yao tayari ilimtamka Raila ndiye mwenye sifa za kugombea uraisi kupitia chama hicho bila ya kuweka utaratibu shirikishi, wazi na ambao utakuwa na misingi ya utu ya kumpata mgombea uraisi wa chama hicho......................
Sasa Musalia kajiunga na mahasimu wa Raila wakiongozwa na Uhuru na "majuto ni mjukuu..............:'
9) Saa ya "Kizazi kipya" imewadia.............
Kutokana na ukweli na bila ya kujali makabila yao, vijana nchini Kenya wamechoshwa na wazee na Raila ambaye ana umri wa miaka 73.............................hana mvuto kwa kizazi kipya...................huo ndiyo ukweli wake.............kuchaguliwa na hiki kizazi cha dot.com ni njozi ya kufikirika tu.........
10) kukabiliwa na kutetea watuhumiwa wa ufisadi.
Moja ya mvuto wa Raila ulikuwa anachukia ufisadi lakini la ajabu alipoingia kwenye meza kuu ya mlo amekuwa akitumia watoto wake kufanya ufisadi kama ule wa kashfa ya mahindi.....................watu walikuwa wanakufa na njaa Raila akaona kivuno kwake!
Swahiba wa Raila, Charity Ngilu alipokuwa kashikwa pabaya na taasisi ya kuzuia Rushwa nchini Kenya.............Raila alikuwa mstari wa mbele kumtetea bila ya kujali mabwawa kibao hayakuchimbwa au yalichimbwa kwa viwango vya chini na mabilioni kutoweka........na miradi ya maji ni nyeti sana katika kumkomboa masikini mnyonge kwenye ufukara wake................Raila alipokuwa upinzani alijiita ni "mkombozi wa wanyonge"................................lakini kila mmoja sasa anajua hizo zilikuwa ni ghiliba..........
HITIMISHO.
1) Kutokana na uchu wa madaraka wa taswira ya Amollo ni dhahiri ya kuwa ni nguvu ya wananchi ndiyo tu itamwondoa kwenye anga za siasa za kenya na Afrika haina muda mkubwa wa kulisubiria hili............kwa hamu kubwa.
2) Kustaafu kwa Raila kwenye anga za siasa za kenya kutapunguza sana misuguano ua kikabila nchini humo.........
Mmh! sikujua kama tunao ndugu zetu wanaozungumzia zaidi ukabila badala ya umoja,
Samahani sisi wa TZ ni wamoja hatujui kabila gani bora kuliko lingine, sikatai ulo sema lkn kwetu hayana tija.
Kibaridi wewe ni mtu ambaye ni hatari sana katika jamii,unauma na kupuliza. Hivi ndugu yako anapoungana na adui yako kukumaliza,utazidi kumchekea tu? Thats was tuju did.kumbuka wakati youthfull mps wakiongozwa na Raila kuingia bungeni kwa mara ya kwanza.alikuepo Tuju,ochilo ayako nk.na bila Raila tuju asingepata ubunge,James orengo ndio alikuwa mbunge wa eneo hilo by that time.lakin orengo alikuwa upande unaompinga odinga akapigwa chini na wanapiga kura wake.kumbuka siasa za kwenu kenya(nimeishi kenya nikiwa nasoma Ku) ni za makabila.kila tribe wana political kingsman wao so anayempinga Raila tena from home land ni traitor huyo....kumbuka Raila ndio alimleta miguna kutoka mafichoni canada,lakin the guy alikuwa hana nidhamu za kiofisi,unakumbuka alivyo missbehave ziarani uganda,unakumbuka alivyograb mic mbele ya wanahabari,unakumbuka alavyokuwa akidemand simu nzuri gari nzuri ofisi nzuri nk.raila akaona huyu hafai ashazoea mambo ya kupigiana kelele mahakamani na wanasheria wenzake sio adminstrator,akampiga chini,eti ndio akaanza kumkashifu raila.je huyo sio adui? ...MKUU KIBARIDI Uliponiacha hoi ni pale unasema raila aelewani na Kikwete,mseveni,nkurunzinza. Sasa Kikwete atamsaidia nini raila,wakati yake yanamshinda,nchi tajiri lakini wananchi maskin,anaulizwa anasema eti ajui sababug.Mtoto wake ndio one of the tycoons wa hapa bongo,wanagrab kila kilichopo,serikali imejaa rushwa kikwete anawaangalia tu.Mtu kama huyo hafai kuwa na urafiki na raila coz ni weak prezo....mseveni ni dikteta ambaye amebaka katiba ya uganda nai kuibadilisha ili atawale milele,mtu kama huyu afai kuwa raila.unakumbuka kisiwa cha migingo bila raila kuingilia kati ingekuwa mali ya waganda siyo yenu tena.....nkurunziza hata asipoelewana na odinga kuna hasara gani?kwanza bado anahangaika kuiconstruct nchi yake yenye makabila mawili tu,na watu wasiozidi milioni 15,yeye bado sana kwenye ulingo wa kisiasa,je mkuu kibaridi unatambua kwamba kuna tetesi kenyatta family wanawekeza biashara zao burundi kupitia kambuni yao ya brooksides na nkurunzinza ndio msimamizi?....wakenya msijidanganye eti you can make it on your own.kumbukeni uchumi wenu unategemea maua na utalii.sasa sijui mtauza wapi maua,au watalii mtawatoa wapi,chai mtauza wapi,kumbukeni zimbabwe walinunua hadi mkate milioni moja per loaf of bread.wakati huo uhuru atakuwa anaenjoy maisha.
RUTA unaweza kuwa mkubwa ki umri lakini ukawa bogus in thinking. Nakala yako umeiandika tarehe 29 Dec.lakini acording to the current political trend in kenya,inaonyesha huna updates whats going on.mudavadi alipokimbia Odm sababu kuu ilikuwa njia itakayotumika kumpata odm flag bearer,huko alipohamia kapakimbia tena,akipingana na njia ya wajumbe aliyokuwa akiidemand odm,je una lolote la kusema abt mm tena?.....RUTA kalonzo na odinga sasa wapo pamoja chini ya mwamvuli wa Cord na wanafanya kampeni zao pamoja.je watambwa hilo? In politics siku zote hakuna rafiki wala adui wakudumu.....RUTA uhuru na ruto ni watoto waliokulia kanu na kulelewa kisiasa na mzee moi,kumbuka moi ndio alimnominate uhuru kuwa mbunge kwa mara ya kwanza na kumpa uawaziri wa local gov,hapo tunaweza sema kanu imerudi kwa njia nyingine,(uhuruto)....RUTA uhuru na ruto wanatumia icc kama njia ya kupata kura za huruma na ndio maana muungano wao ni maarufu sehemu wanapotoka tu.RUTA epuka kucopy na kupaste nakala kutoka kwenye blogs za watu wenye chuki na raila.umekuwa mtu anae eshimika sana humu jf lakini kwa ili umechemsha mkuu.