Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu jaribu kutumia tiba ya dagaa kutibu matatizo kama hayo ya majini na mizimu, nunua zako dagaa wa kutosha kisha utwange hadi upate unga halafu uwe unatia kwenye maji ya kuogea uwe unaogea ni tiba nzuri.Nilishahama mkuu na haya mambo bado yanasumbua
Mzaliwa wa Pili mkuu
Sawa Mkuu nitafanya hivyoMkuu jaribu kutumia tiba ya dagaa kutibu matatizo kama hayo ya majini na mizimu, nunua zako dagaa wa kutosha kisha utwange hadi upate unga halafu uwe unatia kwenye maji ya kuogea uwe unaogea ni tiba nzuri.
Kama hauwezi mtafute mdada mmoja anaitwa Tabibu Lois akufanyie maombi.
Wa kwanza ni WA kiume au wa kike?Mzaliwa wa Pili mkuu
SEMA hapa mkuu,utawaponya wengiMimi nilipitia hali Yako, mizimu hawana nguvu hiyo kama ukijikita kwenye maombi, Mimi wameshanishindwa, nitafute tuongee hata kwa simu
Mkuu hilo ndio suluhisho au huduma ya kwanza?Akili yako haijafungwa wala.
chumba chako kisafishe kwa chumvi ya mawe na wewe pia unaoga na hiyo chumvi ya mawe mara kwa mara.
Achana na habari za waganga utapoteza nguvu zako.
Hama hiyo sehemu kabisa na toa mawazo hayo ya kufungwa.
Nipo kwenye dilema nikubaliane na mambo ya kutambika au niendelee huku niliko upande wa Makanisa, japo kiukweli napata vita kubwa kila napopigana na hizi nguvu makanisani.
Hekima imetumika[emoji120]Option ni mbili hapo, we mhusika uchague unayoona inafaa.
1: Tafuta mzee mmoja anaeeleweka ndani ya ukoo wako, mzee mwenye uelewa wa mambo na busara akueleze kwa kinagaubaga hayo unayoyadhani, faida na hasara utakazopata, akueleze na yaliyomkuta mzee wako...ukiona ni sawa kafanye mambo ya mila (baada ya kuwa ushayapima)
2: Anza upya, anza kwa kujiondolea hayo mawazo katika akili....be positive (hiki ni kitu muhimu sana) usijiwazie gundu na mikosi (ndo unavikaribisha , law of attraction )usiruhusu hayo mambo yatawale akili ukianza tu kuyawaza unaswitch akili iwaze mambo mengine, shiriki ibada kwa imani yako acha kuzunguka zunguka kwenye kila kanisa unaloona. Tiba ya kwanza yaondoe akilini.
Katika hizi mbili zipime zote chagua moja. Kila laheri
Kweli umefungwa na madhabahu ya ukooHabari wana JF, mimi ni new member ningependa mnikaribishe katika Jukwaa letu.
Mimi Ni kijana wa miaka 30’s, kwa mda wa miaka 3 nimekua nikisumbuliwa na Nguvu za giza na Mizimu ya ukoo ambayo imepelekea kuharibu dira ya maisha yangu, nilianza na kuumwa homa za ajabu ajabu, mwili kuchoka, dalili za homa ya Presha.
Nilihangaika sana ikiwemo kwenda kwa waganga wa kienyeji, nikawa napata nafuu lakini baada ya mda hali inarudi palepale, nikajaribu na makanisani ikawa ni vita kali, nako nikawa napata nafuu ila hali inarudi pale pale ikiwa kuhisi mwili unaumwa, kuchoka, macho kuhisi yana kiza na Moyo kuuma sana.
Nilihangaika pia na maombi binafsi ya kujiombea mimi mwenyewe pamoja na watumishi wa Mungu, nikafanikiwa kupunguza hii hali kwa kiasi chake nikapata nafuu.
Kuja kwenu wanaJF ninaomba ushauri kwa sababu nimefungwa upande wa uchumi, akili yangu imefungwa.
Inafika hatua ya kukata tamaa na kuona kila kitu hakiendi na pia kila ninapopata ishu ya kazi au dili lolote hua inafika sehemu mambo yanaharibika, nimekua na roho ya kukataliwa, kila ninapoenda ninadharauliwa na kubezwa, nilishaenda sehemu nikahisiwa mimi ni Mwizi, kiukweli ni kama nina mikosi au gundu.
Siku Moja niliwasiliana na ndugu wa baba ambao wao ni wasukuma, wakaniambia hio kawaida kuna mizimu inabidi kwenda kutambika kwa sababu ukoo wetu tangu enzi ni wa mambo hayo ya kimizimu.
Nipo kwenye dilema nikubaliane na mambo ya kutambika au niendelee huku niliko upande wa Makanisa, japo kiukweli napata vita kubwa kila napopigana na hizi nguvu makanisani.
WanaJF kiukweli nimefika hatua nachanganyikiwa, kila kitu hakiko sawa, nakosa kujiamini kwa kila jambo nalotaka kufanya, ninaomba ushauri wenu na mawazo yenu.
Najua Jukwaa hili lina watu wenye maarifa na maono. Nitashukuru sana
Cc MshanaJR
HayaHoma Sio ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa au shida ya kiroho
Mbona waganga wana maisha mazuri tu na hela nyingi? Mganga maana yake daktari wa asiliKuna kijana tumemzika last year, aliamua kujiuwa tu hakutaka kabisa kukubali kuwa mganga, walikuwa wanamtesa sana kuuumwa tu maisha hayaeleweki kijana wa watu akajinyonga.