Nguzo za umeme za zege sasa ni hatari kwa maisha kuweni makini msikae karibu

Nguzo za umeme za zege sasa ni hatari kwa maisha kuweni makini msikae karibu

Kwahiyo za miti hazidondoki?
Za miti zinadondoka lakini madhara ni tofauti.

Na za mti kabla hata hazijadondoka mtaani mnakua na tahadhari kwasababu zinaonekana kabisa tofauti na hizi za zege si rahisi kugundua.
 
Hapo kuna uhuni, hazina nondo ndani. Mambo ya manunuzi hayo, watu wanajipigia tu, hofu yote imeisha.
 
Makosa ya kibinadamu yapi tena?

Nimewahi kuangalia video ya namna hizi nguzo zinavyotengenezwa, kuna nondo ndani yake, ina maana hapa walisahau?

View attachment 2694302

Kuna mdau aliwalalamikia TANESCO kwa kutengeneza nguzo mbovu mpaka zimedondoka ila TANESCO wamekana kwamba hiyo nguzo iliyoonyeshwa na ITV siyo ya kwao ni ya Kampuni ya Fiber.

Lakini ukiangalia hiyo nguzo unaona kabisa wire ni wa umeme mweusi na umepitishwa kwenye Kikombe vya umeme.
 
Kuna muwekezaji wa ndani, mjumbe wa NEC wa Ccm aliyeongoza kwa kupigiwa kura nyingi Dodoma, anatokea Mufindi, yeye ni Swahiba wa January Makamba, ameahidi kutowa nguzo za miti bure kwenye project ya Rea mkoa Fulani.

Sasa hapa kuna Uturn inaandaliwa kurudi kwenye woods material.
Aisee!!! Wakati mwingine unawaza ...huu uzalendo unaosemwa ni WA namna gani?

Jana nilisikia redio fulani ikimuhoji Mwenyekiti wa wenyeviti wa Chama Fulani alisema, Uongozi wa Chama Chao uliwaagiza kuingiza Viongozi wenye vipato vya kueleweka.
----
Mkuu nadhani uweza kubashiri ni chama gani! Ha ha haaaa!
 
Kudondoka kwa nguzo za umeme za zege imekuwa kawaida kabisa. Mimi mwenyewe nimeshuhudia nguzo mbili Moja ikijeruhi mtu akiwa ndani ya gari.

Wahusika wawataarifu wananchi wasisogelee hizi nguzo. Ni hatari hazina vyuma ndani yake. ikipata unyevunyevu tu inaanguka.

Mimi nilishangaa engineers waliyozitengeneza hizi nguzo hazina expansion joints. Sasa sijui technology iliyotumika hapo ni ipi. Mimi ninavyojua hizi hazidumu kabisa.

Kuna nguzo za umeme za zege zilijengwa kwenye Reli ya kati. Zile nguzo kwakuwa hazina expansion joints zilibubujika zikabakia vyuma.

Hawa sijui wanatumia science gani. Ukipita kwenye madaraja yote, barabara ya mwendokasi na sehemu nyinginezo. Huwezi kuweka zege kwenye jua bila expansion joints. Hayanihusu.

Video hii hapa nguzo imeanguka


Walio idhinisha hiyo tenda wanatakiwa wawajibike! Mradi muhimu hivyo unawezaje kubwa na makosa ya kiinjinia kiasi hicho?
Nguzo za aina hiyo zilipaswa zijaribiwe na kujiridhisha sasa shaka kwamba hazina madhara kwa mazingira na kwa watu!

Wanaoathirika inawapasa wadai fidia mahakamani!
 
Kipindi cha magu walikuwa wana weka ndondo zile nyembamba zinakuwa imara sahivi wamechakachua ni noma
 
Ukute wahusika wa ubora wameshakula Chao wako kimyaaa tuuuuuu utadhani sio wao wanaohusika
Kuna wanaojiita OSHA, Kuna ERB, Kuna CRB Kuna taasisi nyingi za usalama WA structural things, wote wamepata kimya, Sijui wanataka ziue wangapi
 
Watu waliopoteza ndugu zao na mali zao waishitaki serikali kwa uzembe!
 
Kuna mdau aliwalalamikia TANESCO kwa kutengeneza nguzo mbovu mpaka zimedondoka ila TANESCO wamekana kwamba hiyo nguzo iliyoonyeshwa na ITV siyo ya kwao ni ya Kampuni ya Fiber.

Lakini ukiangalia hiyo nguzo unaona kabisa wire ni wa umeme mweusi na umepitishwa kwenye Kikombe vya umeme.
Inawezakana ikawa sio yao, binafsi nilishangaa sana, maana DERM kazi zao nazifahamu, wako serious kwenye hii project.
 
Inawezakana ikawa sio yao, binafsi nilishangaa sana, maana DERM kazi zao nazifahamu, wako serious kwenye hii project.

Basi Serikali inabidi ifanye mpango kabambe a kuwaambia hao watu wa fiber waondoe hizo Nguzo za magumashi zisije kuleta maafa zaidi......Nguzo gani za zege hazina hata nondo ndani au hata mesh wire?
 
Hii nchi bana. Upigaji tu kila kona. Enzi za Nguzo za Miti eti ilikua inaandikwa iko imported from South Africa kumbe inatokea tu Iringa hapo. Tumeingia kwe zege napo upigaji.
 
Back
Top Bottom