Ng'wanakapolo mwanamke aliyetetemesha Magu. Misukule yake ya Kihindi na Kizungu iliwashangaza wengi

Hapo ndio naonaga uchawi hauna maana, kumbe mwisho wa siku hata yeye anakufa!!
 
Ana bahati hakukutana na watu wa Mungu mwenye nguvu wangemsambaratisha na uchawi wake ungeisha
Hao watu walikuwa wapi. Mtu anajulikana Magu, Bunda, na Mwanza na huko kote kuna watu wa Mungu, walikuwa wapi kumshughulikia. Kila mtu ana nguvu zake, wa Mungu ana zake na wa Shetani ana zake. Hii ndiyo maana wacha Mungu wasipofanikiwa wanaingia nguvu za giza, na wa nguvu za giza wakipoteza nguvu wanakimbilia makanisani au misikitini.
 
Umenikumbusha mbali sana kutaja ivyo vijiji
 
Na yule DC aliyeamkia mlimani vipi?
 
Mhuuuuum ya kweli haya jamani. Ila umenikumbusha Mheshimiwa mbunge Malaki Lupondije,Mungu aendelee kumpumnzisha kwa amani.
Nakumbuka kipindi icho cha uchaguzi nilikuwa magu. Kuna wimbo flani wa kampeni hadi Leo naukumbuka licha ya kuwa nilikuwa chalii. "humulaga malaki abhano bhose watongilwe limbu tulekotinda"
 
Sijui sana kuhusu Kanda ya ziwa na sijawahi fika ila kuna mtu aliniambia kama una mambo yanakusumbua unahitaji msaada extra nenda Kanda ya ziwa. Nasikia huko ni balaa mwisho wa matatizo. Kuna ukweli wowote katika hili?!
Inategemea. Ukuryani ni mapanga na sime. Huko (Ukuryani) uchawi si mali kitu, maana ukileta chokochoko ku"ghecha" ni njenje. Ukienda Majita, dili kubwa ni ubishi. Wajita wanaongoza kwa kubisha. Ukifika Zanaki, angalia saana. Afadhali umchukulie mtu mke wake kuliko kumchukulia mpenzi wenyewe wanaita "muyangi" au "mmyangi". Ukijulikana unamtafuni muyangi atafika kwako usiku na kuku. Atamtekenya kuku apige kelele. Ukisikia utakurupuka kutoka unadhania kuku wako wanaliwa anakutia mshale na kuondoka akisema "ubhuryare bhukuryare, ubhikari bhughwikari. Kamura ka Zaza untarahire kungheghera omuyangi" Kwa kifupi Mzanaki anathamini saana muyangi...mengine baadaye
 
Nakumbuka kipindi icho cha uchaguzi nilikuwa magu. Kuna wimbo flani wa kampeni hadi Leo naukumbuka licha ya kuwa nilikuwa chalii. "humulaga malaki abhano bhose watongilwe limbu tulekotinda"
Mzee lupondije yeye alikuwa hana maneno mengi, ni pesa tu, yeye limbu anatumia elimu yake kuwaomba kura wananchi!!shule za sekondari kama BULIMA, MAGU DAY, KINANGO, wanafunzi walifaidi sana, zilikuwa ni ng'ombe na magunia ya mchele tu, na kuna mwanaye mmoja ndiye alikuwa dreva wake mbwembwe nyingi sana!!!
 
Nimekaa maeneo uliyoyasema, jamii hizi si masikini kama unavyosema. Ni wakulima wazuri, wafugaji na wafanya biashara. Kuna wasukuma wanafedha na wengine wanamigodi mikubwa tu ya dhahabu na almasi. Ila huwezi kuta msukuma anajisifia, au kujionesha kwamba ni tajiri. Hawa upenda maisha ya kawaida, japo wana hela.

Unakuta mtu ana ng'ombe wengi, ardhi kubwa ya kulima, wanakula vizuri, ndo maana miili ya kisukuma ni mikubwa, hivi wangekuwa masikini hiyo afya wangetoa wapi? Wengine ni tajiri wa biashara za samaki. Huo umasikini unao usema ni upi?
Mie nachoona kwa wasukuma uwa hawaachi mila zao za kuwa na nyumba za nyasi. Hata ukikuta kajenga nyumba ya bati nyasi lazima iwepo na hasa vijijini. katika nyumba hizo za nyasi ndiko wanakofanyia matambiko yao.
Mwanza, Kahama, Geita, Bariadi, Shinyanga, wasukuma wana fedha, lakini uwezi kuta hata siku moja mtu kaitwa Billionea, au kufahamika ana hela. Wasukuma ni wanyenyekevu, mpaka umchokoze ndo utajua ukorofi wao.
 
Mwafrika hawezi kumroga mzungu

Hilo na kuwaweka msukule wazungu ni CHAI.
Kuna eneo moja Geita ukiwa unaelekea Msalala, kuna makaburi mengi ya wazungu. Wanasema hilo eneo ndiyo palikuwa pajengwe Chuo Kikuu ambacho kipo Uganda, kikitambulika kwa jina la Makerere. Katika hilo eneo ni pazuri sana pana mvuto.
Ila wenyeji waliwaroga wazungu na kuwauwa, kiasi kwamba walikimbia na kuhamia Uganda ambapo walianzanisha Chuo cha Makelele. Hilo eneo lipo waweza fika Msalala ya Geita na kupata historia. Kuna makaburi mengi sana ya wazungu. Walikuwa wanarogwa na kufa kibao wakakimbia hilo eneo.

Usukumani hawa wanaamini sana mambo ya uchawi ni utamaduni wao. Miaka ya nyuma kule Bulima au Sogesca waliuwawa wazungu wengi kwa uchawi. Maeneo ya Nyashimo kulikuwa na wahindi wengi sana. Huko kulikuwa na misukule kibao.
Kama umesoma historia ya mwanamalundi huyu wajerumani walimuogopa kwa miujiza aliyowafanyia. Alifungwa lakini akawa anavuka bahari kama Musa na kwenda kustarehe kariakoo na sehemu mbalimbali wakati huo. Walitaka kumnyonga wakashindwa. Huyu alikausha miti kwa kuonyoosha kidole, aliacha alama za nyao zake katika miamba mingi sehemu mbalimbali za Tanzania. Mzungu hana ujanja kwa uchawi wa mwafrika. Huyu Mwanamalundi kwao wangemwita Mtakatifu kwa miujiza alofanya.

Namfahamu mama mmoja alikuwa missionari huko kusini jombe, huyu alilogwa tena miaka ya hivi karibuni. Akaenda Ulaya ugonjwa hauonekani, lakini hali mbaya akaambiwa na wenyeji atibiwe kienyeji, alisurrender na kutibiwa kienyeji na kupona. Karejea yuko kwao Ulaya. Hii ni story ya kweli. Make alileta dharau kwa wabena wakamtengeneza. Hivyo si kwamba mwafrika hawezi mloga mzungu.
Siku hizi Ulaya wanaamini katika uchawi wanasafiri kwenda kununua uchawi. Na mzee mmoja mzungu ni rafiki yangu huyu ni mchawi. Alienda Meddetranian kununua uchawi, kauwa watu wengi hasa wachungaji. Alinipa historia kwanini aliamua kuwa mchawi. Na kaanzisha dini ya uchawi anawafuasi kibao ulaya na maeneo mbalimbali duniani. Wazungu wanamuogpa sana huyu mzee. Alinambia Ulaya wanaheshimu na kuogopa uchawi toka Africa, kwa sababu unanguvu na Africa ndo mama wa uchawi. Story yake ni ndefu sana. Pia kuna shemeji yangu ni mzungu, huyu dada utokewa na mizimu ya kwao na mamake, yeye utoa ramli na kuongea na watu walokufa. Huko Romenia uchawi ni mkubwa sana.
Uchawi umeongelewa katika vitabu vitakatifu, upo na unanguvu si jambo geni. Uchawi ni nguvu za kiroho, ila waafrika tunadhani ukisema uchawi haupo, utaonekana weye ni wakisasa. Uchawi upo na hata wazungu wapo wachawi, waafrika wapo wachawi, wahindi wapo wachawi na hata wachina. Kikubwa kama una imani ya Mungu endelea kuamini. Na uhakikishe kama unamshika Mungu mshike kwelikweli.
 
Walikuwa wanarogwa ama ni hali ya hewa na zile tropical diseases tulisoma ktk history 😅
 
Miaka ya nyuma alikuwepo bwana mmoja akiitwa Lupondije (Malaki). Aliitwa jina la MALAKI kwa kuwa alikuwa na malaki ya ng'ombe .
Kwenye jina mkuu umetudanganya! Hauitwa MALAKI kwa sababu ya kuwa na ng'ombe wengi bali hilo jina ni la Wa-AIC ambalo ndilo lilikuwa dhehebu lake. Jina lake kamili ni Malaki Levi Lupondije!
 
Walikuwa wanarogwa ama ni hali ya hewa na zile tropical diseases tulisoma ktk history 😅
Hali ya hewa pale ni Ubaridi, make ingekuwa hali ya hewa wazungu waliokuwa Dar es Salaam, au Mtwara huko nao wangekufa sana kwa hali ya hewa. Pia haikuwa tropical diseases. Unajua sikueleza kwa undani, ila ukitaka historia fika eneo husika, utajiuliza kwanini makaburi yalikuwa eneo hilo tu? make ingekuwa hali ya hewa Geita mjini kulikuwa na wazungu kibao tu hata Mkuu wa wilaya enzi za ukoloni alikuwa Mzungu nao wangekufa. Vifo vyao vilitokea kwa kupukutika kama kuku. Na wanasema wakazi wa eneo hilo walikuwa wachawi sana, na walitumia mayai kuwaroga. Maeneo hayo ni baridi na kunamisitu.
Waafrika tunatabia ya kukataa historia yetu, na kuamini katika wazungu. Tunadhani kila asemacho mzungu ni kweli. Ati historia yetu tunaandikiwa na mzungu basi ndo tunaona ni kweli. Kwa mawazo uloyatoa hata kisayansi haiwezekani. Kwanini eneo la ugonjwa liwe katika kijiji kimoja tu tena kwa wamissionary walioishi maeneo ya kanisani. Wakati hali ya hewa ni eneo zima kwa wilaya husika. Tungeona vifo vinatokea katika wilaya yote ya Geita hapo tungesema sawa. Laikini pia historia ya eneo hilo inajulikana hata na halmashauri ya wilaya, je hawani wajinga kutojua kilichotokea? Mpaka wahifadhi historia ya uongo? Tafakari!
 
Mimi iyo history ya ivo vifo siijui mkuu nimefanya tu kujiuliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…