Ng'wanakapolo mwanamke aliyetetemesha Magu. Misukule yake ya Kihindi na Kizungu iliwashangaza wengi

Daaaa!!umenikumbusha mbali sana mkuu, huko ILUNGU, ICHOBELA, KINANGO, NYAMATALA, KAHANGARA!!na huyo mzee LUPONDIJE, alikuja kugombea ubunge wa jimbo la magu 1995, akichuana na Dr.limbu, mzee hata elimu hakuwa nayo ila alikuwa ana mwaga pesa ile mbaya, na alifanikiwa kushinda!!ni kweli nakumbuka haoo magu miaka ile ni yeye tu ndiye alikuwa na ghorofa!!na kwa nje kidogo hapo pembezoni ma barabara ya kwenda msoma alikuwa na zizi kubwa sana la ng'ombe!!!
Lupondje na bana bakwe (mabasi)
 
Ng'wanakapolo tafsiri yake ni mtoto wa Kapolo. Kapolo ni muhogo usio na uchangu, muhogo mtamu.

Miaka ya 1970s hadi 2000 jina hilo lilivuma sana kwenye mji wa Magu uliopo mkoani Mwanza.

Hata kama hukubahatika kumuona kwa macho hakika jina lake ungelisikia tu likivuma maana huyu ndiye aliyewaweka pangoni kwenye vilima vya Nyambitilwa misukule mbalimbali hadi ya kihindi na kizungu.

Miaka ya nyuma alikuwepo bwana mmoja akiitwa Lupondije (Malaki). Aliitwa jina la MALAKI kwa kuwa alikuwa na malaki ya ng'ombe .

Huyu bwana aliamua kujenga jengo la ghorofa kumi pale Magu mjini. Akaanza ujenzi na akiwa anaendelea , Ng'wanakapolo akamfuata akamwambia ghorofa lako liishe hapo, unatuletea mambo ya kigeni (mashikolo mageni) ili iweje? Hapo ujenzi ulikuwa umefika kwenye ghorofa ya nne.

Bwana Malaki hakuwa mkaidi, aliamua aachane na ujenzi ili kuinusuru nafsi yake.

Ng'wanakapolo anatajwa kuhusika na kuwachukua msukule wazungu wawili ambao walikuwa wanajenga barabara ya Mwanza kwenda Musoma.

Wazungu hao walipotea kimiujiza na hawakuonekana tena hadi baada ya miaka kadhaa misukule ya bibi Ng'wanakapolo ilipobainika kwenye milima ya mawe ya Nyambitilwa.

Huko walikamatwa fisi wengi sana wakiwa wamevalishwa hirizi na nguo. Pia ilikutwa misukule mbalimbali wakiwemo wazungu wawili wa Sogesca, muhindi mmoja na Waafrika zaidi ya kumi na tano.

Licha ya Magu kuwa na wafanyabiashara wengi wakubwa wa mifugo na samaki bado wanaogopa kujenga maghorofa kwa kuogopa kulogwa.

Kifo cha Ng'wanakapolo kiliacha gumbo kubwa hapo Magu kwani watu hawakuamini kwamba Ng'wanakapolo anaweza kufa siku moja kutokana na nguvu zake na ubabe wake wa kichawi.
Ilikuaje iyo misukule ikapatikana?
 
Huwezi mshinda shetani kama huna Mungu ndano yako.
Kupigwa chale ni kusajiliwa kuzimu,chale ni lazima itoke damu,ile damu inaenda kuzimu kama kiapo cha maagano ya mkataba Kati yako na shetani kupitia mganga ambae ni wakili wa shetani duniani.Chale ni muhuri au sahihi ya kuingia mkataba na majini yatende kazi kusudiwa.
Yani chale ni kama umewasha bluetooth..unaonekana kirahisi kwenye rada zao.
 
Ng'wanakapolo tafsiri yake ni mtoto wa Kapolo. Kapolo ni muhogo usio na uchangu, muhogo mtamu.

Miaka ya 1970s hadi 2000 jina hilo lilivuma sana kwenye mji wa Magu uliopo mkoani Mwanza.

Hata kama hukubahatika kumuona kwa macho hakika jina lake ungelisikia tu likivuma maana huyu ndiye aliyewaweka pangoni kwenye vilima vya Nyambitilwa misukule mbalimbali hadi ya kihindi na kizungu.

Miaka ya nyuma alikuwepo bwana mmoja akiitwa Lupondije (Malaki). Aliitwa jina la MALAKI kwa kuwa alikuwa na malaki ya ng'ombe .

Huyu bwana aliamua kujenga jengo la ghorofa kumi pale Magu mjini. Akaanza ujenzi na akiwa anaendelea , Ng'wanakapolo akamfuata akamwambia ghorofa lako liishe hapo, unatuletea mambo ya kigeni (mashikolo mageni) ili iweje? Hapo ujenzi ulikuwa umefika kwenye ghorofa ya nne.

Bwana Malaki hakuwa mkaidi, aliamua aachane na ujenzi ili kuinusuru nafsi yake.

Ng'wanakapolo anatajwa kuhusika na kuwachukua msukule wazungu wawili ambao walikuwa wanajenga barabara ya Mwanza kwenda Musoma.

Wazungu hao walipotea kimiujiza na hawakuonekana tena hadi baada ya miaka kadhaa misukule ya bibi Ng'wanakapolo ilipobainika kwenye milima ya mawe ya Nyambitilwa.

Huko walikamatwa fisi wengi sana wakiwa wamevalishwa hirizi na nguo. Pia ilikutwa misukule mbalimbali wakiwemo wazungu wawili wa Sogesca, muhindi mmoja na Waafrika zaidi ya kumi na tano.

Licha ya Magu kuwa na wafanyabiashara wengi wakubwa wa mifugo na samaki bado wanaogopa kujenga maghorofa kwa kuogopa kulogwa.

Kifo cha Ng'wanakapolo kiliacha gumbo kubwa hapo Magu kwani watu hawakuamini kwamba Ng'wanakapolo anaweza kufa siku moja kutokana na nguvu zake na ubabe wake wa kichawi.
Masimulizi ya kijinga kama Yale ya kinjekitile ngwale kubadilisha risasi kuwa maji.
Sasa huyo mchawi wa kisukuma ameacha nini Cha kujivunia huko usukumani?
Kuanzia mbogwe,Geita,Kahama mpaka Tabora?zaidi ya umaskini tu,
 
Back
Top Bottom