NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

Tatizo la hii Bima ya Watoto ya shilingi elfu 50,400 tulikuwa tunachagua mno watoto wa kujiunga, yaani nina watoto watatu basi nalipia yule mtoto tu anayeumwa, sasa kwa mtindo huu lazima mfuko ungeelemewa na wagonjwa.

Yaaani ni kama una gari unasubiri ipate ajali ndiyo uikatie Bima, hapa NHIF walijitia kitanzi wenyewe.
 
Sababu haijasemwa?
 
Kitu gani kilifanya mswada wa UHC usiingie bungeni
 
 

Attachments

  • IMG-20230313-WA0134.jpg
    52.8 KB · Views: 23
TAARIFA KWA UMMA
 
Taarifa ya Mfuko wa Bima inasema Inafanya Maboresho lakini pia wazazi wanaweza kuendelea kuwasajili watoto wao kupitia mashuleni nk. lakini inatakiwa watu wajue mwarubaini wa haya yote yanayoonekana ni changamoto ni mfumo wa Bima ya afya kwa wote.

Huu ni Utaratibu mzuri sana, Serikali imechelewa mfumo wa bima ya afya kwa wote unatakiwa kuharakishwa kwani utakuwa ni mkombozi wa mambo mengi tunayoyaona ni gharama hivi sasa, tena tuleteeni Bima ya Afya kwa Wote TUPONE. Maisha yaendelee tuwe na uhakika wa Matibabu kabla ya kuugua.
 
Wameepusha ubaguzi ... saivi kata familia tu ... watoto kwa 50,400 unapata huduma mpaka milioni 20, we ulisikia wapi duniani. Okoa mfuko
Kwani serikali si inatoa subsidy? Kama inatoa subsidy manake inasaidia wananchi wake kupata huduma za matibabu kwa kuchangia kiwango kidogo.

Hivi ni eneo gani serikali yetu inatoa subsidy? Mbolea..haha
 
Mkuu, BIMA YA AFYA KWA WOTE ni myth tu, hakuna kitu kama hicho na kwa taifa kama Tanzania ni kama haiwezekani tu.
 
Bima ya afya kwa wote itajibu maswali mengi sana ambayo wananchi tunajiuliza kuhusu bima ya Afya. Serikali inatakiwa kufanya kadri wawezavyo kutuharakishia Bima ya afya kwa wote
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-13 at 5.31.46 PM.jpeg
    52.8 KB · Views: 26
Mkuu, BIMA YA AFYA KWA WOTE ni myth tu, hakuna kitu kama hicho na kwa taifa kama Tanzania ni kama haiwezekani tu.
Ukisoma Muswada na kuuelewa utajua kuwa kucheleweshwa kwake ni kwa sababu kuna Majitu yanataka kunufaika kwa kuwepo na mifumo mingi ambayo inatengeneza mianya ya upigaji na huduma zinakuwa hafifu lakini Serkali ikifanya centralization ya mfumo ikawa huduma ya Bima inakuwa NHIF Ndio Mama na Bima ya afya kwa wote ikapitishwa tutakuwa na uhakika wa Matibabu Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…