NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

Lengo wanataka waondoe mchangiaji mmoja mmoja, wanataka waweke nguvu kwenye shule kila mwanafunzi lazima awe na lazi, wakifanya hivyo watapata wachangiaji milioni 10 kwa mwaka ambao watagenerate zaidi ya Bilioni 50

Lengo lao ni wachangiaji wawe wengi.

Wanaondoa ile ya mtu 1 kukatiwa
 
Point dhaifu mno.
 

Mfuko wa Bima ya Afya haujafuta Toto Afya kadi bali unafanya maboresho katika utaratibu wa usajili, tusome taarifa vizuri na katika kipindi hicho mfuko umetoa utaratibu mbadala
 
Maboresho katika Mfuko wetu wa Bima ni muhimu ili kutoa huduma bora kwa wananchi, inapotokea maboresho yanahitajika hatuna budi kuunga mkono jitihada hizi.
 
Mfuko haujaacha kusajili watoto na bima ya afya. Utaratibu wa kusajili watoto unaendelea kupitia familia au shule wanazosoma.
 
Haaa kakwambia nani, uamuzi huu umekuja kwa kuchelewa. Vifurushi vya familia au kaya na kupitia shuleni ndio mpango mzima. Keep it up Mama SSH tupo pamoja. Bi mkubwa tuletee Bima ya afya kwa wote watu tule Maisha huku tukiwa na uhakika wa matibabu.
 
Tanzania wote wanatibiwa

Mtu akishapata tu kadi ya bima kesho yake anaenda hospitali hata kama hana anachoumwa ataenda tu aseme anahisi mafua na homa
Hahahha Tuache kuji understimate kiasi hiki jamani mbona NHIF Wamejikita kwenye kutoa elimu sana. Halafu watanzania wa Leo sio wale wa miaka ya 70&60 wa leo ni werevu na waelewa sana.
 
Asanteni NHIF mi nimependa sana utaratibu wenu wa watoto kusajiliwa kupitia shule wanazosoma aisee hii imetulia kwanza mmetuondolea usumbufu wa kufuata hiyo huduma mjini sisi tuta dili na walimu wakuuu mashuleni kwetu
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-03-13 at 5.31.46 PM.jpeg
    52.8 KB · Views: 17
Mfuko unapumlia mashine upo hoi bin taabani.

Kuna zoezi la uhakiki wa wanachama linakuja soon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…