Ni aibu Diamond kukosa Milioni tano ya Matunzo ya Mtoto. Aache kuzaa tu

Ni aibu Diamond kukosa Milioni tano ya Matunzo ya Mtoto. Aache kuzaa tu

Yanawezekana kama hizo pesa ni zako na umeamua kuzitumia hivo, ila sio kwa kutegemea pesa ya kuomba....
Hata hivo hamisa anataka pesa ya kufanyia show off instagram
hizo pesa ni kwa ajili ya matunzo ya mtoto na mama yake
 
Msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz, amedai mahakamani kuwa hana uwezo wa kumlipa Mwanamitindo Hamisa Mobeto, Sh milioni tano kama gharama za matunzo ya mtoto kwa mwezi.

Diamond amewasilisha majibu hayo katika Mahakama ya Watoto Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobeto kumfungulia kesi ya madai katika Mahakama hiyo ya watoto akidai mambo mbalimbali ikiwamo matunzo ya mtoto.

Katika majibu yake Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa kulipwa kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa hawezi kuzimudu.

Mobeto katika maombi yake kupitia mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Godluck wa Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys, anaiomba mahakama imwamuru Diamond kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa kumsababishia madhara yaliyoishtua familia yake.

Baada ya kupokea majibu hayo mahakama iliahirisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Mobeto kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya mtoto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezeka hivyo aliamua kulifikisha suala hilo mahakamani.

Eti Msanii mwenye hela nyingi mara ajiite Dangote, kumbe ni mbwembwe tu hana kitu.
Kasome sheria kwanza ujuwe inaeleza nini kabla hujajurupuka kuchangia. Isitoshe jambo hili liko mahakamani, hivyo kujaribu kuingilia swala ambalo bado halijaamuliwa kisheria pia ni kosa. Yako mambo mengi ya kuuelimisha umma, usikomalie maisha binafsi ya mtu.
 
Atalipa tu hakuna namna usijione fahari kuzaa watoto ukubali na matokeo atakutana na sheria
 
Iwe isiwe ila milioni 5 Kwa mwezi.hizo ni hela nyingi.unafanya mtoto kama mtaji wako. Kulipa anatakiwa diamond alipe ila sio Kwa milioni 5.hamissa inabidi na yeye ajitume.
Hapa wazazi wetu wametulea Na kutusomesha hadi nasisi tumeaza Maisha na tumeajiliwa wanalipwa mishahala Chini ya milioni mbili. Leo tena unakuta mmezaliwa watano. Leo bado waajiliwa na degree zao wanalipwa bado Chini ya miloni mbili nawanajenga,wanasomesha wanafurahia Maisha sasa mtoto mmoja milioni tano hapo unaona kuna tatizo ndio maana wana wake wanaogopwa na wenye Pesa huwa wanacho fuata ni pesa sasa kunasehemu zingine Pesa haitoki kizembe.
 
Ndo madhara ya kutembea na mademu njaa....yani kwa makusudi anategeshea mimba...
Afu diamond sio kama anakosa iyo 5m...ila kwanini ampe hasa iyo hela??? What for???
 
Wewe unayeona ni aibu, hebu tuwekee hapa mchanganuo wa Sh.5000,000 kwa mwezi kwa mtoto mmoja!!!!

Tanzania hii inafahamika wazi kwamba, baba anayepokea mshahara wa Sh. 5000,000 basi atakuwa ni miongoni mwa baba ambae familia yake itakuwa inaishi maisha safi kabisa.... familia mzima, itaishi vizuri kwa 5M!!!

Sasa ndugu, tupe huo mchanganuo wa pesa inayoweza kuhudumia familia mzima vizuri sana lakini hii leo ionekane hiyo inatosha kwa mtoto mmoja tu!!!!
Mkuu milioni tano ni nyingi sana mzee alikuwa anapokea milioni moja na laki nane tulikuwa tunaishi poa kabisa kusoma na kila kitu hii milioni tano duuu
 
Kuna rafiki yangu alizaa na demu msumbufu yule mwanamke alimsumbua matumizi kufuata kazini anamletea mtt yani alimtesa paka yule jamaa alikuwa anaomba yule mtt ata afariki na yule mtt alifariki kweli nikashaangaa siku ya msiba analia tena
 
Mtoto mchanga kwa mwezi 5ml je akianza shule ya awali kwamezi ikatakuwa bei gani? Tuache kutangaza umasikini tulio nao

Niaibuuuuu
 
Unafkiri mondi angekua maskini angekubali kuwa mchepuko kwa miaka9?au angekubali kuzaa nae mondi alifanya kosa tu la kutokumsoma Huyo demu ni wa aina gani angemjua vzr nadhan hata kusimamisha asingesimamisha
 
Back
Top Bottom