Ni aibu gani uliipata kwenye Interview yako ya Kwanza? Mimi yangu hii

Ni aibu gani uliipata kwenye Interview yako ya Kwanza? Mimi yangu hii

AIBU NILIYOIPATA KWENYE INTERVIEW YANGU YA KWANZA.

Anaandika Robert Heriel.

Simulizi hii ni ya kweli, nimekumbuka tukio hili nikabaki nacheka Sana, naomba nishiriki pamoja nanyi huenda kuna atakayepata somo.

Baada ya kumaliza elimu ya Chuo kikuu nikaamua kuwa fundi cherehani, nikiwa nashona nguo, Fani ambayo nilijifunza tangu nasoma mwaka wa Kwanza pale UDSM. Nilijifunza kushona nguo Kama Fani ya akiba na dharura ikiwa mambo ya elimu yaliniendea mrama, namaanisha kama nisipoajiriwa niwe na pakukimbilia. Basi nikiwa pale Sinza KWAREMI, nikamuomba Fundi mmoja ambaye Kwa miezi sita niliunga urafiki naye, nikamsihi anifundishe kushona hata Kwa kumlipa pesa.

Fundi akaona namzingua Kwa hoja kuwa Mimi ni msomi wa Chuo kikuu wapi na wapi na Kushona nguo, hoja ya pili ni muonekano wangu, fundi alidai muonekano wangu haufanani na kazi ya ufundi nguo, isipokuwa napaswa kuwa katika Ofisi zenye viyoyozi. Basi baada ya Mimi kung'ang'ania Kwa majina kadhaa alikubali.

Basi nikajifunza Kwa bidii kila nilipokuwa natoka Chuoni au pasipokuwa na vipindi, ingekuwa ngumu kunikuta Mabibo Hostel au mti mdigrii au love horizon au vimbwetani nikipiga Stori Kama hakuna vipindi.

Baada ya kubobea kwenye ufundi huku pale mtaani wakiniita FUNDI UCHWARA kutokana na Kauli aliyoitoa Tundu Lissu kipindi kile kuhusu Dikteta uchwara basi nami wakawa wananitania hivyo. Huku wamama wa mtaa ule wakinipa nguo zao za viraka.

Fundi Godfrey (Mungu akubariki) alichukua pesa ya miezi miwili tuu, lakini miezi mwingine akasema Haina haja Mimi kulipia, basi Mimi kazi yangu ikawa kuwahi Asubuhi Asubuhi kufungua ofisi Kwa maana yeye alikuwa anakaa Mbezi mwisho hivyo alikuwa akichelewa.

Saa mbili nilikuwa nimeshafanya Usafi nikiendelea na kazi za ushonaji Kama Ratiba ya siku hiyo ilivyo, Ila nisikatae ukweli kuwa moja ya sababu ya kuwahi kufungua mapema ni kupata wateja WA viraka nijipatie Pesa. Na kweli nilikuwa nikipata, hela ambayo ilikuwa ikinikimu nje ya pesa za bumu ambalo nilikuwa nikizihifadhi Kwa mipango yangu.

Baada ya miaka mitatu nilimaliza shahada ya Kwanza, nilifurahi, nilimshukuru Mungu kwani ilikuwa ni moja ya ndoto yangu tangu ningali mtoto kuwa siku moja NAMI niwe msomi WA elimu ya juu Kabisa.

Sasa muda wa kurejea nyumbani(Makanya) uliwadia. Nani angekubali Kurudi nyumbani?
Wote twajua vijijini hakuna fursa nyingi kama huku mjini, wote mjini kwa sehemu kubwa ndio elimu inaweza kuwa applicable kuliko kijijini. Kijijini labda ishu ya kilimo na mifugo lakini mambo mengine ni uongo tuu.
Utafungua Tuition lakini wanakijiji hawatakuwa na pesa ya kuwapa watoto wao ili wakulipe.
Utafungua Zahanati lakini utamuajiri nani Kwa Mshahara upi akae kijijini, wanakijiji waliozoea kutumia miti Shamba au kusingizia wamelogwa watakujaje kwenye zahanati yako, labda waone magonjwa makubwa.

Nikakaa mjini nikiendelea na harakati za ushonaji huku nikiipigia Hesabu akiba ya pesa ya bumu niliyokuwa nimejibana nikiwa nasoma, haikuwa pesa mingi, ilikuwa 2.3M.
Nikafungua biashara Maeneo ya Tegeta.

Huku nikiendelea kupata shinikizo kuwa nirudi nyumbani, wazazi wakitaka kujua nafanya nini, nami nikawa nawaficha ili wasiniombe pesa [emoji3][emoji3] ingawaje mara moja Kwa miezi miwili mitatu nilikuwa nawatumia hata elfu 50 lakini siongopi, nikiwatumia hiyo ndio ntolee mpaka miezi sita huko[emoji24][emoji24] sio kwamba nilikuwa napenda Bali majukumu hayana uwiano mzuri na kipato.

Shinikizo la kuajiriwa likawa kubwa,
"Ajiriwa wewe!"
"Hivi una akili, ajiriwa, hujasoma ili uwe fundi nguo"
"Wewe utakuwa umelogwa mbona wenzako wanaajiriwa, wewe tuu ndio huzioni Ajira?
Kwa kweli maneno ya kushinikizwa yalikuwa yanatoka pande zote, sio mchana sio usiku.

Kila nikiwaelewesha hawakuwa wanaelewa, nawaambia Ajira Hakuna nilianza kutafuta Ajira tangu nipo mwaka WA Kwanza Kama sehemu ya kufanya uchunguzi wangu kuhusu upatikanaji wa Ajira, sehemu zingine nikawa nawaambia wasinilipe chochote Mimi niwe nachapa kazi nitatumia pesa zangu kwani Mimi bado nasoma Chuo, lengo langu ni kuijenga CV na uzoefu na kugundua changamoto mpya huko niendapo baada ya Kuhitimu Chuo kikuu. Lakini wapi!

Ndio maana nilifikia uamuzi wa kujifunza Kushona nguo Kwa sababu nilijiuliza Kwa mfano nikakosa Ajira nitafanya nini, na kazi za nguvu Mimi siziwezi, au hata nikipata Ajira alafu nikafukuzwa kazi nitafanya kazi gani, hapo wazo la kuwa fundi cherehani likawa Bora baada ya kuyashinda mawazo mengine ya ufundi magari (sikuwa na connection), ufundi welding, ufundi umeme halikadhalika sikuwa na connection.

KAZI ya fundi cherehani mademu wakawa wananizingua, hawanitaki[emoji3][emoji3] ati walivyo wajinga wakawa wananitania; nitatoboa nguo ngapi ifike milioni sita walau ninunue Gari ndogo [emoji3] nilikuwa nabishana nao huku moyoni nikiona ugumu kweli wa kupata hiyo pesa. Hata hivyo sikuwajali Sana. Baadaye nikaacha kushona nikaenda Tegeta kufungua Duka.

Biashara Kwa miaka mitatu ikanipa faida kadha WA kadhaa lakini baadaye ukapata anguko kuu.
Kurudi nyumbani siwezi kwakweli, kubaki mjini nitabakije tena wakati Kodi Mimi, Kula Mimi, umeme na maji vyote Mimi.

Ndipo wazo la kuomba kazi ya ualimu shule moja kubwa hapa jijini DAR es salaam likapata nguvu kichwani.

Nikaomba kazi Kwa bahati nikaitwa interview. Ilikuwa ndio interview yangu ya Kwanza.
Nilikuta wenzangu wengi Sana wapatao Mia na kitu hivi, nafasi ni waalimu watano[emoji3][emoji3]

Tukapiga Written Interview nikapasua, si unajua Sisi wengine ni vipanga[emoji3][emoji3]

Sasa kwenye Oral hapo ndipo nilipatwa na aibu kubwa ambayo mpaka Leo nahisi ilinidhalilisha Mno.

Ukiingia kwenye interview CV na vyeti vyako vinakuwa mbele ya Anayekusaili.
Sasa embu piga picha umeshika CV ya Taikon mwenye ufaulu mkubwa usio na Shaka, ufaulu wa juu wa daraja la Kwanza, kuanzia primary mpaka Chuo kikuu GPA ya juu kabisa.
Angalia umri wangu ungali bado ni mdogo kuashiria kichwa kinachaji.

Sasa wasaili huuliza maswali kulingana na CV na vyeti vya msailiwa.

Wakauliza maswali nikayapangua Kama maswali ya kitoto tuu[emoji3][emoji3]
Sasa walivyoona karibu kila swali najibu tena Kwa kingereza changu cha shule ya Kata lakini kilichonyooka.

Kimya kikatokea huku nikiwatazama nikiwa nimepata Moto wa kutaka kuulizwa maswali mengine magumu zaidi.

Nikawaambia waulize zaidi magumu magumu, wote wakacheka huku baadhi Yao wakiona Kama nawadhihaki.
Akauliza Mzee mmoja swali lakizushi, nikamjibu Kwa reference, wakanipigia makofi huku wakinisifia.

Sasa Mimi nikawa najitukuza nikiwaambia hapa nina miaka mitatu sijashika daftarii Wala kitabu, sijahusika na mambo ya Taaluma nipo hivi, mngenikuta Enzi zangu nyie si ndio mngekoma. Wakacheka[emoji3][emoji3]

Sasa kumbe ajikwezaye hushushwa na ajidhiliye hukwezwa.

Mwalimu mmoja akaniambia nielezee Term iitwayo "Reconnaissance" nikatabasamu nikaelezea Kwa mbwembwe kubwa nikijua hawana maswali ya kuniuliza.

Wakanipigia Makofi, lakini Yule mwalimu aliyeniuliza swali kumbe alijua ningejibu akasema ananiomba niandike "Reconnaissance" ubaoni.

Hapo ndipo kizaa kikatokea, awlai niliona ni rahisi lakini nilipoanza kuliandika ubaoni nikagundua hii Ngoma nalala Yoo!
Nikawa nachanganyikiwa kwenye Hizo herufi zilizo-double. Nikashindwa kuandika Asee!

Nikaandika Reconaissanse" badala ya "Reconnaissance" hapo Yule mwalimu akaruka Kwa kushangilia huku nami nikijua swali hilo limenichenga. Yule mwalimu akasema umeshindwa.

Nikawaambia Kama nimeshindwa basi sistahili kazi hii tukufu ya kufundisha, wakanilazimisha kuwa hiyo hutokea na mbona mengine yote nilijibu vizuri.

Ila ukweli nilisikia aibu kubwa, nikaacha Ile KAZI.

Matambo yangu ndio yaliniponza, Sisi wenye sifa tukiumbuka tunaumbuka haswa Jamani!

Shule hiyo inaneno "FUTURE" Katika jina lake la shule, ni shule kubwa mno. Waalimu WA hapo waliokuwepo miaka minne iliyopita nafikiri mtakuwa mnakumbuka.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Da nimecheka sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Aibu ambayo mimi nimeipata katika interview ni suala la kuabudu....

Picha linaanza kuna mtu kanipa connection ya kufundisha shule fulani ya Dini, nikapeleka CV zangu pale mimi huyo nikapotea kurudi zangu Mkoa baada ya kuona miezi inapita siitwi kwenye Interview ,

Hatimaye miezi kadhaa mbele nikaitwa nikafunga safari hadi jiji la Dar,
nikapewa ile Written Interview then nikapiga ile Oral,

Kimbembe kilianza pale muda wa kuabudu umefika na watu wote ambao walikuwapo pale wakatawanyika wamekwenda kujiaanda kwa ajili ya ibada,
mimi nimekaa mtaani kipindi hicho takribani miaka mitatu baada ya kutoka chuo so mazingira ya mtaani nimeadopt ile mbaya hadi kuabudu imekuwa shida,
Baada ya ibada msaili mmoja akaniuliza mbona haujafanya ibada? Nikajikaza kwa kumwambia niko vibaya naumwa,
Aisee nilijiona dhaifu na aibu kubwa juu yangu hatimaye sikuchaguliwa nikahisi hili la kuabudu limechangia...Basi nilikaa mjini takribani wiki 1 nikarudi zangu Kijijini,

Now Employed.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kitendo cha kukaa kimya unadondosha marks so jibu kwa kujiamini hata kama ni pumba
Aisee, Mwaka huu wote nime u dedicate katika kutafuta Ajira maana ni fresh Graduate (Accounts) Napitia nyuzi za Interview kupata Kauzoefu kidogo. Najiuliza sana maswali endapo nitaulizwa jambo geni na endapo sina idea kabisa itakuaje. Kama wanauliza kupima uelewa aisee Hawatanisahau maana Niko Vzr sana, Ila kama wanauliza Terms ngumu ngumu nahisi naweza nikateleza sehemu
 
Be honest waambie kitu kama hukijui kuwa sijui but nitakifuatilia na kujifunza.
Kuna maswali huwa yanaulizwa wakijua huna majibu kukupima how trustful your are wala
nia sia kulipata swali.
 
Hivi Kwenye Interview kama hujui Swali inakuaje? I mean Kama huna idea kabisa, Unawaambia hujui au Unawaambia waulize jingine?
Huwezi kukosa idea labda kama hujaelewa hamna swali unaweza usitambue labda kamaanisha nn yaani msamiati hujui kwa kingereza ila ukiwa na ukiactivate moody kwamba niko kwenye interview kila swali utajibu kama umeelewa tu utapiga mule mule

Except kwa maswali ambayo yako strictly na majibu yako constant mfano kama hujasoma job duties and responsibilities kama zilivyo kweny tangazo la ajira kutunga utapata tabu sana
 
Mi nakumbuka nafanya interview nilikuta watu wana summary za kusomea na ni oral nimeenda rafu wanaonijua walikuwa wengi wakawa wanacheka tu mi nikajitenga walikuwa wanaitoa kwenye mood kichwani ninajua job duties and respobilities tu hapo sijui hata nikiambiwa tell is about yourself ntasemaje, mambo kibao sijui what are the interest facts about you

Tukaambiwa tukale kwanza baada ya kutambulishwa kwenye panel list kimekaa na watu wanafanya rehearsal kabisa hapo pembeni wanaulizna niliona wanaboa chai sijamliza nikaondoka watu wanapractise mpaka jinsi ya kutembea Dah

Nikapewa namba nilikuwa wa 6 nilipoingia tu nilijibu yote mzee natak kutoka nikaambia tell us eaxctly what you are going to do once you employed in the corporation as you area specialization" nikasema hapa ndio naongezea sauti ndo zile job duties and responsibilities wakasema five things nikataja mpaka tatu nikaambiwa gud nikatoka
 
Ulifanikiwa kupata kazi hapo?
 
Aisee, Mwaka huu wote nime u dedicate katika kutafuta Ajira maana ni fresh Graduate (Accounts) Napitia nyuzi za Interview kupata Kauzoefu kidogo. Najiuliza sana maswali endapo nitaulizwa jambo geni na endapo sina idea kabisa itakuaje. Kama wanauliza kupima uelewa aisee Hawatanisahau maana Niko Vzr sana, Ila kama wanauliza Terms ngumu ngumu nahisi naweza nikateleza sehemu
Huko kuwa uko vizuri au hauko vizuri utakujua baada ya kuwa kwenye interview room 🤣 🤣
 
Ulikua 2019 niliitwa kwenye usaili wa ualimu. Tulipiga written fresh, ikaja practical nikaingia kupiga pindi. Ile shule ni private na wanafunzi wanaumri mkubwa kidogo na wanavaa sare nyeusi chini juu nyeupe.

Miongoni mwa waliokuwepo darasani kumbe alikuwemo mkuu wa shule sikujua maana umri wake Kama wanafunzi tu. Sasa wakati napigisha pindi na msaili anasimamia nikampoint mkuu ajibu swali.

Wanafunzi wakawa wanashangaa,jamaa akajibu swali wakampigia makofi nikahitimisha pindi. Yaliyojiri sinahaja ya kusimulia wote mnajua.
 
Be honest waambie kitu kama hukijui kuwa sijui but nitakifuatilia na kujifunza.
Kuna maswali huwa yanaulizwa wakijua huna majibu kukupima how trustful your are wala
nia sia kulipata swali.
Hapa nimekupata Mkuu, Umeelezea Vizuri sana, Naimani ntajibu kadri ya uwezo na Uwelewa wangu
 
Huko kuwa uko vizuri au hauko vizuri utakujua baada ya kuwa kwenye interview room [emoji1787] [emoji1787]
[emoji23][emoji23] Mkuu ww ulishawahi kuingia kwenye chumba Cha Interview? Hebu tupe Experience yako
 
Huwezi kukosa idea labda kama hujaelewa hamna swali unaweza usitambue labda kamaanisha nn yaani msamiati hujui kwa kingereza ila ukiwa na ukiactivate moody kwamba niko kwenye interview kila swali utajibu kama umeelewa tu utapiga mule mule

Except kwa maswali ambayo yako strictly na majibu yako constant mfano kama hujasoma job duties and responsibilities kama zilivyo kweny tangazo la ajira kutunga utapata tabu sana
Hapo sawa mkuu nimekupata Vyema, Na vipi kuhusu Lugha unachagua au wanakuchagulia? Na Je ni Lugha ipi inafaa kutumia kati ya kiswahili au Kiingereza? Maana tunajua Kiswahili Huwa kina Maneno magumu sana
 
Back
Top Bottom