Ni aibu gani umeshawahi kupata kwenye maisha yako??

Hahaaa!!!

Nilikua kanisani, ukafika mda wa kutoa sadaka, kikapu kimepitaaaaa wa mwisho nikawa mimi kudadeki kila nikitazama nimpasie nani niepukane na msala hakuna.

Akaja katekista(msimamizi) akaniambia nikipeleke kikapu mbele altar, (imagine sijawahi kufika altar tangu nizaliwe.)

Kumbishia siwezi, mle ni Church, utaonekanaje kumvimbia katekista?

Nikasimama kwa heshima(kama vile sina dhambi) nikaanza safari ya kujongea altar wenge kama lote,najiuliza nikifika sijui itakuaje.

nimefika pale sijui nifanye nini aseee!!! Ikabidi nianze kukopi kila anachofanya padre.

Ikawa akiinama na mie nainama, akiinuka na mie nainuka,

Nikamuona padre anaanza kucheka, kumbe anavyocheka tayari kanisa zima hawana mbavu(kumbuka hapo kwaya inaimba)


Kidogo nasikia mpaka wanakwaya wanashindwa kuimba wanacheka. 😄 🤣 😂

Ishu ikawa kugeuka kurudi kukaa, kila naemtazama hana mbavu anacheka.

PIA SOMA :Magari ya milioni Tano (5M) kushuka chini
 
Pole sana mkuu hiyo aibu ya mbele za watu mbaya sana
 
Hebu lete mkuu, tujifunze
Si tunataka tulie
Baada ya kupata ajira nikianza kuwa mlevi wa kutupwa halafu nilikuwa najitamba kuwa nina pesa chafu, sikukumbuka habari ya kujenga nyumba yangu ili nikistaafu nisitaabike.

Mwaka mmoja kabla ya kustaafu nikianza kujenga nyumba ambayo ingekuwa ya kupangisha mungu si Monetary doctor nyumba ikafika katika kiwango lenta lakini isivyo bahati muda wa kustaafu uliwadia.

Nilijisemea kuwa kiinua mgongo changu kitanisaidia kumalizia lakini mambo yalikwenda kinyume na matarajio kwani nilizidisha pombe maradugmfu, nilikuwa nawanywesha marafiki na nilikuwa najitamba hata nikajibatiza kwa jina la Dewji lakini pension nayo iliisha mazima.

Siku moja nilibanwa na njaa kali isiyo na mfano na mfukoni nilikuwa na TSH 1000 niliingia kwenye mgahawa ambao chakula cha bei ya chini kilikuwa TSH 1500 nacho ni ugali. Mazungunzo baina yangu na maman'tilie yalikuwa hivi.

MMI: ugali shilingi ngapi.

MAMAN'TILIE: 1500.

MIMI: (huku nilimpa 1000) hebu naomba unipatie ugali bila mboga.

MAMAN'TILIE: Khah kwa hiyo hutaki mboga au huna hela.

MIMI: Nina hela sema Leo nimeamua Kula ugali peke yake maana katika dunia hii hakuna chakula ambacho sijawahi kula ila ugali bila mboga.

Kumbe watu walikuwa pale mgahawani walikuwa wananisikia, walinicheka na kuanza kunikebehi, yaani siku hiyo niliona aibu ambayo sijawahi kuona mpaka miguu ilikosa nguvu.
 
Hiyo kweli aibu kubwa mkuu, kiuhalisia hakuna anayeweza kula ugali bila mboga
 
Pole sana mkuu mimi nilikuwa nakimbia debate hadi namaliza O-level sijawahi kushiriki Debate
Mimi mara nyingi walikua wananiweka wa kwanza ili kuwachanganya maadui na kuwashusha confidence. Ndio maana hata kwenye rehersal sikuwepo na hawakua na wasiwasi namimi,Ila siku hiyo nilipatikana maana hata sikua nimeambiwa siku hiyo mi naanza
 
Kweli au drama tu?
 
Kwanini wakupopoe?

Atakayekupopoa elewa huyo atakuwa ni 'fuska mbwa'.

Maana yake nini ujue, watu wana wivu sana wa kuona watu wengine wakifanya wayafanyayo wao, tena wakiyafanya kwa ufanisi zaidi.

Mwizi hapendi kuibiwa wala kusikia habari za mtu mwizi.

Mzinzi akikamata ugoni anaua!

Mzinzi ama mwizi akiwa mchungaji ama shehe, si kwa mahubiri hayo ya kulaani vitendo vya namna hiyo.

Hapa umeweka kamtego ka kunasia wazinzi kwa kipimo cha comment watakazoziweka.

Ngoja waje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…