Ni aibu kuandaa sherehe za kupokea ndege

How do you inspire watu ili waone na kuthamini vitu vya nchi yao? Ufanye mambo kimya kimya kisa ni vitu vidogo?

Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Tusiposheherekea achievements za ununuzi wa ndege, hatutaweza kusheherekea siku nchi ikizindua treni zake za umeme, au kusheheherekea siku tutakapozindua kuanza kutumika umeme wa bwawa la Nyerere. Hatutasheherekea hata nchi ikifikia viwango vya kurusha satellites.

How do you build a national pride?
 
Tatizo ni mfumo ccm na wafaidika wake.
Uzuri wa CCM wanufaikaji ni wengi... Ubaya wa Chadema mnufaikaji mmoja kama unavyoona pichani, hii ndio sababu iliyofanya viongozi wamsuse mwenyekiti wao

 
Kila nchi ina historia yake na kila nchi ina utamaduni wake.

SA uliyoitaja hapo last I checked serikali yao ilikuwa inaingiza mabilion ya Rand ili kunusuru shirika lao la ndege lisife. Kutoenda airport kupokea ununuzi wa ndege mpya hakumaanishi kwamba hawajali. Wanajali kwa style yao.

Na hii ndiyo maana ya mtu kuwa huru kifikra na kukomboleka. Haufanyi vitu kisa nchi zingine zinafanya au hazifanyi. Unafanya kwa sababu ya maono na malengo yako kama wewe. Sisi tumeamua Rais aende airport kupokea ununuzi wa ndege mpya kama a symbolic gesture kwa taifa kuonyesha umuhimu wa shirika la ndege imara kwa nchi. Basi.

Ilipotokea Rais anazindua viwanda vinavyoonekana kuwa vidogo kama vya chaki haikuwa na maana nyingine yoyote zaidi ya kuonyesha umuhimu wa nchi kuwa na spirit ya ubunifu na kujitegemea.

Hivi ni nini kimewasibu watu wetu kushindwa kutathmini mambo beyond what they see?
 
Ni bora tuulizaane, hivi hafla ya kwenda kupokea ndege AIRPORT, inagarimu kiasi gani ya hela za walipa kodi wa tz?
Je hiyo hela ya walipa kodi ingetumiwa kununulia madawati, tungepata madawati mangapi ya watoto wetu wanaokaa chini mashuleni?
 
Hata mimi niliwashangaa CHADEMA kuandaa sherehe ya kumpokea Lisu uwanja wa ndege siku ile. Matokeo yake sherehe ilibuma.
Ile sherehe ya chadema kupokea Lissu AIRPORT, hakuna shilingi ya mlipa kodi iliotumika.
 
Kwani si ni ndege yetu tukisherehekea kuna ubaya gani mwajameni.
 
Hivi wewe ukijenga nyumba mpya au ununue gari mpya hapo nyumbani huwa panakuwaje kwa furaha
 
Wakati huo huo watoto wa shule hawana vyoo wanajisaidia machakani!!
 
Wakati huo huo watoto wa shule hawana vyoo wanajisaidia machakani!!
Shule gani hazina vyoo?!!

Yaani wanatarafa wanashindwa kutafuta Suluhu ya hayo?

Yaani wana wilaya wanashindwa kutafuta Suluhu ya hayo?!!

Wananchi wapo.....

Wenyeviti wa HALMASHAURI wapo....

DAS yupo.....
DED yupo.....
DC yupo.....

Tunashindwa kujiongeza kama raia katika maendeleo yetu wenyewe?!!!

#KaziIendelee
 
ni uthubutu wa ajabu! Tena wakusikitisha.
 
Hivi vitu wanavyofanya ni sawa na mtoto aliyenunuliwa andazi alafu anatokanalo nje kulingishia. Kuna vitu kwa karne hii naona ni ujinga tu...
1.mbio za mwenge
2.uzinduzi wa miradi na vitu hasa ukimuhusisha mkuu wa nchi.
Kiujumla hivi vitu vinaongeza gharama tu na matumizi mabaya ya kodi
 
Wewe ndio unasema kitu kidogo, unajua serikali ilikaa miaka mingapi pasipo hizo ndege unazozibeza?hata hivo tunamshukuru Magufuri ingawa amekufa, maana tulikuwa tunaambiwa serikali yetu ilikuwa aina uwezo wa kununua ndege,toka kwa Mwinyi hadi Kikwete akuna aliyethubutu hata kununua angalau inayobeba watu hata watatu au ile inayonyunyuziaga sumu wakati wadudu wabaya wameamia nchi,awamu ya 5 ilioyosha kila kitu kinawekana,acha washerekee.
 
Kuna wanafunzi wameangukiwa na kifusi wakichimba choo cha shule.Hio pesa ya kuandaa hio sherehe ya upokezi ingetosha kujenga choo cha shule.
 
Awajui kubana matumizi ya kodi zetu bali wanachojua ni kubana wananchi walipe kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…