Rweyemam105
Senior Member
- Sep 8, 2012
- 105
- 154
Hallo. Kama title inavyojipambanua. Kati ya miji midogo inayokuwa ndani ya Halmashauri ya Mji wa Moshi, ni pamoja na Mji wa Himo ambao uko karibu na Mpaka maarufu wa Kenya na Tanzania(Holili).
Mji huu umekuwa na viashiria vingi kuonyesha kuwa unakua kutokana na shughuli mbali mbali za kiuchumi zinazoendelea ndani ya mji huo mdogo ndani ya Manispaa husika(Moshi)
Kama viasharia vya kiuchumi vipo, basi manispaa hiyo haina budi kutimiza wajibu wake kwa kupeleka maendeleo Muhimu Kama vile Taa za usiku(Solar street lights) Kama ilivyo kwa miji mingine inayochipukia.
Nitoe tu rai kwa Manispaa ya Moshi iweze kuupa kipaumbele mji huo, kwani kwa sasa umeonekana kukua kutokana na shughuli mbali mbali zinazoendelea ktk mji huo.
Kwa kuhitimisha, suala la Usafi lisiwe ni kwa ajili ya mji wa Moshi mjini tu. Manispaa ijikite kueneza elimu ya usafi mkoa wote wa kilimanjaro, isiwe Kama nyumba ambayo usafi unafanyika sebuleni tu, ili hali ukiingia kwenye vyumba unapishana na Mende na Panya buku. Ninaimanisha, vitongoji vyote vya mkoa wa Kilimanjaro vinapaswa kuhimizwa maswala ya usafi wa mazingira.
Karibuni Marangu & Kilema