Sio kweli kwamba alienda kama mkimbizi. Huyu aliondoka Zanzibar 1960 - kwa mujibu wa DW. Wakati huo hakukuwa na sababu ya ukimbizi.
Aliondoka late 1960's! Jana nilihoji ikiwa by the late 1960's, kulikuwa na security risk kwa kijana mdogo ambae hakuwa mwanasiasa. I know by that time, vijana wengine kama akina SAS walikuwa kwenye hiyo risk na ndo maana Mwalimu akamtupa ubalozini!
Conclusion yangu, Mwamba alitumia janja ile ile ya Watanzania na kwingineko Afrika... kwamba unazamia mbele kwa gia ya ukimbizi na Wazanzibari wanatumia sana hii mbinu,!!
Mwaka juz Makonda alipoanza ku-deal na mashoga, nilipata issue za Wazanzibari wawili walioingia Marekani kwa hoja kwamba maisha yao yapo hatarini kwa sababu ya wao kuwa mashoga. Na hapa ninapoongea, jamaa wote wawili wanakula pesa ya Joe Biden Unyamwezini!
All in all, hadi kesho, pamoja na kuchimba sana lakini sijaona popote ambapo Abdulrazak Gurnah kutajwa kama Mwingereza. Sources zote zinamtaja kama Mtanzania au Zanzibar-born based in UK!
Na lingine ambalo watu hawalifahamu ni kwamba, sio kwamba jamaa baada ya kutoka ZNZ hakuwahi kurudi tena bali back 1984, ndipo kwa mara ya kwanza alirudi ZNZ tangu alipoondoka!!
Tukija kwa mleta mada.... hili jambo linakuzwa sana! Hivi hao akina Samia hata wakisema "alisoma kwa kodi zetu" kwani Wabongo mnapungikiwa nini? Mbona tunapend kujihangaisha na mambo madogo madogo sana?!!
Lakini kwa upande mwingine, asikudanganye... Nobel Prize ni tuzo inayoheshimika sana duniani na ndo maana media kubwa karibu zote duniani, zimeruka na hii issue zaidi ya mara moja!!
]Kwahiyo sioni tatizo lolote akina SSH wakiteleza na ganda la ndizi... that's how the world work! Au mnataka Wakenya waanze kusema jamaa ni Mzaliwa wa Lamu, na alienda mbele akitokea Mombasa? You know they're good at it....