Ni aibu kwa taifa letu kumuona Prof Abdulrazak Gurnah kama shujaa wa taifa letu, wakati huko nyuma hajawahi kutambuliwa kwa kazi alizofanya

Samahani, Mkuu!

Naomba kama kuna kitabu chake chochote alichoandika kwa KISWAHILI unitajie.

Hapa wanazungumza juu ya “ENGLISH LITERATURE AU LITERATURE IN ENGLISH” na siyo Kiswahili/Swahili Literature!!!!!! wabongo vipi?!!
 
Hapa wanazungumza juu ya “ENGLISH LITERATURE AU LITERATURE IN ENGLISH” na siyo Kiswahili/Swahili Literature!!!!!! wabongo vipi?!!
Anashughulika na vitabu vya lugha gani?

Nitajie kitabu chake hata angalau kimoja kilichoandikwa kwa Lugha ya Kiswahili.
 
Mkuu ukipata nafasi ya kufundisha UD na nje huko ulaya bora fanya kazi huko huko hapa hutatambulika utamalizwa na siasa tu.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Nashindwa kuwaelewa watanzania kwa sasa.Wengi hamueleweki kabisa mnachoongea .Sasa nashindwa kuelewa ,kuwa hizi Nazi ni siasa au nikuilamu tu serikali?Huyo jamaa ,kaandika particular s zake mwenyewe kuwa ni mtanzania.Kawapa hao jamaa wa NOBEL .Ameshinda tuzo.Jamaa hao wa NOBEL wamtangaza wao wenyewe kupitia BBC ,Aljazeera kuwa mtanzania kashinda NOBEL ya literature. Je, tatizo la serikali lipo wapi ?Kama MTU kajileta mwenyewe na kusema ni mtanzania ,serikali imkatae ?Nendeni mmulaumu huyo Prof ,kwann anawapa serikali ujiko ,kuwa ni mtanzania.
K
Wewe ndiyo unatakiwa usieleweke. Nikuulize: huyu pro. ni mtanzania kwa mujibu ya sheria za Tanzania?
Kamuulize yeye ndio kaandika particular zake kaziweka kwenye kamati ya NOBEL.Kuwa yeye ni mtanzania. Kosa la serikali ni lipi?Lowassa(2015).Elimu!Elimu
 
Kosa la serikali ni kusema ni mtanzania wakati siyo mtanzania bali ana asili ya Tanzania. Je, mtu yoyote anaweza kuwa mtanzania kwa sababu tu yeye mwenyewe ameandika kuwa ni mtanzania? Kati yangu na wewe ni yupi ameonyesha upeo mdogo wa elimu? Yaani wewe unatetea ni mtanzania kwa sababu tu ni yeye kaandika hivyo! Ukisikia undezi ni huu sasa. Halafu unajiona una elimu!
 
Awamu iliyopita waliachiwa kutoka gerezani walawiti(walihukumiwa kifungo cha maisha na mahakama ya kisutu na kuthibitishwa na mahakama ya rufaa) babu Seya na mwanawe na walifanywa kuwa mashujaa kwa kuhalikwa hadi ikulu (hapa ikulu ilinajisiwa), Naungana na mleta uzi Nyankurungu2020 tuache kuwaona mashujaa watu wasiostahili.
 
Sawa. Mkuu kwa sheria yetu ya uraia bado ni Mtanzania ikiwa hajaukana Utanzania.
Ni raia wa uingereza kwa vile haturuhusu urai pacha.. Anatambua kuwa alizaliwa Zanzibar na ana ndugu Zanzibar lakini yeye sasa ni raia wa Uingereza na anasafiri kwa passport ya Uingereza
 
SIKU ITAKAPO KUJA KUTANGAZWA YA KWAMBA TANZANIA WAMERUHUSU URAI PACHA NDIO SIKU TANZANIA INAPATA MAENDELEO YA KWELI SABABU KUNA VICHWA WAZAWA WA KITANZANIA VIPO DUNIA YA KWANZA WACHA.

NAHAKUNA SABABU YA KUWAKATA WATU WENU AMBAO WAMEKWENDA NJE KUTAFUTA MAISHA KWA AJILI YA FAMILY ZAO LEO HII UNAWAAMBIA SIO WATANZANIA NA WAKIRUDI NCHI ZAO ZA ASILI WANA TREATIWA KAMA WAGENI.

BASI HATA KAMA HAMTAKI KUWAPA URAI BASI AT LEAST INGIANZISHWA SHERIA ZA KUWATAMBUA DIASPORA WA KITANZANIA NA KUWAPO SPECIAL STATUS YA KUISHI BILA VIZA NA KUFANYA CHOCHOTE CHA KIMAENDELEO KAMA MTANZANIA WA KAWAIDA ILA WASIJI INVOLVE NA MAMBO YA UTAWALA AU UCHAGUZI AT LEAST INGE MAKE SENSE KULIKO KUWAFANYA KAMA WAGENI.
 
Huko nyuma CCM-Zanzibar waliwahi kuandamana kumfukuza huyu mtu huko zanzibar kutokana na rangi yake.

Ubaguzi wa rangi ulimuondoa Zanzibar.Ubaguzi wa rangi kutoka CCM ulimfanya huyu mtu kuikimbia Tanzania na kwenda kuomba uraia uengreza.
 
Ni raia wa uingereza kwa vile haturuhusu urai pacha.. Anatambua kuwa alizaliwa Zanzibar na ana ndugu Zanzibar lakini yeye sasa ni raia wa Uingereza na anasafiri kwa passport ya Uingereza
Mkuu ikiwa anasafiri kwa paspoti ya Uingereza nakubaliana nawe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…