Ni aibu sana mwanaume mwenye umri 35 na kuendelea kukosa uwekezaji wa kuanzia millioni 30

Ni aibu sana mwanaume mwenye umri 35 na kuendelea kukosa uwekezaji wa kuanzia millioni 30

Nijiue kwa sababu sijawekeza?
Wewe umeongelea nafsi yako na namna unavyoyapokea na kuyachukulia mambo yanayokujia au kukutokea......watu wengi tumetofautiana kimawazo, utashi na fikra hata kwenye mambo yanayofanana.......andiko limewalenga watu hao ambayo hawana utashi na mtazamo kama wa kwako.....
 
Huwa nashangaaga sana hivi muda wote huo wa miaka kumi ya utafutaji wako unakosa kuwa na asset zenye thamani ya pesa hizo
Kwamba shetani kakuchukia sana kana kwamba anaona akikupa hivyo vitu utamsaliti.

Au mnapata ndio starehe zimewazidi miaka 35 inakushindwa million 30 tu kweli halafu mnakazana ipo siku mungu atatusaidia hivi mpo serious kweli.

Kuna jamaa alisemaga muuwawe mnalitia hasara taifa.

Ni aibu tena aibu sana mwanaume kama wewe unakosaje kuwekeza bhana aah hata kiwanja kule Ituli ndani ndani nacho huna.

Hata tumbuzi twa kujivunia labda baada ya miaka mitano wanaweza fika 50 ukauza nao huna kweeeli kabisa yaani kabisa
ila smat ya m3 na kagheto kakumbususia wake za watu unalo tena limesheheni vitu ambavyo haviwezi kuku move on wakati ujao

Tuache kujipa matumaini ya hovyo hata Mungu wenu hawapendi watu wa namna hiyo.

Umri ndioo huoooooooo unaenda msiseme sijasema.

Pia mnatabia za kutokujifunza mambo mapya kila kitu unachoambiwa utasikia motivesheni spika, kila kitu kwenu hakiwezekani

(Ngoja tupate tangazo)
👇
Wakuu samahani kwa yote ni mimi MR PIPA ambaye nilipata hiyo hela nikaenda kuhonga naombeni mnisaidie japo 5000 hali tete michongo imebuma natumaini ombi litashughulikiwa.

(Twende tuendelee) hivi kwa nini umri huo umeshindwa kuwa hata na m30 sehemu mnafeli wapi? Kama ww mwenyewe umejisaliti kwa kuto kuwa na kiasi hicho nani atakuamin, biashara asubuhi jioni mahesabu.

Na namwomba shetani watu kama nyinyi muwe na gundu hadi kwenye mbususu yaani mnyimwe ili akili ziwakae.
We bwana tafadhali.
 
Umesema miaka 10 ya utafutaji sio? Kuanzia 25 hapo unamaanisha!

Sawa, twende pole pole, mimi ni kijana nilikulia maisha ya kuunga unga, home msosi mmoja kwa siku, nimepita pita shule kwa msaada wa serikali, nimemaliza nikiwa na miaka 24. Sina cha kurithi wala sijaanzishiwa maisha.

Miaka 4 ya kutafuta kazi, sina kitu hapo! Miaka 2 iliyofuata nikiwa na ajira ya mshahara wa 1,000,000/= basic, nikaanza kupanga ghetto na kujiweka sawa!

Ili kuepuka kuwa centre point ya familia, najivisha majukumu, kuvuta wengine ili wajitegemee! Kwa miaka 4 napambana na maisha yangu na ya familia(shule, kula, matibabu na pango)

Miaka 10 ya utafutaji wa halali ndo hiyo hapo na umri ndo huo hapo! Sh 30m inapatikanaje?
- Au kwa mikopo ya riba iliyoshushwa? Poda? Michezo au Mission town? Kuwa chawa? Kulamba midomo?
Fact, huyo mwambaa kaingiwa na pepo
 
Ulivyo andika tu huu uzi wako ikabidi niende kwenye post zako za nyuma i mean profile lako ili nijue wewe ni mtu wa aina gani.
Uzi wa pili tu kukutana nao sikuona umuhimu wa kuendelea mbele maana majibu nikawa nimeyapata.

Ipo hivi, ukimtegemea Mungu wa mbinguni aliyeziumba mbingu na nchi, kufanikiwa huwezi kujipangia ni mpaka Mungu akufungulie mlango huo.

Mungu kujibu maombi ya uchumi huwa haangalii umri bali tunasema Mungu huwa hawahi wala hachelewi bali kila mtu na wakati wake alio kusudia yeye.

Kwenye huo uzi wako nimeona unammwagia sifa shetani kwamba ukitaka utajir ni chapu anakupa kupitia waganga.! Sehemu nyingin unasema amekupa siri ya kujua utamu wa mbususu.!
It is ok kwa staili hiyo nikupe hongera kwa kufanikiwa kwa umri wa miaka 35 kumilik mil 35 inawezekana hicho ni kiwango cha chini inayo zaidi.

Yote tuyafanyayo hapa duniani hutokana na maamuzi, hivyo acha walioamua kuto mkimbilia shetani wafanikiwe kwa muda wao huenda at 40's or 60's haijalishi.

Nimechok kuandik ngoja niishie hapa.!
[emoji2936][emoji2936]
 
Life begins at 40 ni njia ya mtu aliyechezea muda wake kujifariji. Maisha yanaanza immediately ukishapata akili timamu, kama hiyo akili timamu unaipata at 40 kuna shida sehemu "The earlier the better"
Wewe hujaelewa mantiki ya usemi huu.
 
Man proposes and God disposes. Maisha hayako hivyo na kupata siyo ujanja au akili yako bali ni kile ambacho Mungu amekukadiria. Kuna watu wanatajirika wakiwa na miaka hamsini hadi sitini. Wapo wanaotoboa wakiwa vijana wadogo kabisa. Wapo waliokuwa matajiri wakubwa na sasa wamefilisika hawana hata mia moja. Ukipata mshukuru Mungu na usiwaone wasionacho kuwa hawana akili wala malengo. Hujafa hujaumbika. Dunia ni duara. Unaowacheka leo kesho wanaweza kuwa mabosi wako.
 
Utafutaji una mambo mengi mkuu, unaweza kupambana ile unakaribia kuona mwanga mara ghafla unaserereka kurudi nyuma hatua 800.

Nilipofikisha umri wa miaka 27 nikawaza kuanza kujikongoja mdogo mdogo, nikasema wacha ninunue pikipiki kwa ajili ya boda boda, nikanunua pikipiki 4, nikasema wacha nitafute na kashamba nilime nilime hata vimahindi kwa ajili ya biashara.

Mwaka haukuisha bodaboda 2 ajali, mambo yakawa mengi, kurudi shamba nako nyani wamevuna kabla ya muda[emoji23][emoji1787].

Hili la nyani lilinitia hasira nikatelekeza shamba.

Unaanguka, unanyanyuka, unakung’uta vumbi safari inaendelea.
 
Mtoa mada inaonekana anahisi ametoboa kwenye miaka yake ya 20s so anawazoom wenye miaka 35 anawaona maboya ambao bado wana hustle.
 
Back
Top Bottom