Ni aibu sana mwanaume mwenye umri 35 na kuendelea kukosa uwekezaji wa kuanzia millioni 30

Nijiue kwa sababu sijawekeza?
Wewe umeongelea nafsi yako na namna unavyoyapokea na kuyachukulia mambo yanayokujia au kukutokea......watu wengi tumetofautiana kimawazo, utashi na fikra hata kwenye mambo yanayofanana.......andiko limewalenga watu hao ambayo hawana utashi na mtazamo kama wa kwako.....
 
We bwana tafadhali.
 
Fact, huyo mwambaa kaingiwa na pepo
 
[emoji2936][emoji2936]
 
Life begins at 40 ni njia ya mtu aliyechezea muda wake kujifariji. Maisha yanaanza immediately ukishapata akili timamu, kama hiyo akili timamu unaipata at 40 kuna shida sehemu "The earlier the better"
Wewe hujaelewa mantiki ya usemi huu.
 
Man proposes and God disposes. Maisha hayako hivyo na kupata siyo ujanja au akili yako bali ni kile ambacho Mungu amekukadiria. Kuna watu wanatajirika wakiwa na miaka hamsini hadi sitini. Wapo wanaotoboa wakiwa vijana wadogo kabisa. Wapo waliokuwa matajiri wakubwa na sasa wamefilisika hawana hata mia moja. Ukipata mshukuru Mungu na usiwaone wasionacho kuwa hawana akili wala malengo. Hujafa hujaumbika. Dunia ni duara. Unaowacheka leo kesho wanaweza kuwa mabosi wako.
 
Utafutaji una mambo mengi mkuu, unaweza kupambana ile unakaribia kuona mwanga mara ghafla unaserereka kurudi nyuma hatua 800.

Nilipofikisha umri wa miaka 27 nikawaza kuanza kujikongoja mdogo mdogo, nikasema wacha ninunue pikipiki kwa ajili ya boda boda, nikanunua pikipiki 4, nikasema wacha nitafute na kashamba nilime nilime hata vimahindi kwa ajili ya biashara.

Mwaka haukuisha bodaboda 2 ajali, mambo yakawa mengi, kurudi shamba nako nyani wamevuna kabla ya muda[emoji23][emoji1787].

Hili la nyani lilinitia hasira nikatelekeza shamba.

Unaanguka, unanyanyuka, unakung’uta vumbi safari inaendelea.
 
Mtoa mada inaonekana anahisi ametoboa kwenye miaka yake ya 20s so anawazoom wenye miaka 35 anawaona maboya ambao bado wana hustle.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…