Umesema miaka 10 ya utafutaji sio? Kuanzia 25 hapo unamaanisha!
Sawa, twende pole pole, mimi ni kijana nilikulia maisha ya kuunga unga, home msosi mmoja kwa siku, nimepita pita shule kwa msaada wa serikali, nimemaliza nikiwa na miaka 24. Sina cha kurithi wala sijaanzishiwa maisha.
Miaka 4 ya kutafuta kazi, sina kitu hapo! Miaka 2 iliyofuata nikiwa na ajira ya mshahara wa 1,000,000/= basic, nikaanza kupanga ghetto na kujiweka sawa!
Ili kuepuka kuwa centre point ya familia, najivisha majukumu, kuvuta wengine ili wajitegemee! Kwa miaka 4 napambana na maisha yangu na ya familia(shule, kula, matibabu na pango)
Miaka 10 ya utafutaji wa halali ndo hiyo hapo na umri ndo huo hapo! Sh 30m inapatikanaje?
- Au kwa mikopo ya riba iliyoshushwa? Poda? Michezo au Mission town? Kuwa chawa? Kulamba midomo?