Ni aibu, uchanga, na kukosa weledi kwa wapinzani 'kushadadia' na kutumia taarifa ya CAG kuikosoa Serikali

Katika demokrasia ya vyama vingi, vyama vya upinzani hutafuta madudu ya serikali na kuyatoa kwa jamii. Hapa Tanzaia vyama vyetu vya upinzani vinatumia taarifa za serikali kuikosoa serikali.

Kwa mfano taarifa ya CAG ni taarifa ya serikali ikionyesha ilivyotengeneza taasisi za kuisaidia kujisahihisha na kuonyesha kuwepo kwa uwazi. Hili la serikali kuonyesha uwazi ni jambo la kupongezwa.

Kwa maana hiyo ni aibu kubwa kwa vyama vya upinzani kuitumia kama msingi kwa kuikosoa serikali. Kwa maana nyingine kama serikali ingeamaua kutoiweka taarifa ya CAG hadharani wapinzani wasingekuwa na cha kusema.

Hii inaonyesha haviko tayari kuwa wapinzani wala kuwa chama tawala.
Wapinzani walipiga kelele juu maamuzi mengi ya serekali ambayo madhara yake yameibuliwa na report ya CAG e.g. manunuzi ya serekali kuto kufuata taratibu, teuzi za watendaji wakuu wa mashirika ya umma na wajumbe wa board kuto kufuata weledi, ukosefu wa uwajibikaji, kupeana vyeo kwa ushabiki wa kisiasa n.k. Kwa ufupi hakuna madudu yaliyoibuliwa ambayo wapinzani hawajayazungumzia.
 
Unawezekana uko sahihi- sasa baada ya ripoti kutoka sasa wanajadili nini?
 
Kabisa kwa sababu hawana jipya- If they have something to say and want to tell us, they should tell us what we do not already know.
Hawana uwezo wa kwenda kufanya auditing ya mahesabu serikalini. Na sehemu ambapo wangewasilisha maoni yao rasmi ni bungeni, ambapo hawapo. Sasa wafanyeje?
 
Unatumiaje taarifa ya mwenzako? huo ni wizi
Hivi we jamaa una akili timamu? Hivi unajua maana ya neno Serikali wewe?
Serikali sio chama cha mapinduzi acha kujitoa ufahamu.
Serikali ni zaidi ya chama
Acha kuleta uchama kwenye ishu za kitaifa
 
Serikali ni ya CCM hutaki hamia Burundi
 
Nimesema na ninasema wapinzani wanayo haki ya kuikosoa serikali lakini hawezi kutumia taarifa za serikali kuikosoa- sijui kwa nini unapata tabu kuelewa
Kwa hiyo Zitto Kabwe alipokuwa akichambua taarifa za CAG wakati akiwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mahesabu ya serikali (PAC) alikuwa anakosea?

Tofauti ni kwamba kipindi kile walikuwa Bungeni na sasa hawapo!!!
 
unakosoa serikali au taarifa? Ninachosema hapa ni kazi ya upinzani kuikosoa serikali; wanakosoa serikali kwa taarifa walizozipata wenyewe na si kwa kutumia taarifa za serikali
Taarifa hizo si zinahusu serikali? Je, serikali ikisema imepata hasara kwenye biashara ya ndege kwanini wapinzani wasiseme na kuikosoa serikali kwa jinsi inavyofanya biashara ya ndege bila kuwashirikisha sekta binafsi?
 
serikali inasema imepata hasara kwenye biashara ya ndege- sasa hapo unakosoa nini?
 
Tunakosoa ufanyaji biashara wa hovyo unaosababisha hasara kila wakati.
Kama ni hivyo hamhitaji kusimama kwenye ripoti ya CAG mnajidharililisha
 
Umenikumbusha nchi fulani miaka fulani mkuu wa kaya alizibana hizi taarifa, na CAG mmoja akataka kwenda kinyume na mkuu wa kaya na kazi ikawa mwisho wake, na wakazi wa kaya ile wakaya hawajui chochote ikawa ni kusifu na kuabudu tu.
 
upinzani sasa hivi wanalamba asali hata hawajui waingie na gia gani kuwahadaa wananchi bado wanashangilia agizo la kuachiwa mikutano kuwa huru huku muda ukiwatupa mkono
 
Katika demokrasia ya vyama vingi, vyama vya upinzani hutafuta madudu ya serikali na kuyatoa kwa jamii. Hapa Tanzaia vyama vyetu vya upinzani vinatumia taarifa za serikali kuikosoa serikali.

Kwa mfano taarifa ya CAG ni taarifa ya serikali ikionyesha ilivyotengeneza taasisi za kuisaidia kujisahihisha na kuonyesha kuwepo kwa uwazi. Hili la serikali kuonyesha uwazi ni jambo la kupongezwa.

Kwa maana hiyo ni aibu kubwa kwa vyama vya upinzani kuitumia kama msingi kwa kuikosoa serikali. Kwa maana nyingine kama serikali ingeamaua kutoiweka taarifa ya CAG hadharani wapinzani wasingekuwa na cha kusema.

Hii inaonyesha haviko tayari kuwa wapinzani wala kuwa chama tawala.
Upinzani haupo bungeni kwa wizi wa kura wa yule punguani taarifa au udhaifu wa serikali wangeutoa chooni? Muwe mnafikiria kabla ya kuandika maujinga haya
 
upinzani sasa hivi wanalamba asali hata hawajui waingie na gia gani kuwahadaa wananchi bado wanashangilia agizo la kuachiwa mikutano kuwa huru huku muda ukiwatupa mkono
Ungesema muda wa kufanya nn ungeonekana wa maana hapa unaonekana kama KASUKU/KIKARAGOSI tu unayeitikia mwimbo wowote
 
Back
Top Bottom