Wapinzani walipiga kelele juu maamuzi mengi ya serekali ambayo madhara yake yameibuliwa na report ya CAG e.g. manunuzi ya serekali kuto kufuata taratibu, teuzi za watendaji wakuu wa mashirika ya umma na wajumbe wa board kuto kufuata weledi, ukosefu wa uwajibikaji, kupeana vyeo kwa ushabiki wa kisiasa n.k. Kwa ufupi hakuna madudu yaliyoibuliwa ambayo wapinzani hawajayazungumzia.Katika demokrasia ya vyama vingi, vyama vya upinzani hutafuta madudu ya serikali na kuyatoa kwa jamii. Hapa Tanzaia vyama vyetu vya upinzani vinatumia taarifa za serikali kuikosoa serikali.
Kwa mfano taarifa ya CAG ni taarifa ya serikali ikionyesha ilivyotengeneza taasisi za kuisaidia kujisahihisha na kuonyesha kuwepo kwa uwazi. Hili la serikali kuonyesha uwazi ni jambo la kupongezwa.
Kwa maana hiyo ni aibu kubwa kwa vyama vya upinzani kuitumia kama msingi kwa kuikosoa serikali. Kwa maana nyingine kama serikali ingeamaua kutoiweka taarifa ya CAG hadharani wapinzani wasingekuwa na cha kusema.
Hii inaonyesha haviko tayari kuwa wapinzani wala kuwa chama tawala.