Ni akili ama matope ? Unasomesha mtoto shule za ada kubwa anaishia kuwa Winga , sababu wewe mzazi huna kampuni wala biashara yoyote ya kumrithisha

Ukweli mchungu ambao darasa la saba na form 4 wazamani watakuja kupinga😄😄😄😄

Kwa utafiti usio rasmi wengi wa waliosomesha vijana EM na wanaoendelea kusomesha watoto EM ni;

1. watu waliopata pesa kwa shida sana bila kuwa na elimu kubwa yaani darasa la saba na form 4 wa kayumba.Hawa wanakuwa na hali ya kutokujiamini(inferiority complex mfano ni Msukuma yule mbunge) wawapo mbele za hawa wasomi uchwara. Kwahiyo hasira zote za kuzarauliwa na wasomi uchwara wanapeleka watoto huko EM.

2.Middle class wa kibongo ambao hawana akili timamu ya kujua nini cha kuwekeza mwishowe unakuta hawana hata nyumba wala gari mpaka wanafikia kustaafu.

3.Malimbukeni wanaopenda mashindano na majirani wa mtaani kwao au ndugu zao.Hawa hawajui nini kinaitajika kwa dunia ya sasa wala hawana dira ya miaka 10 au 15 ijayo.Baada ya kusomesha watoto zao EM watarudi kulaumu serikali baadae kuwa wapewe ajira.

Kwa kifupi haya ndo makundi ya jamii ya watanzania watetezi wa EM na washabiki kindakindaki wa huu upotevu wa rasilimali.
 
Kijana punguza hasira tafuta hela!!!

Kama hiyo elimu yako ni mali sana igeuze pesa😄😄😄.Elimu zenyewe mmepata kwenye vyuo vya kata mara jalalani alafu unapiga kelele. Wewe zaidi ya madesa uliyokariri unakitu gani cha ziada tofauti na kusubiri ajira za serikali.

Tafuteni hela elimu kazi yake ni kutoa ujinga na kukufanya uwe na uwezo mzuri wa kufikiri. Hakuna sehemu inasema umesoma ili serikali ikuajiri.Igeni wasomi wa huko duniani.

Tafteni hela!!! sikuizi mpaka bodaboda na wachoma chips wanadegree acheni ngebe🤗
 
Wanawake wengi wana hii mentality na kuwalazimisha waume zao kusomesha watoto shule za gharama

Hoja yao ni kuwa pesa zitatumika kwa michepuko mwisho wa siku mzee anashindwa kupanga list yake vizuri huku umaskini ukitamalaki kwenye familia
 
Hakuna ajira ya ngazi za juu unapata kwa sababu umesoma EM ajira za ngazi za juu wenzako wamesoma nje ya nchi tena watoto wa wakubwa.

Wewe wa EM utaishia tamisemi huko, ukasaidie wananchi.Ukibahatika sana utapate kwenye vitaasisi vya serikali utakuwa middle income ila hamna kitu bado ni mtumwa tu maana hata kidumu na fagio wapo kibao level hizo.
 
Namba 3 umeua mkuu kundi kubwa lipo hapo hasa wanawake wanaolea wenyewe bila baba
 
Wanawake wengi wana hii mentality na kuwalazimisha waume zao kusomesha watoto shule za gharama

Hoja yao ni kuwa pesa zitatumika kwa michepuko mwisho wa siku mzee anashindwa kupanga list yake vizuri huku umaskini ukitamalaki kwenye familia
Ukioa kilaza lazima akupande kichwani.
 

Wewe unahamisha mada.

Mtoa mada hajaponda elimu kabisa. Ila ameponda kusomesha shule za gharama huku mzazi hauna uwezo wa kumpa mwanao ajira inayoendana na thamani ya shule ulizomsomesha

Watu wanasoma shule za bei nafuu na wanafika udsm kibao na wanakuwa best student wa chuo. Bila kuumiza wazazi kiuchumi ila wanapata elimu
 
Ni kizaizai inferiority complex inawapoteza kwenye reli wanakosa focus.Mwisho mtoto akigraduate ndo wanaanza kufunguka akili kuwa walipoteza pesa bure.
Kuna dogo mtaani alikuwa anasomeshwa international school akiwa la kwanza baba ake ni mchaga ila mama ndio anakaza eti mtoto wampeleke international school basi siku za likizo akija na vingereza vyao vya kuunga unga mother anafurahi kweli mtaa wote wanavimba

Hawajafika mbali mtonyo ukakata wakamhamisha boarding za kawaida mtoto kaishia form two kaacha leo hii ukimkuta ni maharage ya mbeya kama wengine, sifa huwa hazisaidiii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…