Ni akili ama matope ? Unasomesha mtoto shule za ada kubwa anaishia kuwa Winga , sababu wewe mzazi huna kampuni wala biashara yoyote ya kumrithisha

Kuna dogo mmoja kasoma shule hizo kafika Hadi chuo Sasa ni mganga wa kienyeji.

Ni ujinga na upuuzi wa Hali ya juu sana Kwa mzazi ambae huna assets za maana kujistress kulipa mamilioni shule za EM
 
Kuna dogo mmoja kasoma shule hizo kafika Hadi chuo Sasa ni mganga wa kienyeji.

Ni ujinga na upuuzi wa Hali ya juu sana Kwa mzazi ambae huna assets za maana kujistress kulipa mamilioni shule za EM
Mganga wa kienyeji anatema kizungu
 
Mkuu kwa nini unapinga ushahidi wa wazi.
Mtoa mada hajatoa conclusion kama ulivyodai. Ni open discussion ambayo inatakiwa itupe tafakuri. Kila mmoja atafakari mwisho wa siku wa anachokifanya.
Dhana ya kufungua kampuni ndio suluhisho la kizazi kijacho. Unakuta ulionza nao primary mpaka chuo kikuu hakuna alie anzisha kampuni hata mmoja. Wakati hao waasia ni wachache ila wanaongoza kwa makampuni.
Kampuni si ndio msingi wa ajira kwa dunia ya sasa.
Nadhani kuna namna inatakiwa turekebishe akilili zetu kutoka mazoea na kuwa wabunifu zaidi.
Kama ajira ni chache kwa nini uendelee kutumia gharama kubwa wakati hujui nani atamuajiri mwanao. Kwa nini familia sasa zisiwe chanzo cha kubuni ajira ya watoto wao ?
Wekeza kwenye hio ilimu ila ukumbuke kumuandalia cha kufanya baada ya kuhitimu.
Sisi wenye watoto wanaosoma tuchukue tahadhari, tupambane kuwaaandalia mazingira watoto. Kila mtu anaelimu siku hizi. Tena mitandao ndio imemaliza value ya elimu. Ila sio kila mtu anapesa na investment.
 
Mkuu kwa nini unapinga ushahidi wa wazi.
Ushahidi gani ? mwisho wa siku binadamu anatakiwa kupata atleast basic needs ili aweze kusurvive bila hivyo atachukua hata chako wewe tajiri.., In short kutakuwa hakuna Society, hivyo hao kama wanapata mkate wao wa kila siku all the best
Mtoa mada hajatoa conclusion kama ulivyodai. Ni open discussion ambayo inatakiwa itupe tafakuri. Kila mmoja atafakari mwisho wa siku wa anachokifanya.
Pili hii ni fallacy watu hawasomi tu ili wapate pesa ingekuwa hivyo wenye pesa wasingesoma.., wanachofanya hao wazazi ni part ya wenyewe wanachokiona ni wajibu wao (kumpatia mwanao elimu bora iwezekanavyo) na hapo kabla elimu ndio ilikuwa ufunguo wa maisha (ingawa dhima ya elimu ilikuwa ni kumpatia mtu nyenzo za kupambana na mazingira yake yaani kuondoa ujinga) hivyo hata asiyekwenda shule kama amejifunza / anajifunza hio ni Elimu....

Kwahio kama elimu imekuwa not fit for purpose au ya gharama wakati watu tunatoa Kodi basi wa kulaumu sio wazazi wanaojinyima kumpa mwanao all they can bali ni wale tunaowalipa Kodi zetu kushindwa kuja na mbinu za kufanya Elimu kuwa fit for purpose.
Dhana ya kufungua kampuni ndio suluhisho la kizazi kijacho.
Hii ni fallacy ya kipuuzi sana.., watu wanadhani kufungua Kampuni (kuipa Serikali njia zaidi ya kula kodi na jasho lako) ni jambo rahisi..., Mtaani ni pagumu balaa na sio kila mtu anapaweza kunahitaji discpline ambayo waliyonayo ni wachache sana katika biashara 100 zinazoanzishwa ulimwenguni asilimia mpaka 90 zinafeli katika mwaka wa kwanza tu..., kwahio the only sure thing kama taifa ni kuhakikisha kunakuwa na middle income ya kutosha watu wanaoweza kupata ujira kwa kufanya lolote (be it hao mawinga ambao ni kosa la serikali kutokuwa na infrastructure hivyo taifa la madalali na wachuuzi) au kuwa na Sera za kuweza kutumia nguvu kazi iliyopo ili watu wapate ujira..., sababu na hii ni cha mtoto mbegu tunazopanda za upuuzi tunaofanya leo tutaanza kuuvuna hapo kesho
Unakuta ulionza nao primary mpaka chuo kikuu hakuna alie anzisha kampuni hata mmoja. Wakati hao waasia ni wachache ila wanaongoza kwa makampuni.
Hao waasia wengi ushaenda kwao na umekuta wanafanya nini, hakuna nchi yenye matabaka na mafukara wa kutosha kama India, kwahio hawa unaowaona huku ndio baadhi ya creme de la creme; Au ushakutana na watanzania waliopo ughaibuni wanavyochapa kazi; hata ukiwa na waafrika laki moja wenye makampuni bongo (tena wapo wengi nenda Brela) ila ndio hivyo wengi ni makampuni ya briefcase na kampuni zinazopumulia mashine..., na hata zingekuwa kampuni bora kama mia 200 (je katika karne hii ya teknolojia na mashine) Kampuni hazihitaji tena watu wa kufanya kazi (kutoa ajira) unategemea hao waliobaki watafanya nini ? Au kila mtu aanzishe kampuni yake ili tuweze kuuza bidhaa za mchina na kuuza vya kuuza (bandari n.k.) siku vikiisha turudi kufanya kile ambacho tunaona leo hii hakifai?
Kampuni si ndio msingi wa ajira kwa dunia ya sasa.
Kampuni ? Kampuni ni chombo kilichoanzishwa miaka na miaka nyuma huko iliyopita ili kuondoa risk / uwajibikaji wa mtu binafsi kama mambo yakienda kombo..., na ndio chombo kilichogundua kwamba unaweza kuuza share kwa wengine hivyo ukipata faida au hasara na wao wanapata bila kufanya shughuli moja kwa moja..., na ndio hizo kampuni zilizokuja na kuleta ukoloni nchini Afrika kwa kupewa support na nchi zao..., Dunia ya sasa tena unaweza ukasema uanzishe Kampuni huende Brela tena na Kodi zetu hizi ukawa unacheza kwa kuwapa walamba asali faida (Kwahio kwa ushauri kama una tender sehemu au requirement kwamba huwezi kupata kazi bila kuwa Kampuni wala usiende huko) utabakia kuifanyia kazi Serikali...
Nadhani kuna namna inatakiwa turekebishe akilili zetu kutoka mazoea na kuwa wabunifu zaidi.
Hakuna jipya hapa ambalo utabuni halijawahi kufanyika ila kuna mazingira yanabadilika hivyo inabidi kama taifa / dunia tubadilike na sio mtu mmoja mmoja; yaani kama utumwa ulivyomalizwa na Industrial Revolution na ndivyo hivyo hivyo hii Capitalism as we know it today itamalizwa na Teknolojia / Automation.., sababu it no longer create employment....

Kama ajira ni chache kwa nini uendelee kutumia gharama kubwa wakati hujui nani atamuajiri mwanao. Kwa nini familia sasa zisiwe chanzo cha kubuni ajira ya watoto wao ?
Yaani hata kabla haujawaza na kufanya jambo ambalo litamsaidia mwanao miaka ishirini from now majority hata hawajui kama kesho watakula au jioni watakula (na kumbuka kumfanyia mwanao na kumpa pensheni hio sio wajibu bali ziada) ila kumpeleka shule na kumlisha ni wajibu na kazi yako wala sio ombi (kama ulishindwa kufanya hayo basi usingeanzisha familia). Pili huwezi kumpangia mwanao maisha huenda ukasema uanzishe law Firm au Hospital ila kumbe yeye msanii na anapenda kuimba (then what?!!) Au ndio hapo mnaanza kukosana ? Cha maana kama uwezo unao mfungulie akaunti na muwekee pesa huko fixed akaunti ili siku akifikisha miaka kadhaa mpe afanye anachotaka..., Tatizo una equate maisha na Pesa


Wekeza kwenye hio ilimu ila ukumbuke kumuandalia cha kufanya baada ya kuhitimu.
Unachoongelea ni cha kusadikika na out of touch.., moja huwezi kumuandalia mtu cha kufanya mtu sio robot na ana matakwa yake na anachopenda (nimeona familia nyingi vita kazi ya wazazi na watoto kutokana na kulazimishana cha kufanya) mbili unaongelea watu ambao hata milo mitatu hawana wapangie watoto cha kufanya baada ya miaka 20 ?; Si wangeweza hicho wangefanya leo ? Kwahio again badala ya kulalamikia wazazi lalamikia serikali yako kutokuwa na miundombinu sahihi ya wananchi wake kuwa na disposable income

Sisi wenye watoto wanaosoma tuchukue tahadhari, tupambane kuwaaandalia mazingira watoto. Kila mtu anaelimu siku hizi. Tena mitandao ndio imemaliza value ya elimu. Ila sio kila mtu anapesa na investment.
Kama unadhani kila mtu ana discipline ya investment think again (hakuna mtu ambaye hajui kwamba akinunua nyanya Tshs 10 akauza 12, na akanunua tena na kuuza 12 na kuongezea mtaji kwenye mtaji na mtaji mwisho wa siku mtaji utakua mkubwa na hivyo kupata faida na faida) ila tatizo ni kufanya kile ambacho anajua...

Kwahio kwa jamii zote kwa kufahamu hilo ndio maana wanahakikisha wananchi wao walipa kodi wanapata ujira na kuwa na insurance ya pensheni ili mwisho wa siku wasiwe mzigo kwa jamii
 
Mchepuko hauwezi kumaliza milion 4 kwa mwaka hata niwe nayo kumi

Sasa ada ya mtoto kwa mwaka ni shingapi kutaka kujimwambafai tu mtaani na nyie muonekane
Kwamba unataka kusema wanaume huwa mna mchepuko mmoja na kingine huyo mchepuko wako anatoka kijiji gani hadi hamalizi milioni nne kwa mwaka, hivi wanaume wenzio wanaposema mambo yanayoongoza kuwamalizia pesa ni pombe na wanawake huwa wanamaanisha nini unafikiri, by the way hata kama wa kwako hamalizi ila bado hizo hela unazohonga ungeweza kuongezea kwenye ada ya mwanao every penny counts remember
 
Hili ni suala muhimu na la kimjadala sana, wazazi wengi wanao na waliosomesha watoto wao shule za gharama ni watumishi wa umma na wafanyabiashara kwa wale walikuwa na bahati kutoka familia za biashara unawakuta kwenye baishara za wazazi hala ula kwa wale watoto wa watumishi wa umma na parivate companies kama hawajapata kazi na mzazi hana biashara ni majanga makubwa. Inasikistisha sana unapokutana na mdangaji graduate. Suala la ajira na kuwa mfumo unaopelekea watu kujiajiri ni muhimu sana. Aidha kuwa na skills nacho ni kitu muhimu. Mtoto wa mkulima anaweza kuwa bodaboda baada ya chuo aliyekuwa anakula mkate na siagi kila siku atakuwa nani..?
 
Kwahiyo akilipa ada kubwa kwa mtoto ndio hatachepuka sijui huwa mnawazaga ushubwada gani wanawake

Upo tayar mtoto aletwe na gari kwa ada ya mil6 kwa mwaka au zaidi wakati hata nyumba mmepanga eti kisa atahonga

After all na miada yote hiyo mtoto akimaliza anakuwa kama wa mleta mada hana la kufanya kwani wazazi hamna connection yoyote ya kumsaidia mtoto

Kwa hali hiyo si bora kweli nitumie izo pesa nizigawe nyingine nijengee au nifanye maendeleo mengine nyingine nikale mbususu niufaidishe mwili
 
Pili hii ni fallacy watu hawasomi tu ili wapate pesa ingekuwa hivyo wenye pesa wasingesoma..,
Is it ? Ili iweje. Waliposema elimu ni ufunguo wa maisha walimaanisha maisha yepi ?
Kuna masisha bila pesa ? Kwa hio watu wanasoma tu kujifurahisha ? Kama ni hivyo kwa nini vijana wanadai ajira ?
Hao wenye pesa wameishajua kuwa elimu ni pesa na ndio maana wanaendelea kusomesha. Dhana ya kuwa hatusomi tupate pesa umeitoa wapi ?
Je kazi ya maarifa unayopata shule ni ya kujifurahisha tu ? Mbona Eliku ni mateso bila pesa hakuna atakae vutiwa nayo.
Mvuto wa elimu umepungua kwa kuwa mtu hana uhakika wa ajira.
Tusidanganyane, wewe unaingiza pesa kupitia hio elimu ndio maana huoni shida wanayopitia vijana waliowekeza muda na mamilioni ili waje wapate kazi.
Hizo fedha boy nk zipi juwandaa wanafunzi wawe bora kulio wenzao ili wawashindekwenye kazi. Sikuzuii mtazamo wako ila kwa wengi ni Elimu ni pesa, kazi, mamlaka nk.
Wazungu wanatusumbua kwa swbabu ya elimu ambayo inawaingizia mabilioni ya fedha.
ELIMU BILA PESA HAINA MAANA YOYOTE.
 
Hii sio chai waulize wazazi waliosomesha watoto mpaka vyuo vya ulaya na mpaka sasa hawana kazi. Wazazi tunaumia sana. Watoto wanazidi kuzeeka miaka inasonga mbele kazi hakuna. Kazi aliyosomea akiomba hapati. Hatukuwatayarisha kufanya biashara hata ufundi wala kilimo. Mfumo haukuwa hivyo. Pengine tungewasomesha kiasi tu waweze kujitegemea ktk fani fulani mapema. Hebu fikiria kazi za viwandani au binafsi watoto wanalipwa 200,000 kwa mwezi. Unamlipia nauli na pengine unaishi nao. Hiyo mshahara ndio anajinunulia mavazi nk. Ili mradi asikae nyumbani akapata msongo wa akili. Usiombe yakukute. Kama madaktari wa watu WANAKOSA KAZI NA KUAJIRIWA ZAHANATI BINAFSI KWA KAMSHAHARA KADOGO AU KUKOSA PIA HATA HIYO BINAFSI.
 
Hadithi za Abunuwasi hizi, hats hivyo kiingereza siyo elimu, kule Uingereza ht wehu huongea kiingereza
 
Mtu mzima unakuja na hoja za kiumaskini na wivu🚮
 
wahindi na Wachaga wanasomesha watoto shule za gharama ila wanabalance wanamiliki na biashara za familia pia.

Ni upuuzi kuwekeza hela yote ya familia kwenye kusomesha tu
Hao wachaga umewataja kishabiki uhalisia hauko hivyo. Wachaga bd maskini km makabila mengine Tena wao Wana hali mbaya maana hawana rasilimali ya maana. Unalinganisha wachaga na wahindi? We kwl hamnazo.
 
Narudia tena kusema hili, na ntalisema hili kila wakati. "Kama una uwezo wa kumsomesha mtoto shule nzuri, basi fanya hivyo maana itamsaidia mtoto kuanzia mbele ya ulipoanzia kimawazo katika harakati za kutafuta maisha."

Huwezi kufananisha thinking na reasoning ability ya mtoto aliyesoma kayumba na mtoto aliyesoma shule zinazojitambua. Nina mifano halisi kwenye hili na hata mtoa mada ukitaka kupprove hili tafuta mtoto wa std 5 anayesoma moja ya shule tano bora za msingi za EM katika eneo ulilopo ujadili nae jambo kwenye angle yeyote ile ya maisha then nenda tafuta mtoto aliye form 2 aliyesoma pure kayumba ujadili nae jambo lilelile halafu uje ufute uzi wako hapa haraka.
 
Maisha ni mipango, ila jamii yetu bado wanafikiria maisha ni bahati na nasibu. hata huyo winga akiamua kuwa na mipango dhabiti atakuja kutoboa. Swala la elimu ya darasani yaani shuleni haitoshi, mtoto inahitajika kuandaliwa na lifeskills za kazi mtaani au nyumbani akiwa bado anasoma yaani mdogo. Asilimia kubwa Elimu ya darasani ni kwaajili ya ajira tu
 
Is it ? Ili iweje. Waliposema elimu ni ufunguo wa maisha walimaanisha maisha yepi ?
Kuna masisha bila pesa ? Kwa hio watu wanasoma tu kujifurahisha ? Kama ni hivyo kwa nini vijana wanadai ajira ?
Elimu inaleta ufahamu hata upate pesa haimaanishi kwamba elimu imekwisha au ndio mwanzo na mwisho wa elimu

Na nimekwambia elimu ilikuwa ufunguo wa maisha wakati system ilikuwa sustainable kama jamii inawapa watu elimu / ufahamu ambao ni nguvu kazi ya kuweza kuja kutumikia taifa hivyo mwisho wa siku mtu huyu ana guarantee ya kupata ujira Unaongelea maisha bila pesa (hivi unajua pesa ilikuja baadae katika mfumo wa maisha ya binadamu)? Bila ni kirahisishi cha maisha (a means to an end ila sio the end of the means)
"Only when the last tree has been cut down, the last fish been caught, and the last stream poisoned, will we realize we cannot eat money."
Hao wenye pesa wameishajua kuwa elimu ni pesa na ndio maana wanaendelea kusomesha. Dhana ya kuwa hatusomi tupate pesa umeitoa wapi ?
Kwahio kwa akili yako kina Prince Williams, au Dangato au watoto wa Wafalme hawasomi sababu tayari wana pesa ?

Mtu anayesoma Bible Studies au Historia ya Mkoa fulani anafanya hivyo ili apewe pesa kiasi gani ? Mwingine anakusanya Degrees kama Prestiege utampangia huyo ? Na kama nchi tunafundisha watu wapate pesa au waweze kufanya kile kinachohitajika kufanyika ?
Je kazi ya maarifa unayopata shule ni ya kujifurahisha tu ? Mbona Eliku ni mateso bila pesa hakuna atakae vutiwa nayo.
Unaangalia vitu kwa mafungu tena kwa perspective yako na sio perception ya watu tofauti unaongelea Elimu ni mateso ? Binadamu ni enqisitive by nature kwahio wanataka kupata ufahamu.., unadhani kina Faraday, Newton walifanya wanachofanya ili wapate pesa kiasi gani ? Au wale watafiti wanaotoka kwao na kutumia pesa za ukoo mzima kuhamia kwenye mapori kufanya utafiti wa Archives wanafanya hivyo ili walipwe nini ?
Mvuto wa elimu umepungua kwa kuwa mtu hana uhakika wa ajira.
ajira ni pesa au ajira ni Security ? Na elimu ni shule au Elimu ni uelewa ? Ukishafahamu hayo nadhani tutaweza kuongelea mambo kwenye page moja..., Na kwa kuona kwako hakuna ajira ukaona suluhisho ni kuondoa Elimu ?
Tusidanganyane, wewe unaingiza pesa kupitia hio elimu ndio maana huoni shida wanayopitia vijana waliowekeza muda na mamilioni ili waje wapate kazi.
Ningekuwa nawaza hayo ningekuwekea nyuzi za kutosha ninazolalamikia status quo na kinachoendelea sasa hivi ?
Hizo fedha boy nk zipi juwandaa wanafunzi wawe bora kulio wenzao ili wawashindekwenye kazi.
Rudia uzi wangu kwanini unaishi na moja ya kazi ya mzazi ni kuhakikisha mwanae anapata elimu (wala hio sio hisani ni wajibu) sasa mwingine anaona prestige au mwanae akienda shule nyingine ananungunika kwahio yeye yupo radhi asumbuke maisha yake yote ili mwanae aende shule kama hizo ambazo kuna guarantee ya division one (be it ataelewa au hapana) hayo ni maisha yake na uchaguzi wake hatuwezi kumpangia..., Ila kama elimu haifai na ni gharama siwezi kulaumu mzazi aliyempeleka mtoto Fedha Boys bali Serikali ninayoilipa Kodi kwanini hizi shule nyingine haziwi kama ile...

Hilo moja la pili ndio hili tunafanyaje katika dunia ya leo ambayo nguvu kazi haina tena demand kuhakikisha wananchi wanapata ujira ? (Je kwa kila mtu kuwa mchuuzi au kuhakikisha kuna vyanzo vya UMMA pia ambavyo vinasaidia majority..., yaani badala ya kumpa Bandari mtu wa mbali UMMA unasimamia kwa ajili ya kupata Makusanyo 100 percent hivyo kupunguza kumbana huyu mbangaizaji)


Sikuzuii mtazamo wako ila kwa wengi ni Elimu ni pesa, kazi, mamlaka nk.
Sasa hapo umetoka kwenye Pesa umekuja kwenye kazi mamlaka n.k. (in short umejumuisha kila kitu) na kumbuka hapo umeweka security ambayo ukiwa na pesa utapata basic needs (chakula malazi na mavazi) ila unaweza ukapata hayo ukiwa kijijini bila pesa au unaweza ukapata pesa, kazi mamlaka na vinginevyo bila elimu ya shule (ingawa hakuna mtu asiye na elimu sababu kujifunza sio lazima uende shule)..., Lakini kama watu hawana hizo basic needs basi hio sio Jamii sababu kitawaka na watu kukabana mitaani

Extreme Poverty anywhere is the three to Society Everywhere....
Wazungu wanatusumbua kwa swbabu ya elimu ambayo inawaingizia mabilioni ya fedha.
ELIMU BILA PESA HAINA MAANA YOYOTE.
Elimu ni uelewa na hakuna mtu ambaye hana elimu hata wewe kuingia humu na kuweza kuandika unayoandika ni Elimu..., sasa kuhusu umaana ndio hapo tunakuja mtu binafsi..., mwingine mzazi anataka tu prestige kwamba watoto wangu wanasoma sehemu fulani (kwahio anakuwa ametimiza wajibu wake wa kusomesha na kulala kwa furaha kwamba kama baba / mama amefanya kile amacho kwake ndio anaona kinafaa) Na kuhusu pesa kila mtu akipata pesa sawa kwa kila wakati basi kutakuwa na inflation sababu watu hawali pesa (vya kununua vitakuwa vichache kuliko cha kununulia) hivyo basi badala ya kuangalia nyenzo (pesa) tuangalie kile kinachotafutwa na pesa (mahitaji) na yawe na gharama ambayo kila mtu anaweza kuimudu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…