Ni asilimia 21 tu zitaenda kwa Wazanzibari katika Nafasi 1,097 za kazi kutoka TRA, marekebisho yanahitajika

Ni asilimia 21 tu zitaenda kwa Wazanzibari katika Nafasi 1,097 za kazi kutoka TRA, marekebisho yanahitajika

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
1635155698485.png

Kwanza nitoe pongezi kwa serikali iliyosikia kilio cha vijana kwa kutoa ajira zaidi ya elf 1 TRA.

Kama mnavyojua, Kwenye ajira wazanzibar hupewa asilimia 21, kwa hio katika hizi nafasi 1,097 ni sawa na wazanzibari 230 tu,

230 hao bado ni wachache kulingana na idadi kubwa ya vijana wanaomaliza vyuo

Naona ingependeza walau kuwe na wazanzibar 300 ili kufidia fidia vijana wengi ambao bado wapo mitaani na degree zao.
 
Tuwe wawazi hizo nafasi zigawiwe kwa kulinganisha idadi ya wakazi, say 60,000,000 kwa 1,500,000; then update asilimia ratio
Zanzibar ni nchi kamili. Sio sawa na mwanza ama mbeya huko wanakoangalia usawa wa idadi wanapogawa pembejeo.

Jiulize kwanini Zanzibar lazima iwe na raia wake katika vyeo viwili vya juu kila awamu yaani mgombea urais na mgombea mwenza wa Tanzania ni lazima mmojawapo atoke zanzibar kila awamu.

Maswala ya idadi ni kwenye mikoa sio nchi
 
Tunaposema Rais Samia anatoa ajira muwe mnaelewa,

Kasi ya Rais wetu inatia moyo kwa kila Mtanzania,

Hongera Rais Samia kwa ajira mpya tuko na wewe daima ,
Kwa hili la ajira nampongeza maana kaupiga mwingi kwerikweri in Jiwes voice
 
si mkaajiriwe kwenu zanzibar huku tanganyika mnafuta nini
Muungano si mnaupenda sasa hasira hizi unatoa wapi? 🙂 🙂

Mashirika ya zanzibar mengi yameshajaa mkuu, kwa sasa wacha vijana wajaribu bahati yao hizi ajira mpya za muungano.

TRA ni mamlaka ya mapato Tanzania sio mamlaka ya mapato Tanganyika.

Tanganyika + Zanzibar = Tanzania

Nakutakia mchana mwema .
 
si mkaajiriwe kwenu zanzibar huku tanganyika mnafuta nini

Ajira sio za tanganyika ni za Tanzania.

Jiulize kirefu cha TRA je ni Tanganyika revenue authority ama Tanzania revenue authority?

Wa Zanzibar wana haki ya kisheria katika ajira za Tanzania zote. Ingekuwa za Tanganyika ungekuwa sahihi
 
Wanzanzibar subirini za kwenu za ZRB, nyie ndo mnaongeza uhaba wa ajira Bara, hakuna mbara aliyeko ZRB au ZSSF lakini nyie mko bara mmejazana, wabara tulioko huku znz tuko kibishi lakini hamtaki hata kutuona
 
ZRB na ZSSF ni mashirika ya serikali ya zanzibar

TRA ni shirika la nchi mbili Tanganyika na Zazibar inayounda Tanzania

JIONGEZE!!
 
Ajira sio za tanganyika ni za Tanzania.

Jiulize kirefu cha TRA je ni Tanganyika revenue authority ama Tanzania revenue authority?

Wa Zanzibar wana haki ya kisheria katika ajira za Tanzania zote. Ingekuwa za Tanganyika ungekuwa sahihi
Kuna mzanzibari anaijua Tanzania kweli? Ikiwa mnaijua Tanzania. Leseni ya udereva imeandikwa JMT lakini haitakiwi kutumika znz, unakamatwa na askari aliyevaa nembo ya Jamhuri ya muungano wa Tz.

Ukiiuliza unaambiwa si suala la kimuungano. Huu muungano unawanyonya wabara tu. Mzanzibari kujenga nyumba bara si hoja lkn mbara kujenga nyumba zanzibar ni habari.

Mzanzibari kumiliki duka la vileo ni halali lakini kwa mbara zanzibar ni nchi ya kiislam. Aisee nyie mimi nawachukia sana kwa sababu ni wabaguzi kuliko kawa
 
Back
Top Bottom