Nilipe nisepe
JF-Expert Member
- Sep 9, 2024
- 1,467
- 3,496
Mtu akifaa na hela zake zinakufaa!,
Acha kusumbua watu na wewe tafuta zako,pesa za marehemu zimekufa nae.
Acha kusumbua watu na wewe tafuta zako,pesa za marehemu zimekufa nae.
Nani alihusishwa na marehemu kabla hajafa aliweka wapi hiyo pesa siku aliyo lipwa na ilibaki hapo siku zote?Hapana Kuna scenario unakuta mtu ameuza shamba walau m100 baada ya wiki kafariki na hakuna kinachoonekana kwenye acc,
Mkuu kuna NMB na CRDB hawajambo kukata pesa za watu na hii inajulikana, yaani hata ukiwa unapumua.Ni banki kubwa tuu yaani,kwa sababu za kisheria siwezi kutaja majina
Mtu kauza shamba hela zimeingia akazitoa labda kulipa deni au katapeliwa utajuaje mkuu?Hapana Kuna scenario unakuta mtu ameuza shamba walau m100 baada ya wiki kafariki na hakuna kinachoonekana kwenye acc,
Mkuu nimewahi kufanya kazi Bank mwaka mmoja na na miezi kadhaa.Ni sawa japo hili haifichi ukweli kuwa Wafanyakazi wengi wa Mabenki huchomoa fedha kwenye account za watu mara baada ya kuona account ipo domant ndani ya miezi 3 hadi sita wakiamini kwamba wateja wanaweza kuwa wamekufa.
Refer kesi ya mzee mmoja kule Arusha dhidi ya NMB kwa kuchukuliwa kwa 100M kwenye account yake kinyemela.
Hicho ulichoandika ni hypothetical, uncouth, uncultured and immaterial!Kwenye harakati za maisha nimekutana na mambo ya kustajabisha ya ajabu:
Case1: jamaa alikuwa mfanyabiashara akamfungulia mtoto wake acc kwa majina yake kimsingi humo ndio alikuwa anamwekea dogo fees na Hela ya ada.sasa siku moja huyo mdingi kamwekea dogo Hela ya ada kama kawa na baadae dingi akaana kuumwa,dogo kujaribu kuvuta mpunga kadi ikasumbua dogo alivyojielezea wakamwambia mwenye acc afike,dingi hakuweza kufika na alifariki dunia.dogo kafuatikia mirathi avuta zake mpunga amalizie masomo,jamaa wakamwambia mwenye acc yako Kuna 500000tuu,basi dogo akawaambia chukueni na hiyo.dogo akaacha na chuo.
Case 2.jamaa dada yake alikuwa mwajiriwa wa serikali ,akawa anaumwa lakini akaamua kuprocess mkopo kama 25m hivi,mkopo ukawa umeingia vizuri,Sasa kimbembe baada ya siku chache yule dada akavuta uzi.msimamizi wa mirathi hakuna kitu kwenye acc.Mambo haya yote yemenifikirisha sana kuhusu usalama wa pesa zetu.ninaomba ushauri ni nini kinatakiwa kufanyika pindi unapokuwa na kiasi kikubwa cha pesa bank,je ni benki gani hawana tabia za kijinga jinga ,au ni namna gani wakuu mnahifafhi fedha zenu
Mkuu hizi ni KASUMBA tu za mitaani hela za bank hazikwapuliwi kama unachukua maembe shambani........Watu wanazitetea benki kwa sababu hayajawakuta, lakini mtu akifariki wafanyakazi wa benki ni wezi, wakigundua mtu kafa, wao ndio wakwanza kukutaarifu kuwa fedha zimesharudishwa BOT, uongo mtupu
Kuna uzi humu walilamba 100M ya mzee mmoja pale Arusha so yote inawezekana.Mkuu nimewahi kufanya kazi Bank mwaka mmoja na na miezi kadhaa.
HAKUNA mtumishi wa Bank anaweza kurisk kazi yake kwa kutoa hela mazima ya mteja akidhani amekufa au hata akijua amekufa...... Hili ndio KOSA kubwa sana kwa watumishi wa Bank na manemejimeti huwa zipo seriou sana kwenye kosa hili....UNAFUNGWA mchana kweupeee
Bankers wasio waaminifu huwa wanachungulia acc ambazo zina mzigo mkubwa na zipo DOMANT kwamuda labda unakuta Acc huwa inaingiza au kutoa hela mara moja tu kwa mwaka mwezi wa 12 tu na ina B za kutosha.
Kuna wajuba huwa wanataka hela za fasta labda 500M anafanyia shughuli yake ndani ya miezi mitatu kisha anarudisha 600m...,. Hapo ndio watumishi wanachangamkia wanaitoa kinyemela anapewa mjuba na baada ya miezi mitatu anarudisha 600, wanarudisha 500 kwenye acc ya watu wao wanakula 100m
Hapo balaa ni mwenye acc akitokea ghafla akakuta hela imepingua. Au anaweza kuomba bank statement akaona hela ilitoka kwa miezi kadhaa ikarudi na hautambui huo muamala
Lakini kuiba mazima hela ya mteja kwa Bank ni next to impossible..... Risk ni kubwa mmno KUFUNGWA