Ni baraka kwa introvert kujifahamu kuwa ni introvert na kuamua kuutumia uintrovert wake kwa manufaa!

Uwe na kifua cha kuvumilia neno "ubinafsi" .Introvert ina tafsiri ya ubinafsi, sana kama upo kwenye Community (sio kweny society)
Sidhani kama introverts ni wabinafsi. Mimi watu wengi wananiambia nina sifa za introverts na nimekuwa nikitoa sehemu ya resources zangu kwa wengine hasa wahitaji including muda. Hii pia imekuwa ni kitu ambacho nakifurahia
 
Magonjwa ya kizungu hayo
Magonjwa ya Kizungu? Basi Wazungu wana bahati sana!

~ Wakati magonjwa ya Kiafrika kama kipindupindu yakihatarisha uhai wa Waafrika, magonjwa yao yaitwayo INTROVERT yanawafikirisha na kuibuka na chanjo kwa ajili ya watu wao.

~ Wakati magonjwa ya Kiafrika kama Malaria yakiwarudisha Waafrika nyuma kimaendeleo, magonjwa ya Wazungu yaitwayo INTROVERT yanawasaidia kusonga mbele kupitia ubunifu wa Kisayansi na Kiteknolojia.

Wazungu wana bahati sana! Ugonjwa wao wa introvert umewazalia watu ambao wamekuwa na manufaa makubwa kwa Mataifa yao: Barack Obama, Vladmir Putin, Thomas Edison, Abraham Lincoln, Warren Buffett, Hillary Clinton, Elon Musk, n.k.
 
Elon hpn kwa Kweli tajiri yule anaropoka ropoka snaa kila dkika 5 anatwit no siyo
 
Naona uanttauta watu wake pm Kwamba wee Ni mtabiri
 
Mtu wa hivi hata kwenye Misiba au Harusi au Shughuli tu za wanaomuhusu kama ndugu au marafiki utakuta anakwepa. Atachanga vizuri tu kama ni harusi lakin ikija kadi anagawa.
 
Mtu wa hivi hata kwenye Misiba au Harusi au Shughuli tu za wanaomuhusu kama ndugu au marafiki utakuta anakwepa. Atachanga vizuri tu kama ni harusi lakin ikija kadi anagawa.
Na ukiona amekuja kwenye sherehe yako, ujue ni kwa sababu amekuheshimu tu. Hana "time" na sherehe yako. Ungemwomba akuchangie tu lakini asihudhurie, angeweza kukuongezea na hela ya ziada ya "asante" kwa kutokumsumbua.
 
V
Vitu vingine tuwaachie wazungu, asili yetu ni kujichanganya hao wanaoiga uzungu wanajipa stress bure tu.
Chura anaweza kuishi majini na nchi kavu, lakini kuna mazingira anayoyapendelea zaidi kati ya hayo mawili.

Mamba anaweza kupambana hata akiwa nchi kavu, lakini akiwa majini anakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda.

Ndivyo ilivyo kwa introvert. Yeye si anti - social, bali anafurahia zaidi mazingira fulani yaliyo kinyume na yale ya extrovert.

Kama ni mazungumzo ya kupiga tu stori, anapenda kufanya na mtu aliyezoeana naye, tuseme, rafiki yake wa karibu.

Iko hivi! "Chaji" ya introvert inakuwa ipo full muda wote, wakati extrovert inakuwa na nafasi inayohitaji kujazwa na "makelele", n.k.

Hiyo ndiyo inayomfanya extrovert apende "kuzurura"! Anapokutana na watu na mazingira ya kelele kunalisaidia "tenki" lake kujaa.
 
Hata mm kwa huyo nimeshangaa jamaa ana maneno mengi sana huyo kila leo na tweet zake za utata utata
Kwanza, ninakiri kuwa simfahamu Elon Mask, zaidi ya kumsoma google, n.k.

Mitandao yangu pendwa ni JAMII FORUM na QUORA. Twitter, Facebook n.k. simo, kwa hiyo sijui anachopost Musk.

Lakini kwa mujibu wa wanaoifahamu, yeye mwenyewe akiwemo, wanasema ni INTROVERT!

Kuna wakati alishawahi kusema kati ya mambo ambayo huwa anafanya tu kwa kuwa inamlazimu, ni kuongea mbele za watu. Hayupo comfortable katika hilo.

Suala la yeye kupost twitter hakumuondolei uintrovert. Labda tu ujue kuwa kati ya eneo ambalo maintrovert wanalimudu sana ni kuwasiliana kwa njia ya maandishi. Hata vitabu vingi vinavyouzwa sana waandishi wake wengi ni Introvert.

Introvert ni hodari wa kuandika, lakini hapendi kuongea sana.
 
Hata mm kwa huyo nimeshangaa jamaa ana maneno mengi sana huyo kila leo na tweet zake za utata utata
Kwanza, ninakiri kuwa simfahamu Elon Mask, zaidi ya kumsoma google, n.k.

Mitandao yangu pendwa ni JAMII FORUM na QUORA. Twitter, Facebook n.k. simo, kwa hiyo sijui anachopost Musk.

Lakini kwa mujibu wa wanaomfahamu, yeye mwenyewe akiwemo, wanasema ni INTROVERT!

Kuna wakati alishawahi kusema kati ya mambo ambayo huwa anafanya tu kwa kuwa inamlazimu, ni kuongea mbele za watu. Hayupo comfortable katika hilo.

Suala la yeye kupost twitter hakumuondolei uintrovert. Labda tu ujue kuwa kati ya eneo ambalo maintrovert wanalimudu sana ni kuwasiliana kwa njia ya maandishi. Hata vitabu vingi vinavyouzwa sana waandishi wake wengi ni Introvert.
 
Unaweza kukuta ile account zake za mitandaoni anaendesha mtu mwingne on behalf. Yeye yuko zake busy huko kwingne hana habari.
 
Mimi ni introvert mixture ya melancholy na phlegmatic, kuna introverts ambao ni waongeaji wakiwa tu na watu waliowazoea na huwa wakimya sana wakiwa na watu wasiowazoea, na huyo ni mimi

Mimi kuna ndugu na jamaa zangu ambao sijawazoea wanajua mimi mkimya sana, ukiwaambia ni muongeaji wanakataa katakata, wakati kuna marafiki zangu niliowazoea wanajua mimi muongeaji sana

Hata shuleni ulikuwa ukiwauliza classmates mimi ni mtu wa aina gani, wanakuambia mimi mkimya sana ila wakati huo huo ulikuwa ukiwauliza roommates, wanakuambia mimi muongeaji sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…