Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Ukipanda basi mwite konda muulize hivi sehemu fulani tunafika saa ngapi? Akikujibu hivi “ hivi ni vyombo vya moto tuombe tu Mungu jua tayari umepatikana,
au ukisikia inategemea barabarani kukoje

mimi nilipanda basi linaitwa simba mtoto natoka TANGA naja DAR
nilichelewa nikakuta RATCO ishajaa
na basi ya mwisho ndio hiyo SIMBA MTOTO
huweziami i ile basi inatembea na FUNDI
Kutoka saa 11 tanga tumefika UBUNGO saa 8 usiku kilaa baada kilometer kadhaa FUNDI anashuka chini Uvunguni

nikahapa sitapanda lile basi tena
 
Mwaka 2014 kwa mara ya kwanza kwenda moshi .imefika saa sita mchana inatakiwa nirudi darkesho,nikaforce nisilipe hotel niondoke siku hiyo hiyo.nilipanda za kenya kuja dar kama sikosei ni Akida.basi tulifika kariakoo saa saba usiku.yaani wao ni mizigo na kupekuliwa pekuliwa. Karibu kila maeneo ya ukaguzi plus taarifa kuwa wanalala njiani hawalali hotelin bongo.mara ya pili tahmeed la kutoka kenya kupitia tanga hadi dar .nalo flilipata ukaguzi plus .
 
NEW FORCE.. sitapanda kwa sababu si waaminifu. Niliagiza parcel flan hv from dar to tukuyu, lakin baada ya mzigo kufika tukuyu wakaanza kunipiga chenga akat mzigo ulishalipiwa kila kitu. Nmekereka mpaka leo.
 
Kampuni ya Sai baba bado nipo? Kwa kweli at their prime, ilikuwa ni kampuni nzuri na marcopolo zao zile wakati ule ndiyo fashion
Nazionaga bado zipo but kuzipanda hapana.
Huwa zinasimama hovyo njiani haziachi abitlria hata wa 2,000!
 
Tate niko njiani hapa natoka Tanga, yaan naona wengi wanasema Nacharo, Tashriff au Ratco ndio yako vizuri,
 
Tate niko njiani hapa natoka Tanga, yaan naona wengi wanasema Nacharo, Tashriff au Ratco ndio yako vizuri,
Na huo ndiyo ukweli mchungu. Biashara ya usafirishaji inahitaji uwekezaji. Nunua magari mazuri, maada ya miaka michache uza, nunua mengine!

Sasa Simba Mtoto na Raha Leo sijui hela wanapeleka wapi! Kwa sasa hawana tofauti na akina Shambalai! Yaani kuna Simba Mtoto moja ya Tanga - Dodoma, ina siti za 2 by 3! Si dharau hizi kwa watu wa Jiji la Dodoma!
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119] atali mkuu
 
Niliwahi kupanda kimbinyiko, ilikua Dar-Dodoma. Kama ningeondoka na baskeli, wangekuta nishafika Dodoma dadek zao. Maana nilitoka Dar saa nane, nikafika Dom saa sita usiku!

Aisee ilo bus lilikua likitembea au linanyata [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…