Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Ni basi gani uliwahi panda ukajuta na ukasema hutokaa ulipande tena?

Haujawahi kupanda mabasi ya mwanza ee[emoji23][emoji23]movie za mkojani hazijawahi kukosekana.
Kwa mabasi niliyoyapanda kwangu yote ni mazuri kwa safari.
Tanzanite kabla hazijaamia mbeya,Ally’s no 1,Zuberi na mwisho ni Travel Partners yote haya kwangu ni mazuri sana tatizo ni movie za mkojani tu kha
Kweli hizo movi wahusika wachukue mawazo ya wadau. Hazifai ni za kitoto kitoto sana.
 
Bus gani umewah panda na ukajutia safari yako.
Hii Post haina Afya kwa Biashara
Inamaana kama Kampuni ina mabasi 15 moja likazingua barabarani haina maana mabasi yote ya Kampuni ni mabovu?; Ungeandika watu wataje mabasi waliyosafiri nayo wakayapenda nanini walichokipenda ingeleta Afya zaidi
Naamini siku ukiingia kwenye Biashara hata kama ni ya kuuza maandazi utanielewa!
 
Aisee fikoshi ni ovyo, mwaka juzi nilimsindikiza dogo alikuwa anasafiri aiseee kwanza gari linafika stend liko nyomi Hadi mlangoni na anaenda mbali. Ikabidi siku hiyo safari iishie stend, siku ya pili yake napo kama Kawa gari inaingia stend iko full.
Tukawa wakali tukadai nauli akapanda gari jingine. Na siku hizo tunalisubiri linaingia stend saa tano, siku ya pili yake likangia stend saa saba na wakati ilipaswa lifike saa mbili asb hapo stend

Daah [emoji23][emoji23] iyo kampuni hapana alaf Siti zake ni 3/2 nilijuta mimi
 
Kwasababu zakibiashara na huenda sasa hivi wamebadilika hivyo sitawataja, wanabrand ya rangi Blue na ofisi zao pale Shekilango..hawa watu walitutoa Ubungo saa sita mchana kwenda kahama badala ya saa 12 asubuhi.

Dar lux [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Simba Mtoto ya kutoka Tanga kwenda Dodoma! Ilibakia kidogo tu itumwage Mto Wami baada ya break kufail.

Nilijalaumu sana imekuwaje nikapanda gari bovu kiasi kile! Siku hizi huwa napanda Nacharo tu. Nikikosa siti bora nikapanda hataTashrif! Ila siyo Simba Mtoto!
 
Al hushoom kutoka Moro kwenda Dodoma enzi hizo tulitoka moro asubuhi tukafika dodoma usiku.

Usisingizie tochi kipindi hiko kulikuwa hakuna tochi wala vibao vya 50. Gari inasimama kila kituo kupakia abiria dakawa, turiani, sijui dumila kote huko linasimama.

Sijui hii kampuni kama bado lipo.

Sidhan sijaiona pale mbezi
 
Hii Post haina Afya kwa Biashara
Inamaana kama Kampuni ina mabasi 15 moja likazingua barabarani haina maana mabasi yote ya Kampuni ni mabovu?; Ungeandika watu wataje mabasi waliyosafiri nayo wakayapenda nanini walichokipenda ingeleta Afya zaidi
Naamini siku ukiingia kwenye Biashara hata kama ni ya kuuza maandazi utanielewa!

Nimekuelewa sana mkuu nilikosea kidogo mwanzo wa thread
 
Kuna kipindi nilikua mwz nataka kuwahi arusha nikauliza bus linalotembea vizr likapelekwa kwenye hili bus 😃😃😃😃
Ni balaa nilitoka mwz sa12 ar tukafika sa8 mchana chuma inatembea kama ndege ni kiboko 🤚🤚🤚
Sahihi kabisa hio chuma enzi zake ilikua inakimbia kishenzi,sijui siku hizi.
 
Back
Top Bottom