Mwaka 2006 nilipanda basi ya Mohammed Trans kutoka Dar kuelekea Mwanza, safari ilianza vizuri tu kuanzia Dar hadi Dodoma hakukuwa na shida yoyote, kufika Manyoni ilikuwa bado ni vumbi kipindi hicho ikaanza kunukia ile harufu ya vyuma (Madereva na mafundi watanielewa hapa) lakini basi iliendelea kutembea hivyo hivyo. Nilikuwa nimekaa upande wa kushoto seat No. 45 kutoka mbele ndipo zilipo tairi za nyuma. Tukapita Ikungi hadi ilikuwa imebaki kama 20km kufika Singida mjini ndipo tairi zote mbili za nyuma upande niliokaa zilichomoka na kuelekea porini huku nikiwa naziona jinsi zilivyokuwa zikikimbia [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23]
Dah! Aisee basi iliserereka na kusimama.
Watu wote tulishuka kwenye basi kufika chini iligundulika kuwa stadi zote zimekatika!! Hiyo ilikuwa jioni majira ya saa 11 hivi. Tulikaa pale hadi saa 2 usiku. Tangu siku hiyo niliichukia sana kampuni ya mabasi ya Mohammed Trans