Ni biashara gani ambayo huelewi faida wanapata vipi?

Ni biashara gani ambayo huelewi faida wanapata vipi?

Maduka ya IPhone pale Makumbusho...
kwa maana.
Pale Frame ni gharama ,maduka yapo mengi sana, matumizi yao binafsi, matumizi ya ofisi....halafu nikiangalia mtaani Techno,Infinix na Samsung ndiyo nyingi.
Kuna mtu alianzisha uzi humu akasema ana wasiwasi na aina ya biashara wanazofanya pengine kuna aina nyingine ya biashara si bure

Unakuta mtu ana bonge la duka ila simu ni chache tu kama sio kadhaa ila yamejaa macover tu, sasa ukioanisha na gharama za frame mahesabu hayaji kabisaaa
 
Ujenzi wa maghorofa makubwa ya biashara na ofisi,wanapataje faida...?
-Ujenzi una gharimu mabilioni.
-uendshaji wa Majengo unahitaji mamilioni
-Kodi zao zipo juu
-Majengo mengi hata nusu ya floor zote zipo wazi.
Hapo wengi ni kama wanahifadhi pesa tu, yaani badala ya kwenda kuiweka benki, anaamua kuilaza tu hapo.., kumbuka , pesa inashuka thamani, pesa ukiweka leo benki, kama ilikuwa na uwezo wa kununua gari, ukienda kutoa baada ya miaka 30, unaweza usipate hata baiskeli. Ila nyumba na rdhi vinabaki na thamani kama sio kuongezeka
 
Then why wasi
Inunue Hisa,Bonds & Biils,Fixed account,Hedge fund..value ya pesa huko inabaki palepale...
And mostly ni matajiri weusi.
 
JAMIIFORUMS
-mnalipa kodi
-mnalipa pango,maji,umeme
-mnanunua mitambo
-Mnalipa mishahara na viinua migongo.
-Mnanunua vifaa,mnafanya marekebisho
-Hamfanyi matangazo
-Mnalipia gharama za kesi mahakamani
-Mnalipia server,vibali.
Mr.Melo,mnatengenezaje faida.
MODS ,tuleteen mkuu Melo,
Mana usikute faida ni kubwa nasi tunakaa kizembe tu hapa mjini.
 
Back
Top Bottom