Point of No Return 19
JF-Expert Member
- Jul 2, 2023
- 203
- 472
Wakuu,haya tuambieni Ni biashara Gani ulianza na pesa kidogo na inakulipia bills zote,saidia na wengine 🤔🙏❤
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bado uko nayo hiyo biashara?Nikiwa chuo mwaka wa Kwanza
Nilijichanga changa nikafungua
Vijiwe viwili vya kuuza pweza
Kimoja mitaa ya mwenge
Kingine buguruni
Nikawapata madogo wawili wakutoka lindi wakawa wananiuzia
Nilianza na capital ya laki moja na themanini (180k) kwa kila kitu
Yaani
Meza 2 za kishkaji
Themosi, vikombe, vijiko, bakuli
Majiko ya mkaa
Mkaa kidogo
Viazi vya kachori
Mafuta
Pweza nilianza na kilo 5
Nauli za madogo
Nk
Baada ya miezi minne nilifungua
Vijiwe vingine vitatu
Gongolamboto
Mbagala kwa Aziz ally
Ubungo riverside njia panda ya makoka
Na ilikuwa inanipa pesa nzuri kwa wakati ule
Changamoto ilikuwa ni kupitia na kuzunguka vijiwe vyote kukagua nini kinaendelea
Nilichofanya nilikuwa nachukua faida buku 2 kila kijiwe kila siku, na hiyo pesa naikusanya jumamosi
Kila jumamosi nilikuwa nachukua elf 70
Na mara chache ilikuwa inapungua kulingana na changamoto
Nashukuru wale vijana walikuwa waaminifu, sikuwa nawalipa mshahara, yaani niliwaachia mtaji mi nachukua buku 2 kilichobaki chao, ila nazingatia mtaji anaulinda
Niliiacha kitambo sanaBado uko nayo hiyo biashara?
Kweli, wengi hutumia sana ndumbaBiashara yeyote ukiwa na uchangamfu nauserious unapata wateja ukizubaa basi ila wenzako wanatumia maujanja yao hapa hawakuambi
Ingekua uchawi upo basi hakuna mtu angekua na maisha duni.Biashara yeyote ukiwa na uchangamfu nauserious unapata wateja ukizubaa basi ila wenzako wanatumia maujanja yao hapa hawakuambi
Hasira yanini ?? Kuwa mpole kama hutumii basi ni weweIngekua uchawi upo basi hakuna mtu angekua na maisha duni.
Acha mawazo ya kipumbavu wewe ni mtu mzima.
You're becoming a man.Ingekua uchawi upo basi hakuna mtu angekua na maisha duni.
Acha mawazo ya kipumbavu wewe ni mtu mzima.
Asante studio.Ingekua uchawi upo basi hakuna mtu angekua na maisha duni.
Acha mawazo ya kipumbavu wewe ni mtu mzima.
Uchawi kwa ajili ya utajiri ni kama shule, sio kila anayesoma anafaulu.Ingekua uchawi upo basi hakuna mtu angekua na maisha duni.
Acha mawazo ya kipumbavu wewe ni mtu mzima.
kanisa kidogo tuWakuu,haya tuambieni Ni biashara Gani ulianza na pesa kidogo na inakulipia bills zote,saidia na wengine 🤔🙏❤
Mkuu ndo nakomaa nayo bado sjawa consistent profitable lakini inalipaforex sijui ningekuwa wapi