Ni biashara Gani ulianza na pesa kidogo na inakulipia bills zote,saidia na wengine πŸ€”πŸ™β€

Uliazaje azaje mkuu naomba idea yko kidogo nipate mwanga
 
"Usikae na hela always ukishauza jioni ukifunga hesabu hela yote kanunulie bidhaa zingine..... " Nimependa sana hiki kipengele
 
Haya sasa ndio mambo
 
Kwamba Buku 2 kwa siku kijiwe cha pweza??????????? Au mimi kuna kitu sielewi hapaa
 
Kwamba Buku 2 kwa siku kijiwe cha pweza??????????? Au mimi kuna kitu sielewi hapaa
Yes maana walikuwa wanauza supu ya pweza, pweza, na kachori

Na madogo walikuwa wanapata faida sana, sometimes kuna siku walikuwa wanaondoka na faida ya elf 15 na zaidi mkuu

Kati ya hao madogo saivi wawili wapo kariakoo wanapiga pesa kupitia mitaji iliotoka kwenye pweza,

Mwingine bado nnae mimi mpaka Leo ingawa ana mishe zake zingine anafanya
 
Kwa pweza mbona kama ulikuwa unachukua hela ndogo sana kulinganisha na mzunguko wa biashara ulivyo....
 
Ilikua 2018....

Nilianza kuuza dawa za mbu nilikua na mtaji wa 60k tu....
Nilikua naenda Kule kariakoo naunua box zima la hizo dawa zile za kuchoma zipo karatasi lile box limeandikwa SHENKE...

Enzi zile bei ilikua 50k japo bei haikua constant kesho yake unaweza kuta kimepanda Hadi 70+k...

Mimi nilikua nachukua box zima nikija nafungua humo kuna vibox vidogo vidogo ndo nilikua nawauzia wale "wauzaji wa rejareja" maeneo ya mbezi Louis ile stand ya maramba mawili....

Box liliisha nilikua na uhakika wa kupata 20+k... Kuna siku ilikua kuuza box mbili Hadi tatu ni kawaida hasa bei ikipanda kariakoo ilikua n full bata....
View attachment 2818492
 
Nami pia
 
Kuna ndugu yangu alifanya hivi kama wewe.Aliweka duka ila target yake kubwa ilikuwa kwenye MCHELE NA MAFUTA YA ALIZETI.duka lilikuwa la rejareja target products zilimlipa sana.Mpaka leo ni mfanyabishara mkubwa.
 
Kuna ndugu yangu alifanya hivi kama wewe.Aliweka duka ila target yake kubwa ilikuwa kwenye MCHELE NA MAFUTA YA ALIZETI.duka lilikuwa la rejareja target products zilimlipa sana.Mpaka leo ni mfanyabishara mkubwa.
Vijana wanaidharau hii lakini Ni nzuri kwa anayeanza na unaweza kuibadilisha badaye ukawa wholesaler
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…