Ni bima ipi ya afya bora kukata? Tupeane uzoefu na ushauri

Ni bima ipi ya afya bora kukata? Tupeane uzoefu na ushauri

Hivi kumbe walibadili jina, nilidhani walifirisika. Nilikua naitumia miaka ile, enzi za hela ya mzungu wa African Barrick.

AAR ilikua Bima poa sana, tulikua tunaruhusiwa hata kupata huduma Pharmacy tu bila kupitia kwa daktari.

Sema walipigwa sana na wanachama wao.
Nikweli kaka walikuwa wanatoa huduma nzuri sana, ila baada ya kuwa assemble gharama zimeongezeka hata uendeshaji umebadilika pia
 
Binafsi ni mdau wa afya na ni mnufaika wa bima ya taifa NHIF , Tanzania kwa ujumla tuna bima za afya nyingi sana kama :-
-NHIF
-ASSEMBLE
-STRATEGIES
-JUBILEE
-Cigna
-BRITAM
-BUPA
-UAP
-HEALIX
-WCF
-CHF
-Aetna
-NSSF
Na nyinginezo nyingi je wewe ni BIMA ipi unaweza mshauri mtu ajiunge na kwa faida zipi?

Binasi pamoja na Changamoto zote bado ntamshauri mtu ajiunge na NHIF iwe ya standard ,supplementary au VIFURUSHI kwa sababu zifuatazo -

1. Inapatikana Nchi nzima

2. Haina kiwango na ukomo wa matibabu kwa siku

3. Ina huduma zote muhimu kama kumwona daktari, vipimo, upasuaji na madawa muhimu yote.

Wewe je una uzoefu na ushauri upi?​
Bima nzuri ya afya ni wewe kuishi kiafya mkuu,Magonjwa mengi ni magonjwa ya Tabia, hizo Bima sana sana zitatusaidia kwenda kupewa madawa na sio suluhisho.
 
Magonjwa ya Tabia ndio magonjwa yanayo tusumbua sana,na Makampuni yacmadawa na hizo Bima ndio sehemu wanatajirikia.Bima sio suluhisho,Bima haiwezi fanya usipate kisukari,Kansa,Presure na kadhalika. Ila kubadilia mifumo ya maisha kutatufanya tusipate hayo magonjwa.

Sasa kimjini mjini watu wengi kinacho wapa kiburi ni hizo Bima za afya,wanaishia kuwa watumwa wa hospitali daily wako hospitali.Akikohoa tu huyo hospitali,
 
STRATEGIES, inanipeleka mpaka INDIA nikiugua, nauli yakwenda na kurudi juu yao na million Moja na laki Tano kama fedha ya kujikimu unapatiwa. Unatibiwa hospital wanazotibiwa wabunge na wafanya biashara wakubwa.
Vifurushi vyao vipoje?
 
Nimewahi kutumia Assemble wakati ikiitwa AAR, nililazwa Bugando aisee ilikuwa burudani, bima ilikuwa inacover hadi misosi. Ulikuwa ni mwendo wa kuku na sato.
Ulikuwa umejilipia au ulilipiws nankampuni
 
NHIF sasa hivi hawalipi hela ya kumuona daktari mmoja mmoja wanalipa hela ya Matibabu kwa siku hiyo uliyokwenda kutibiwa ,ukifika hospitalini ukaona Daktari mmoja au watatu wao wanalipa hela ya Daktari mmoja wakiwa wanamaana wanalipa Visit ya siku hiyo sio hela ya Daktari .

Hivyo kwa sasa unaweza kwenda hospital ukatibiwa na daktari bingwa wa Magonjwa ya ndani ,meno ,wa kawaida ila hapa watalipa ya Daktari mmoja ambae ni superior kwa hapa ni physician

Ukitibiwa hosp A leo ukaenda hosp B leo leo bado utasomeka uko hosp A huko hosp B utatibiwa kama ni Emergency au umepewa rufaa jambo ambalo la kawaida tu .
Ni Daktari hata wawili kwa hospitali moja uliohudhuria kwa siku hiyo ama, ni hurusiwi kwenda hospitali ingine mpaka iwe ni dharura
 
N
Binafsi ni mdau wa afya na ni mnufaika wa bima ya taifa NHIF , Tanzania kwa ujumla tuna bima za afya nyingi sana kama :-
-NHIF
-ASSEMBLE
-STRATEGIES
-JUBILEE
-Cigna
-BRITAM
-BUPA
-UAP
-HEALIX
-WCF
-CHF
-Aetna
-NSSF
Na nyinginezo nyingi je wewe ni BIMA ipi unaweza mshauri mtu ajiunge na kwa faida zipi?

Binasi pamoja na Changamoto zote bado ntamshauri mtu ajiunge na NHIF iwe ya standard ,supplementary au VIFURUSHI kwa sababu zifuatazo -

1. Inapatikana Nchi nzima

2. Haina kiwango na ukomo wa matibabu kwa siku

3. Ina huduma zote muhimu kama kumwona daktari, vipimo, upasuaji na madawa muhimu yote.

Wewe je una uzoefu na ushauri upi?​
Hizi zingine sizijui nilikuwa najua tuna ya NHIF tu 😅
 
NSSF Changamoto ni hapo kuchagua kituo cha afya kwenda kingine mpaka rufaa kutoka hapo
Ni limitations maana ukiwa nje ya mkoa hospitali uliochagua ni chagamoto tho wameruhusu dharura ukiwa nje ya kituo chako utapata huduma ila ni procedures unaweza ukaondoka kwasababu ya mlolongo
 
Back
Top Bottom