Ni bima ipi ya afya bora kukata? Tupeane uzoefu na ushauri

Nikweli kaka walikuwa wanatoa huduma nzuri sana, ila baada ya kuwa assemble gharama zimeongezeka hata uendeshaji umebadilika pia
 
Bima nzuri ya afya ni wewe kuishi kiafya mkuu,Magonjwa mengi ni magonjwa ya Tabia, hizo Bima sana sana zitatusaidia kwenda kupewa madawa na sio suluhisho.
 
Magonjwa ya Tabia ndio magonjwa yanayo tusumbua sana,na Makampuni yacmadawa na hizo Bima ndio sehemu wanatajirikia.Bima sio suluhisho,Bima haiwezi fanya usipate kisukari,Kansa,Presure na kadhalika. Ila kubadilia mifumo ya maisha kutatufanya tusipate hayo magonjwa.

Sasa kimjini mjini watu wengi kinacho wapa kiburi ni hizo Bima za afya,wanaishia kuwa watumwa wa hospitali daily wako hospitali.Akikohoa tu huyo hospitali,
 
STRATEGIES, inanipeleka mpaka INDIA nikiugua, nauli yakwenda na kurudi juu yao na million Moja na laki Tano kama fedha ya kujikimu unapatiwa. Unatibiwa hospital wanazotibiwa wabunge na wafanya biashara wakubwa.
Vifurushi vyao vipoje?
 
Nimewahi kutumia Assemble wakati ikiitwa AAR, nililazwa Bugando aisee ilikuwa burudani, bima ilikuwa inacover hadi misosi. Ulikuwa ni mwendo wa kuku na sato.
Ulikuwa umejilipia au ulilipiws nankampuni
 
Ni Daktari hata wawili kwa hospitali moja uliohudhuria kwa siku hiyo ama, ni hurusiwi kwenda hospitali ingine mpaka iwe ni dharura
 
N Hizi zingine sizijui nilikuwa najua tuna ya NHIF tu 😅
 
NSSF Changamoto ni hapo kuchagua kituo cha afya kwenda kingine mpaka rufaa kutoka hapo
Ni limitations maana ukiwa nje ya mkoa hospitali uliochagua ni chagamoto tho wameruhusu dharura ukiwa nje ya kituo chako utapata huduma ila ni procedures unaweza ukaondoka kwasababu ya mlolongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…