Ni bima ipi ya afya bora kukata? Tupeane uzoefu na ushauri

Ni bima ipi ya afya bora kukata? Tupeane uzoefu na ushauri

Mbona mshikaji kaandika kwa uzuri kabisa ni nini mnabishana sasa? Yeye ni mtumiaji wa hiyo bima na amedai kuna kifurushi kinatoa hiyo huduma ya gym wewe na Error 404 mnabisha tu bila uthibitisho wowote ule. Mwisho kasema wapigieni wahusika mpate uhakika zaidi bado mnabisha, Watanganyika mna matatizo sana.
Kaandika vizuri lakini service Gym kwenye bima nimepata shaka Waja Hospital ndio hospital kubwa Geita na hatutoi huduma hiyo kwa mfumo wa bima zaidi ya Physiotherapy . Labda haelewi tofauti ya hizo huduma
 
kwan gym si moja ya majukumu ya physiotherapy ? au simwelew physiotherapist?
 
kwan gym si moja ya majukumu ya physiotherapy ? au simwelew physiotherapist?
Physiotherapy ni mazoezi yanafanywa kama tiba mfano umepata stroke ukapata udhaifu wa viungo unafanyiwa mazoezi ubongo ukumbuke kazi yake na kiungo kirudi kawaida , Gym ni broad ikihusisha mazoezi ya kuweka sawa mwili hata kama hujapata shida au ugonjwa wowote haya Bima huwa hawalipii
 
Kaandika vizuri lakini service Gym kwenye bima nimepata shaka Waja Hospital ndio hospital kubwa Geita na hatutoi huduma hiyo kwa mfumo wa bima zaidi ya Physiotherapy . Labda haelewi tofauti ya hizo huduma
Wengine wanatembea na story za vijiweni
 
Sintoendelea Tena na hii mada, Kwa sababu ww unaleta theory zakwenye makaratasi Mimi nazungumza uhalisia. Wapigie uwaulize hivi nikifurushi Gani ambacho kinajumuisha huduma ya gym kwenye bima yenu, Kisha wakisema hakipo waulize, mbona baadhi ya wafanyakaz wa DEPOT ZA MAFUTA na MIGODINI wanafanya mazoezi kwa kutumia bima yenu, kwenye baadhi ya GYM za KIGAMOMBONI, Posta na Geita?. Then utuletee mrejesho.

Kua na siku njema.

Nilifika hadi kigoma gym zinapokea iyo Bima. Unachosema ni sahihi mkuu
 
Binafsi ni mdau wa afya na ni mnufaika wa bima ya taifa NHIF , Tanzania kwa ujumla tuna bima za afya nyingi sana kama :-
-NHIF
-ASSEMBLE
-STRATEGIES
-JUBILEE
-Cigna
-BRITAM
-BUPA
-UAP
-HEALIX
-WCF
-CHF
-Aetna
-NSSF
Na nyinginezo nyingi je wewe ni BIMA ipi unaweza mshauri mtu ajiunge na kwa faida zipi?

Binasi pamoja na Changamoto zote bado ntamshauri mtu ajiunge na NHIF iwe ya standard ,supplementary au VIFURUSHI kwa sababu zifuatazo -

1. Inapatikana Nchi nzima

2. Haina kiwango na ukomo wa matibabu kwa siku

3. Ina huduma zote muhimu kama kumwona daktari, vipimo, upasuaji na madawa muhimu yote.

Wewe je una uzoefu na ushauri upi?​
bima ya afya bora,ni kuacha sigara,pombe,bange,ngono!!!
 
Back
Top Bottom