Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Maisha ni mazuri mkikutana mnaoelewana
Tuishi kwa kusaidiana ndio maana ya maisha na usela wa kweli
 
You guy....My guy....
Been a long... Happy to see you here HA
 
Da maisha haya we Acha tu sitasahau nikiwa mdogo tumekuja dar kwa shemeji yangu mm na mdogo wangu
Bas bwana mdogo wangu akaanza kuumwa hakuna aliyekuwa anajali si sister wala shemeji
Si ndo nikalopoka mbona dogo hampeleki hosp?BIG MISTAKE
Shemej akanitimua kwake nikaondoka na mdogo wangu na kwenda kuishi nyumba aliyojenga mama nikiwa na mdogo wangu mgonjwa.
Tukaanza kukaa na cjui hela ya dawa nilipataga wap dogo akapona
Mfukoni nilibakiwa na Mia 5 tena mbovu nikawa naenda na dogo kula mihogo na tunapomaliza kula ndio tunatoa ile hela na wauzaji walikuwa wanatugombeza wanaturudishia ile hela kwa hiyo kesho tunabadilisha sehemu ya kula na cha ajabu tunarudishiwa tena hiyo jero:Mungu huyu
Sasa basi kwa sababu nyumba ya shemeji ilikuwa karibu na nyumba aliyojenga mama (tulipokimbilia)watoto wa sister wakawa wanakuja kushinda pale(majaribu hayo)
Ikabidi nishindwe kuacha kuwapa chakula wale watoto wa ndugu yangu nakumbuka nilitumiwaga elfu 30 na mama hivyo tukawa tunakula kwa kujibana na wale watoto wa dadangu(japo kwao kulikuwa na kila kitu)ila c unajua watoto
Yaani nilikabidhiwa jezi na mchezo wala siujui..ikabidi ninunue gunia la mkaa nianze kuuza na mdogo wangu(kumbuka wote ni watoto)ili tuweze kupambana na jiji la dsm
Mungu alileta mkomboz yule mzee wa bandari(mungu akurehemu)yaan yule kuku uliyetununulia pale bandari atukuwahi tena kula kuku mtamu kama yule(nadhan kuku kwa wakati ule kilikuwa kitu cha Thaman sana kwetu)
Now tumekuwa tunataman kurudisha fadhila kwako ila ndo hivyo kazi ya mungu
 
See God now!!!!

Mungu anatutoa mbali, anatupeleka mbali....Glory to the Most high alone.

As long as your happy,I'm happy and GOD is Happy..
Enjoy life My friend Humble..Wewe ni mtu poa sana.... Na unastahili kila kilicho chema kwenye hii Dunia...

NB,Usiwe unapotea namna hii hapa jukwaani..Wewe una vitu vyako special sana sana...Hatuvipati popote hapa...Amini kwamba.
 
Mzee baba upo?
Msalimie CCNP Engineer
 
Nimesoma hii Comment yako machozi yamenilenga[emoji26]

Iko hivi Mkuu...Kuna watu ni Daraja,Baraka katika maisha ya watu wengine....Hata wewe pia...

Hujawahi kuona unaweza kuwa kwenye changamoto fulani halafu Mungu anamleta mtu wewe mwenyewe huelewi..Then huyo mtu atakusaidia kwenye hiyo changamoto.. ukivuka hapo anaondoka na siyo mmegombana... ni ukaribu tu unapungua..Maana yake ni nini? Kazi yake ameimaliza...Anatakiwa akafanye kingine kwa wengine na wengine tena...Hawa watu wanaitwa "Destiny Helper"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…