Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Sitaki kuamini Humble African mzee wa forex alifulia kiasi hiki mi najua utakuwa mtu mzito sana bongo hii.
 
Maisha ni safari ndefu sana nikikumbuka ya nyuma namwambia tu Mungu Asante umejua kunifurahisha[emoji120]nishawahi kuzimia na njaa mara mbili
Mkuu hii post nimecheka,siyo Kwa kufurahi hapana, ila najaribu kuimagine, tukio ambalo lilitokea, Kuna mdada alizimia msibani, wakadhani homa. Mmoja akasema tumpikie uji kwanza ndipo tumpeleke hospitali, wakapika uji, alivyokunywa uji jasho lilitoka sana tena sana, ugonjwa uliisha, kumbe alikuwa na siku kadhaa hajanywa hata maji
Acha tu maisha haya.
 
Ukiwa na njaa ni sumu kunywa maji, unakufa ukinywa maji nakwambia. Utumbo utajinyonga haraka sana
 
Hii inaweza kuwasaidia

Kwa hustler yeyote ukiingia kwenye mji au nchi yoyote ambao ww ni mgeni huna pa kufikia wala hujui utapata wapi kibarua, cha kufanya uliza mwenyeji yeyote akuelekeze mahali Soko kubwa la mji lilipo.

Amini nakwambia hutolala njaa pindi ukifika sokoni na hutakosa kazi ya kufanya hata kubeba mzigo utabeba na pesa utapata.

Why Sokoni na si mahala pengine? Sokoni ndio sehemu ambapo kuna mzunguko mkubwa wa pesa katika mji au kitongoji husika. Baada ya hapo sasa utaweza kuangalia ufanyaje ili utoke kimaisha.

Sehemu nyingine ambayo inaweza kukuokoa ni Migahawani au Hotelini. Hii sehemu inaweza kukuokoa usilale na njaa na pia unaweza kupata ujira mdogo. Ukifika maeneo hayo omba kazi ya kufanya usafi na hata kuosha vyombo. Hii itakusaidia sana kupata ujira mdogo na chakula pia.

Mwisho kabisa ni nyumba za ibada iwe msikitini au kanisani. Huku kunaweza kukupa fursa ya kukutana na watu wenye hofu na kumjua Mungu hivyo ni mara chache sana kwa wewe mgeni kukosa hifadhi au chakula, na ukiwa nao vizuri unaweza ukapatiwa connection ya kazi.

Kikubwa ukifika sehemu yoyote jiepushe sana kuomba Fedha bali omba kibarua /kazi ,hii itakuwezesha upate pesa ya kujikimu na vilevile kukuepusha dhidi ya fedheha na udhalili wa kuombaomba. Kumbuka mwanadamu hapendi kuombwa pesa.

Katika kutafuta pesa epuka kitu kinachoitwa kuona aibu, watu watakuchukuliaje nk. Mwanaume hachagui kazi as long as kazi hiyo ni ya halali na haimuondolei utu wake.
 
Dah me ndo kila ck maana napenda vitu vizur, nipo radh kutoa hela yote ndan na nisijue yq kesho kwa ajil ya kitu tu sas sikiliziq mbele hapo kama co mim wa jana kuwa na malaki
 
Nikweli kaka, Mungu ni mwema wakati wote
 
Ukiwa na njaa ni sumu kunywa maji, unakufa ukinywa maji nakwambia. Utumbo utajinyonga haraka sana
Mkuu watu wameshindia maji pekee,mtu akiwa na njaa anapiga maji njaa inapoa msishs yanasonga.

Maji sio sumu mkuu,unaweza kunywa na yakapoza njaa,ukiona tumbo linauma zaidi sio maji yaliyosababisha bali ni kitu kingine
 
Watoto hutakiwi kuwazoea kama si watoto wako, ila wa ndugu, majirani waogope kama ukoma.

Kwa ufupi wafukuze wakuogope
Nilishawahi kubambikiziwa kesi aisee ila cha ajabu sikuwa na mazoea kabisa na huyo mtoto, nilikuwa teenager tunakwenda kucheza mpira uwanjani karibu na kwao. Nakuja kustuka mama kambeba mtoto na mwanawe mwingine wa kiume wanakuja kubisha hodi home kusena kuwa nimemtia vidole mtoto wake?!!! Aisee nilishangaa sana sasa sijui alijua akija vile atapata chochote kitu kutoka kwetu.? Aisee tulimtimua mbaya sana yule bi mdashi.

Usizoee kuwa na urafiki na watoto wadogo kama sio wanao.Dunia imebadilika ,muda wowote unaweza kubambikiziwa kesi ili watu wachume pesa.

Kuna jamaa mmoja alikuwa ni dereva wa daladala amepanga kwenye nyumba moja sasa vitoto vya mule ndani vinamazoea vikimuona vinaenda kwake kuangalia Tv, sometimes anapika anawapakulia wanakula kisha baadae kila mtu kwao, dah kuna siku anarudi home mchana gari kamwachia deiwaka mchizi wake ili yeye arudi kulala kidogo, kuingia ndani kulala mlango hakuusindika wote basi kuna kitoto cha maza mmoja kikaingia ndani nacho kikapitiwa na usingizi, mama yake akawa anakitafuta hakioni,baadae kinaonekana kinatoka kwa jamaa...yule mama akakichukua kibinti chake akaenda kuripoti polisi kuwa jamaa kamlawiti mwanae...aisee kesi ikawa kubwa, polisi wanamwambia jamaa kuwa anakwenda kuozea jela maisha. Ikabidi jamaa ajitetee sana huku na huku ikamtoka zaidi ya laki 5....yule mama akagawana na askari ile pesa.

Kuwa makini kuna wanawake/wamama ni washenzi na mashetani wanaweza kuutumia upendo wako kwa watoto ili kuchuma pesa na hata kukuangamiza
 
so sad champ
RIP that legend
 

Daah! Aisee huyo binadam kweli alikuwa anajua maumivu ya kukosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…