Ni changamoto zipi umewahi kupitia ukiwa katika hali ya umasikini?

Kumbe Dar ikakushinda ukarudi kwenu Mbeya au Dodoma.

Umeona umasikini ulivyo mbaya?
Dar sio tuu nimeishi Bali nimesoma hapo Mlimani naijua vizuri..

Watu wanashindia mihogo na vile vimahindi mnapaka pilipili na mnalia chumvi πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†

Ukigeuka huku shombo ,mbele madimbwi Kila sehemu kiufupi ni hovyo , majority wanashindia biashara uchwara za kuuza maji,wanakoishi Sasa afadhali nguruwe πŸ˜ƒπŸ˜ƒ

Niliwahi mtembelea Jamaa yangu alikuwa anakaa ubungo,asiee mtu anachota maji ya msimbazi huo umejaa mataka eti ndio anatumia khaa !!
 
Sasa huoni ni sababu ya umasikini wao?

Tatizo we naye unaandamana na masikini, tafuta marafiki ambao wanaweza kukusaidia na sio kulala stooo
 
Sasa huoni ni sababu ya umasikini wao?

Tatizo we naye unaandamana na masikini, tafuta marafiki ambao wanaweza kukusaidia na sio kulala stooo
Utokee familia ya chini uje kupata rafiki Tajiri never labda ni bahati ikutokee Sasa utakutana nao wapi? Saizi ndio ninao Sasa ila ningesndelea kubakia Dar ningekufa maskini 😁😁
 
Basi watakiwa ukimuona mtu anaishi Dar umsalimu maana si kazi rahisi kabisa kuishi Dsm
75% ya watu wanaoishi Dar ni maskini wa kutupwa πŸ˜†πŸ˜† na kama unataka kuwa maskini Hadi unazikwa endelea kuishi huko huko..

Kwanza wakati narudi Mkoani kilomouma maana niliacha mademu zangu kibao huko 🀣🀣

Ila uzuri kufika Mkoani nilisoyea miezi kama 6 ila msoto wa nafuu maana Niko mazingira ya home home..

Baada ya mda nikapata kazi Kwa yule mama wa PMM aliyetaka kununua mtaa huko.Buguruni ,from hero to zero ndio nikapatiaga upenyo..

Sina hamu na Dar πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mkuu familiya ya msela ambaye alihakikisha unakula nyumbani kwake na mkewe kukufungia kingine ambaye ameshatangulia mbele ya haki, huwa unapata muda kuitembelea?.
 
Wimbo wa Kamandaaa wa Duz nundaz enzi hizo wakina Feruz Daz baba wanashinda kwenye vimbweta vya pale Azania wakiishusha mistari
Daaah umenikumbusha mbali sana..Enzi hizo mchwa mpaka kapunguza ukali,Daaah kweli maisha yanasonga ni mda sasa almost 20yrs
 
Mkuu mjini mipango ila mkoani kuna fursa pia
 
Mkuu familiya ya msela ambaye alihakikisha unakula nyumbani kwake na mkewe kukufungia kingine ambaye ameshatangulia mbele ya haki, huwa unapata muda kuitembelea?.
Wamekuwa sehemu ya familia yangu kwa sasa. Watoto wake aliowaacha wadogo kama kuja kujua kuwa sikuwa ndugu wa damu wa baba yao nadhani itakuwa ni hivi karibuni tu sababu wamekuwa wakubwa kuweza kuelewa mambo. Na hilo halijaathiri upendo na heshima kubwa baina yetu.

Harusi ya binti yake nilisimama kama baba wa binti (nahisi unaweza kuhisi ukaribu wetu ni wa kiasi gani)

Msaada wake kwangu haukushia kwenye chakula tu. Alinipa connections ambazo zimenifikisha nilipo leo (sio tajiri lakini hakika namshukuru Mungu sio maskini pia), kupitia hizo connection kulifanya ukaribu wetu uwe zaidi kabla ya mauti yake sababu ya muingiliano wa moja kwa moja wa kibiashara kiasi cha familia zetu kuwa mithili ya ndugu mpaka leo hii.
 
Mungu alivyo wa ajabu, ukipata fedha unaugua kisukari! Daktari anakukataza kula vinono
 
Huu ujumbe unatia moyo Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…