Daàaaah, umenikumbusha jirani yangu alinunua TV ya m1.25 na subwoofer la nguvu katumia wiki moja wezi wakaja wakawapulizia wakalala usingizi hadi tunawaamsha saa tano asubuhi baada ya kuona kimya sana hiyo nyumba hali tumegana nao usiku wa kulala na hawakuwa na safari yoyote.
Kuwakuta ndani wakaamka kila mmoja akitokea chumba tofauti wezi walibeba na kuwatenganisha mke na mme na kupeleka vyumba tofauti. Wezi ao hao walikula msosi kwanza ndo wakabeba mzigo na hela kidogo iliykuwa around.
Wezi wa namna hii washenzi sana ila dawa yao ni ndogo tu wanapuliza lakini wanakukuta uko macho unakimbizana nao.