Ni dhambi na nuksi kuoa mwanamke alieachika au kuachwa kwa mwanaume mwingine na angali huyo mwanaume yu hai

Kwakweli Hawa majirani zetu wamezidi kunamtu kaleta Uzi mumewe Malaya anatak avunje ndoa ameshindwa alaf akiondoka et kivuli kivuli Iko kwio [emoji23][emoji23][emoji23]
Umelogwa wewe sio bure[emoji23][emoji23][emoji23], bangi hizi. Ila binafsi, kwa maoni yangu, sikubaliani kabisa kuoa mtalaka au mjane maana walishaianza safari ya ndoa tayari ila mimi nakuwa nadandia tu katikati kufuata safari yake ya maisha. Nahitaji kutengeneza na kusimamia safari yangu mwenyewe sio kufuata mwelekeo wa mtu. Kwaupande wenu wanawake, nivile mtakavyoamua maana mimi sio mwanamke. Ila kuoa mtalaka au mjane hapana kwakweli.
 
Siamini kama kuna mtu kujifunza kutokana na ndoa iliyovunjika hivyo ataiweza kuijenga vyema ijayo. Siamini kamwe, hivyo bora nianzishe mwenyewe nijue nilivunda mwenyewe nasi kusema binti wawatu kumbe hakubadilika bado. Maana hata kama aliyemuacha ndiye mwenye shida mfano muhuni ila alifikia kufanya maamuzi magumu ya kuolewa na muhuni basi hajui kushughulisha kichwa chake katika maamuzi muhimu ya maisha yake, hivyo siamini mtu huyo hubadilika. We live once then make better decisions if not best for your life.
 
Ni wewe na maamuzi Yako sio sheria
 
Hii Mada ni Nzuri pamoja na imekuja kikatili. Kumuelewa mleta mada inabidi tuivue miili ya nyama tuzame kiroho zaidi.

Humu tutakutana na kwanini wanawake wana Bikra wanaume hawana. Pia kwanini wanandoa wakiishi muda mrefu hupeleekea kufanana.. Na zaidi itabidi tujue na mahusiano ya kuzini na kumbemenda mtoto.

Hivyo basi kwa macho ya kuona hauuwezi kuiona shida ya kuoa mke wa mtu Isipokua wenye macho ya maono, na hii ni kwa sababu MWANAUME KAUMBIWA WANAWAKE na WANAWAKE WAMEUMBIWA MWANAUME.

Kitendo chakutolewa bikra kiroho nikuweka nadhiri ya kuwakilisha uumbaji kupitia mwanaume huyu mmoja tuu.. kama mwanamke atachepuka basi inatakiwa aachwe. ila atambue maumivu ya mwanaume wake ni laana atakayomuambukiza mpaka mume mpya. Na kama ni mwanaume kazingua na kuacha mke bila sababu ya usaliti nae ataondoka na laana ya maumivu ya mkewe.

So hata ukiachwa na mwanaume kama yuko hai hautakiwi kuolewa mpaka aridhie hapo agano huisha maana mnakua katika misingi ya haki.

TUTAMBUE TUU.. HAKUNA HAKI YA MTUU INAYODHURUMIWA
.. ITALIPWA TUU KATIKA KIPIMO KILE KILE.
 
Ni wewe na maamuzi Yako sio sheria
Duh! Yaishe dada mkubwaπŸ˜‚πŸ˜‚, ila ninachojua hakuna mama mwenye mtoto wa kiume atapendelea mwanae aoe mtalaka au mjane yaani nasema hakuna. Ila kwakuwa bado hujafika uko, wewe waweza liona dogo ila kwa upande wa mwanaume linamshusha hadhi na heshima kabisaaa yaani kabisa. Tena mama atakwambia msijuane, mnaangalia upande wenu tu jishusheni kwenye viatu vya wanaume pia. Kuna vitu vingi sana tunatofautiana kijamii yaani saana. Mke kutokupendeza na kupata mahitaji yake vizuri ni juu ya mume ila mume kuchakaa hakuna mwanamke atakayeulizwa bali mwanaume ataulizwa. Hatufanani na kamwe hatutakuja kufanana na hicho ndicho kinachofanya dunia iwe tamu. Nyie mnaona uke wenza fresh ilimradi staha ila si mwanaume yaani hicho ushike.
 
Wanasema mwanamke mpumbavu na mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ,so mwanamke mwenye akili na mwerevu hatoruhusu ndoa yake ivunjike kwa namna yoyote ile hivyo wanaume hatuhusiki
Kwahiyo mwanaume mlevi, mpumbavu na asiejua majukumu yake hana shida ila mwanamke anatakiwa aendelee kumbembeleza? How pathetic
 
Tutaaminije kuwa unayosema ni kweli?, humu jamiiforum mtu akikwazana na Malaya wake huko anakuja kusigina mitandaoni

Huna tofauti na Ile mijimama shapeless inavyowazibia riziki wadada wazuri wenye figure zao mjini utaskia wanaume wote ni mbwaaa
Hahahahahaja
 

Twende kwa maandiko mkuu,mkono mtupu haulambwi.
Mathayo 5:31-32 inaliweka wazi hili,inasema,
31 Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
Mathayo 5:31

32 lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
 
Nuksi yake ni ipi mkuu hebu fafanua vyema
Usifikiri mwenzio aliyeshindwa kuishi na huyo mwanamke ni mjinga ila mjanja ni wewe wa sasa. Kilichompata mwenzio siku moja na wewe lazima kitakupata. Babu yetu alikuwa anatuambia oa mwanamke alifiwa na mmewe( ukizingatia wakati magonjwa kama ukimwi hayakuepo) lakini usioe mwanamke aliye talikiwa na mwanamme mwenzio.
Nilishuhudia jamaa alioa mwanamke aliye achwa mara mbili na wanaume tofauti tofauti akaja kuolewa na jamaa yangu wa karibu. Kuna siku akajilaumu mwenyewe na kusema nanukuu " huyu mwanamke kaachwa na wanaume wawili mm ni watatu yaani wote wawili waonekane hawana akili isipokuwa mimi?!" Wakati akiyasema hayo wakati huo amesha tendwa kama walivyo tendwa waliomtangulia.
 
Kwahiyo mnaleta nuksi na mambo ya tabia ya, tafsiri ya kuachana ni mmeshindwana tabia au mwenendo.
 
Mwanamke kikawaida anaishi na mzimu wa kila mwanaume alotoka nae sasa mwanamke ambae alisholewa kivuli Cha mume hua hakitoki bila sababu ya msingi ya kuachana inayokubalika kimaandiko ya Mungu
Unaweza kuwa sahihi,na mwanaume alieachika nae vipi huwa hana mizimu kutoka kwa mke aliyeachana naye au hii inawahusu wanawake walioachika peke yao...?
 
Unaweza kuwa sahihi,na mwanaume alieachika nae vipi huwa hana mizimu kutoka kwa mke aliyeachana naye au hii inawahusu wanawake walioachika peke yao...?
Mizimu haikwepeki mfano kama alikuwa anarogwa na mkewe, mkewe kama mchawi, kama mwanaume kamwacha mkewe Kwa hila pia ni noma
 
Vipi wewe ukiwa mgane
Hautaoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Vipi kuhusu kuoa aliyeacha?
 
Kwa mwanamke hivyohivyo

Kuolewa na mwanaume aliyeachika sijui aliyeachwa ni nuksi

Nina dada yangu aliolewa na mtalaka,
Hakuna picha aliacha kuona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona cha nini wenzio wanasema watakipata lini.
Muache mkeo uone kama kesho utamkuta kachunda.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…