Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Ni faida gani ataipata Mungu kwa kuwachoma moto binadamu siku ya mwisho?

Ajabu kweli ....hilo swali ulitakiwa umuulize Mungu alafu unakuja hapa kutuuliza sisi. ..kama sio uonevu ni nini
 
Shetani ni 'imaginary spirit' kuna mambo tunafichwa tu, haiwezekani Mungu atumie muda mrefu na ubunifu namna hii kuumba the said Mbingu kisha mwanadamu halafu akorofishane na kajamaa kadogo tu kisha alete distruction kubwa namna hii duniani na huko ahera tunakoambiwa!
Wewe unamawazo kama yangu yani...
 
palikuwa dampo la jiji kama kulivyo pugu. yesu alifananisha mwisho wa waovu sawa na kutupwa kwenye dampo la jiji. hakuna moto wa mateso bali kuna uzima wa milele kwa waadilifu na kifo cha milele kwa waovu.
Duh hili nilikuwa silijui ati!!
 
Swali zuri, hili jibu utalipata kwenye Quraan tu, hichi ndo kitabu cha Mungu mwenyewe.

Inabidi niivute Quraan karibu,Kwa sasa sina mda, nkipata mda ntakuja hapa tuelimishane vizuri.
Tunakusubiri kwa hamu..na mungu akufanyie wepesi upate kutupa elimu..ila tuta angalia logic
 
Mjadala mzuri,japo naona upande mmoja unatoa hoja na upande mwingine unatoa vitisho.

Mleta mada kaonesha kutokuamini uwepo wa moto wa milele,na sijaona hata sehemu moja alipoonyesha kuwa kutoamini kwake kuwa hakuna moto ni sawa na ruksa ya kutenda mabaya.

Mnaoamini uwepo wa moto (watu wa imani) mtego upo kwenye kukatazwa kuhoji tu,ukikubali tu kuanza kuhoji utaujua ukweli na utakuwa huru.

Mungu asingetaka tuhoji asingetupa huo ufahamu wa kuhoji kama jinsi alivyohakikisha haturuki hewani kama ndege bali tunatembea na kukimbia.
 
Salaaam..

Kwanza kabisa naomba niweke msimamo wangu kiimani, mimi naamini mungu yupo na ndie muweza wa yote.

Turudi kwenye mada..nacho jua mimi adhabu huwa inatolewa ili iwe funzo kwa mkosaji au kwa watu wanao mzunguka huyo mkosaji..adhabu hii huwa ni fundisho kwa mkosaji ili asirudie tena kosa pia ni funzo kwa wengine ili wasifanye kosa hilo.

SWALI:

je adhabu hiyo ya moto itakua ni funzo kwa nan??

Na je ni faida gani mungu ataipata kwa kuwa choma moto viumbe alio waumba mwenyewe..

Je shetani alipangwa ili maisha yawe hivi??

Nawasilisha..karibuni

Hakuna haja ya kutukanana ndugu zangu. Binadamu ameumbwa kureason. Dini ni imani na imani lazima iwe reasonable. kwa utangulizi huo naomba kujibu swali kwa mtazamo wa Ki-kristo.
Kuna tabia za Mungu ambazo lazima tuanzie nazo ili kujibu swali hili vizuri.

  1. Mungu ni Mtakatifu
  2. Mungu habadiliki
  3. Mungu ni mwenye Upendo na huruma
  4. Mungu ni mwenye haki

Tabia yake ya utakatifu haijawahi na haitakuja kuvumilia uovu/dhambi. Tabia ya Mungu inahitaji viumbe wake waishi kama yeye maana ni watoto wake. Tabia ya kutobadilika inamfanya Mungu asiwe ni wa kuendeshwa na matukio. alichopanga amepanga na kitafanyika no mater what. Tabia ya upendo na huruma humfanya Mungu kuvumilia na kutoa fursa kwa waovu kujirudi baada ya maonyo yake. Haki ya Mungu inaonekana pale anapotimiza takwa la umbile lake kutotendewa haki.

Sasa dhambi ni tatizo kati ya Mungu na wanadamu wote nikiwemo na mimi. Hii haiendani na tabia ya Mungu, hili linasababisha hasira ya Mungu kuwaka juu yetu wote. Mungu anafanyaje sasa? 1. Kwa upendo wake anaokoa wote wanaomkubali Yesu kwa maana hasira yake juu yetu imewekwa juu ya Yesu. 2. anawachoma moto wote wanaomkataa Yesu ili haki itendeke na kubaki kuwa mtakatifu.

Kwa hiyo siyo suala la Mungu kupata faida, bali kuweka sawa mahusiano na tabia yake.
 
Lakini vitabu vinasema kuwa ni moto wa milele..je kutakuwa na mahusiano mazuri hapo kati ya mungu na wanadamu??hebu fafanua vizuri
 
Lakini vitabu vinasema kuwa ni moto wa milele..je kutakuwa na mahusiano mazuri hapo kati ya mungu na wanadamu??hebu fafanua vizuri

Mahusiono na tabia yake sio na wachomwa moto. Yaani tabia yake ibaki kuwa takatifu.
 
Mkuu ulishawahi kaa siku moja ukafikiria jinsi mwili wa binadamu ulivyo complex? Na nani hasa aliudesign na kuutengeneza hapo ndio utajikuta lazima uamini kuwa Mungu yupo tena kweli kabisa.
Super computers za sasa ziko designed na binadamu like you and me na ziko complex like any other system or human body na zinafanya kazi close to human brain,in future ukiongeza na AI (artificial intelligence) na mambo kama quantum computers,material science etc,nafikiri super computers zitakuwa more complex and powerful than anything you ever know na uwezo kuliko human brain millions times, nafikiri swala kuhusu mungu in future litaweza kujibiwa precisely kutokana na maendeleo ya science and technology...ni swala muda tuu
 
Na vitabu vinatuambia Mungu (our father),sasa baba kweli anaweza kumchoma mwanaye moto wa milele maana kwa hali ya kawaida tuu baba atamtetea mwananye na atakuwa tayari kuchukua adhabu ya mwanaye hata kama ni jambazi , na vitabu vinasema mungu ni mwenye huruma na mwenye kusamehe kuliko chochote kile tunachokifahamu,sasa vipi hapo hakuna msamaha kweli? nina doubts zangu na haya maandiko lakini ill keep to myself for now
 
Basi wapagani wana thinking capacity kubwa [emoji1]
Wapaagani pia wana imani zao...modern religious civilization huwaona hawana dinj kwa kuwa hawasapoti their beliefs. Anyway thats how religiuos philosophers argue..
 
Eti wanasema religion limit your thinking capacity...religion philosophers

Thinking capacity also is a belief, kwa hiyo hakuna asiye na imani ya dini. Kama huna imani na Mungu una imani na uwezo wako wa kufikiri. Hiyo ni dini yako. you are your own creator or nature is your creator.
 
Nadhan hoja ya msingi hapa si swala la kuchomwa....bali lile swala la kuchomwa milele....hapo kwenye umilele ndo panaleta utata hasa....! Mfano umefanya dhambi miaka 80 yaan uhai wako wote...vip uje uchomwe milele na milele daima?! Na daima?! Si swala lenye haki kwakweli!
 
Swali zuri, hili jibu utalipata kwenye Quraan tu, hichi ndo kitabu cha Mungu mwenyewe.

Inabidi niivute Quraan karibu,Kwa sasa sina mda, nkipata mda ntakuja hapa tuelimishane vizuri.
binadamu watabaki kuwa binadamu tu,eti quraan kitabu cha MUNGU mwenyewe kuna wenzako watakuja nao watasema biblia ni kitabu cha MUNGU mwenyewe hivyo hivyo mwisho wa siku wote hamjibu hoja mnaanzisha hoja yenu ambayo hata haihusiki........
 
Nadhan hoja ya msingi hapa si swala la kuchomwa....bali lile swala la kuchomwa milele....hapo kwenye umilele ndo panaleta utata hasa....! Mfano umefanya dhambi miaka 80 yaan uhai wako wote...vip uje uchomwe milele na milele daima?! Na daima?! Si swala lenye haki kwakweli!
hizi siasa sasa kama sio kujifanya tunajua sana haki kama MUNGU ajuavyo
 
Back
Top Bottom