Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

kuna mahali nilishiriki kuaga msiba mmoja nikakuta magari matano matatu yakiwa BMW yametaga kabisa.

ingawa jamaa ana pesa ila nikawaza si bora auze tu watu wayapasue kuliko yanavyozidi kuoza.

ila zilikuwa akili zangu nisiekuwa na mpunga.
Huo msiba sio ununio kweli
 
Mkuu tukiwaambia watu Yale Ni magari ya matajiri hua wanabisha sana,Ile ngoma inatakiwa warranty ikiisha unachukua Chuma kingine chap.
Hichi ndio kinawabeba huko kwa wenzetu.. Hiyo warranty tu ndio msaada.. Maana trip za garage za kutosha.


Link nimeweka hapo. Ukipitia utajua kila mtu analia... Nyingine ni mpya kabisa ila ni mawazo tu.
 
Mambo mtaani na huko jf ni mbingu na ardhi, wanaosemaga spare za toyota hazisumbua sijui wanapataga waapi hili
Kusumbua na bei ni vitu viwili tofauti..

Sio Toyota zote spare ni cheep... Urahisi wa Toyota ni kwamba unapata gari la hali yako... Sasa unategemea Harrier iwe na shokup bei sawa na Vits?
 
Sina experience sana na magari ila kuhusu bajaji simshauri mtu anunue bajaji ambayo ndio toleo la kwanza kuingia sokoni na zile ambazo hazina mfumo wa Kick.

Nimeonja joto la jiwe sina ham nazo kabisa
Bajaj kwa hawa madereva ni biashara kichaa
 
Nimetokea kuyachukia magari yote baada ya juzi kupewa lift mwenye gari akaweka mafuta ya elfu 40 na hayakufika hata Lita 12
Nimeweka 40 juzi nikapewa Lita 11
Nikabaki naduwaa maana sikutumia gari kama miezi 2 na niliacha ina mafuta sasa nikawa naenda kibaha kupitia bahamoyo nikasema wacha niwke mafuta kabisa.... hatar anaupiga mwingiii
 
Hichi ndio kinawabeba huko kwa wenzetu.. Hiyo warranty tu ndio msaada.. Maana trip za garage za kutosha.


Link nimeweka hapo. Ukipitia utajua kila mtu analia... Nyingine ni mpya kabisa ila ni mawazo tu.
😄😄😄😄 Uko sahihi kabisa mkuu,Ni vile tu Wajerumani weusi wa JF hua hawakubali ukweli huo mzee.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kiujumla magari mengi ya ulaya hassa uingereza na ujerumani karibu yoote yanakuwa over Engineared ! Wanazingatia saana usalama na comfort ya gari, vile vile yanakuwa yametembea saana kilometa nyiingi, likiisha warranty wanauza.
Kwa namna hiyo kununua yaliyotumika used, kuwa na changa moto nyiingi saana na kati ya gari kumi saba hazifiki miaka mitatu Bongo, ununue iliyo kuwa bado ina upya itakupa muda kiasi, nimemiliki nyiingi tu kweli likiwa used na model chini ya miaka 13 hazifai. Bora kuanzia 2015 ambazo ni za gjhali saana. Sishauri mtu mwenye kipato chochote kununua gari ya zamani mno za Europe ni pasua kichwa.
Kwa mjapan Nissan nyiingi zinafanana spare parts zake tabu na bei juu mfano. Namiliki Nissan Patrol y62 ya 2017 - gari V8 ina nafasi ina nguvu nilinunua mpya sasa inasoma laki km kwenye Dash board ilipofika kM 92,000 ilisumbua sana senser, ignition coils,plugs,rejeta, fuel pump n.k. nilisimamisha miezi mitatu nakusanya nguvu kuagiza spare na ufundi wa uhakika limegharinu zaidi ya milioni 27. Kwa sasa lipo saafi illa sishauri kuwa mtu awe nalo labda uwe na uwezo wa pesa, natumia kwa safari sasa sana na lipo saafi na lina bugia wese balaa gari ya starehe na nguvu.
Nimenunua gari mbili hilux 2017 used na harrier 2008 used yaani na enjoy hamna shida natumia killa siku na masafa mafupi mambo safi na wife nimemchukukia Crown Athletic 2010 ( alikuwa na Bmw x5 ilitushinda) ana enjoy na kwa sasa hata pesa zinabaki na mjengo wetu unaelekea kwisha bado kidogo.
Nimemiliki namshukuru mungu gari nyiingi aina nyiingi , Gari ni Toyota kwa Africs.
Nissan naitangaza hakuna mteja na mpango wa kuliuza lipo safi sasa hata offer niliyopeea ya Mill 100 bora kuliko likianza matatizo.
Nimeagiza Toyota Prado Diesel litafika mwishoni mwa mwaka kwa njia ya finance la mwaka 2021 ni mara dufu bora.
Kuna jamaa yangu analo la 2016 hadi leo KM 278,780 hamna shida ni Breki na service tu.
Kwa uchache Bongo ni Toyota hata ukiwa na pesa vipi zingine ni majanga tu.
 
Yaani hapa unaidiss mercedes benz



Halafu hapa unakuja kuipraise Jeep.

Kuna Jeep Wrangler nyingi tu Engine na Gearbox vyote kafunga from Mercedes. Halafu bei mkasi. Halafu ndio gari inaongoza duniani kwa kutoshuka bei kama nyanya.
Ubovu wa gari sio Gearbox na Engine tu, kama BM engine zao waga ziko vzr, inategemea na aina gan ya engine na toleo lip
 
Back
Top Bottom