Kiujumla magari mengi ya ulaya hassa uingereza na ujerumani karibu yoote yanakuwa over Engineared ! Wanazingatia saana usalama na comfort ya gari, vile vile yanakuwa yametembea saana kilometa nyiingi, likiisha warranty wanauza.
Kwa namna hiyo kununua yaliyotumika used, kuwa na changa moto nyiingi saana na kati ya gari kumi saba hazifiki miaka mitatu Bongo, ununue iliyo kuwa bado ina upya itakupa muda kiasi, nimemiliki nyiingi tu kweli likiwa used na model chini ya miaka 13 hazifai. Bora kuanzia 2015 ambazo ni za gjhali saana. Sishauri mtu mwenye kipato chochote kununua gari ya zamani mno za Europe ni pasua kichwa.
Kwa mjapan Nissan nyiingi zinafanana spare parts zake tabu na bei juu mfano. Namiliki Nissan Patrol y62 ya 2017 - gari V8 ina nafasi ina nguvu nilinunua mpya sasa inasoma laki km kwenye Dash board ilipofika kM 92,000 ilisumbua sana senser, ignition coils,plugs,rejeta, fuel pump n.k. nilisimamisha miezi mitatu nakusanya nguvu kuagiza spare na ufundi wa uhakika limegharinu zaidi ya milioni 27. Kwa sasa lipo saafi illa sishauri kuwa mtu awe nalo labda uwe na uwezo wa pesa, natumia kwa safari sasa sana na lipo saafi na lina bugia wese balaa gari ya starehe na nguvu.
Nimenunua gari mbili hilux 2017 used na harrier 2008 used yaani na enjoy hamna shida natumia killa siku na masafa mafupi mambo safi na wife nimemchukukia Crown Athletic 2010 ( alikuwa na Bmw x5 ilitushinda) ana enjoy na kwa sasa hata pesa zinabaki na mjengo wetu unaelekea kwisha bado kidogo.
Nimemiliki namshukuru mungu gari nyiingi aina nyiingi , Gari ni Toyota kwa Africs.
Nissan naitangaza hakuna mteja na mpango wa kuliuza lipo safi sasa hata offer niliyopeea ya Mill 100 bora kuliko likianza matatizo.
Nimeagiza Toyota Prado Diesel litafika mwishoni mwa mwaka kwa njia ya finance la mwaka 2021 ni mara dufu bora.
Kuna jamaa yangu analo la 2016 hadi leo KM 278,780 hamna shida ni Breki na service tu.
Kwa uchache Bongo ni Toyota hata ukiwa na pesa vipi zingine ni majanga tu.