Ni gari gani huwezi kununua Wala kumshauri mwingine anunue?

Mkuu, hiyo Subaru yako ina matatizo makubwa tu... Subaru hata iwe imechoka vipi, lita 1 inaenda sio chini ya kilometa 10 iwe Impreza au Forester...
Hamjanielewa nimesema subaru inanyonya mafuta halafu kwa siku unaweza tumia elfu 90 .
 
Hamjanielewa nimesema subaru inanyonya mafuta halafu kwa siku unaweza tumia elfu 90 .
Ndio ila hapo kuna tatizo kubwa sana ktk hio Subaru yako... Mafuta ya elfu90 ni lita 25 ambapo inatakiwa utembee kilometa 250... ambapo Subaru zote kwa kawaida inatakiwa itembee sio chini ya Km10 kwa lita 1. Nenda garage nzuri wataalam wa Subaru... Nimetumia Subaru Impreza na Forester kwa miaka 5, sijawah kutana na utumiaji mkubwa kias hiko
 
Gari zote Za kijerumani isipokuwa benz, gari zote Za UK, Nissan xtra, Nissan Mach, hino, vits new model,
 
Umeeleza vizuri..
Samahani lakini, we ni Muhaya..??
 
Mzee umeua.mim toka mdogo pale mwenge karibu na polisi kwa nyuma ule mtaa ma bmw na mabenz mazur mazur ila mabov hatar
 
Ufafanuzi tafadhali
Natumaini wazima nyote humu.
Nimeona nitolee mchango wangu hapa kwenye Nissan March.
Nimemiliki Nissan March (Old), yafuatayo ni Mazuri yake:
  1. Very economy kwenye Mafuta.
  2. Ni kizuri kwa matumizi ya kila siku, wale wa mishemishe za kubebea vitu vyepesi hapa na pale, kinawafaa.
  3. Engine yake ni Ngumu Ukiijali Service kwa wakati, rejeta itaitaji modification kidogo kwa kureplace zile Plastic top covers kwa steel top covers ili kuzuia kuchemsha.
Changamoto zake:
  1. Spear Mpya dukani hamnaga, nishasota sana maduka yote makubwa ya Nissan, wanakwambia hamna demand ya spear parts kwa hizi gari maana ni zakitambo. Spear parts utapata kwenye Used tu mfano ilala, Tandale kwa Dar.
  2. Spear parts ni Ghali mno so unatakiwa ujimudu.
  3. Spear parts kwakua ni used, zinakua na maisha mafupi mno, so kujikuta unabalidilisha spear moja mara 2 mpaka 3 kwa mwaka ni kawaida mno.(mfano Hub bearings, shock-ups..)
  4. Kiujumla maintainance ya hichi kigari iko juu sana compared na wenzake kina VITS, IST, DUET, SUZUKI K nakadhalika.
  5. Ukimiliki Mjini tu, ukienda chaka huko utaki telekeza.
 
Mi nina mazda cx 5 yangu mwaka wa nne sasa japo ilipata ajali imesharudi barabarani tayari iko fresh kabisa..... Napata heshima gari ni maamuzi tu na uelewa kuna gari zinahitaji u smart kichwan sio kichwa I mweupe halafu unataka umiliki lazima tu utaanza kumtukuza mjapan hasa Toyota but always mm nasema bongo hasa Tz hatuyapendi magari tupo poor why kenya European zinafanya vizuri sana
 
Mkuu, hiyo Subaru yako ina matatizo makubwa tu... Subaru hata iwe imechoka vipi, lita 1 inaenda sio chini ya kilometa 10 iwe Impreza au Forester...
Vipi kuhusu mnyama legency kila kukicha watu wana jitahidi kuziuza tena bei ya kawaida Forester xT habari nyingine inapuuliza wese asikwambie mtu
 
Vipi kuhusu mnyama legency kila kukicha watu wana jitahidi kuziuza tena bei ya kawaida Forester xT habari nyingine inapuuliza wese asikwambie mtu
Legacy zinauzwa cheap kwasabab zimepoteza mvuto na muonekano wake kama tax za kizaman alafu ndani space ndogo😅, ila si kwamba ni mbovu au zina shida... Subaru XT tena uikute ni Turbo inavuta wese sana wenyew wanasema Turbo ili isile mafuta inataka speed ukiwa high way ndio utainjoi ila ukiwa na trip za mjini tu wese linaenda, japo sio sana kias cha kutisha ni 9km per lita...
 
 
Imprezza ina tofaut gani na IST? Kwa cc?

Mkuu usijidanganye na cc 1490 za subaru ukadhani ziko sawa na za IST.

Cc za gari zinaweza kutumika ku determine power na ulaji mafuta wa gari, ila sio kigezo pekee cha ku determine hizo.

Kuna vitu vingi sana vina determine na inabidi uwe unalijua gari moja moja na mifuno yake ndipo utaweza kujua ipi unakula zaidi.

Factors ni kama hizi
  • type ya engine
  • mwaka wa gari
  • aina ya mafuta inayotumia
  • technology iliotumika

Mfano mdogo tu, kuna gari inaitwa Mazda rx 8, hii gari ina cc1300 tu, ila ndugu ya tu usijidanganye ukaifukuzia ikakukalisha wewe na cc2500 za brevis yako. Na inabugia mafuta kuliko hata toyota za Cc2500. Why? Sababu inatumia rotary engine tofauti na za toyota.

Turudi katika ulinganisho wako, Subaru wanatumia boxer engine, ni powerful na zinabwia mafuta ukilinganisha na cc za engine za toyota.

Yaani ukiweka subaru ya cc1490, 1990 zinabwia wese na powerful zaidi ya toyota za same engine size

Mfano mimi natumia Volkswagen polo ina cc 1380 tu, ila kanakunywa mafuta vizuri na kanakimbia kuliko hata IST ya 1490, na hata baadhi ya magari ya cc2000+ nawakalisha vizuri tu

I hope umenipata hapo
 

Unajua lkn turbo ina-operate vipi?Yaani turbo 'ifunguke' kweli kweli halafu Muda huo eti consumption ndio iwe ndogo?Aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…