Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Jamani nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa kuna kikao cha chama kinaendelea Ikulu. Sasa mimi najua wale wengine waliisha pigwa stop siasa mpaka 2020 na mikutano marufufu hata ile ya ndani ni shida tu kila siku wanafurushwa sasa iweje hawa wanafanya tena kwenye nyumba ya umma? je hawa wengine nao wakiomba kwenda kufanyia vikao vyao kumbi za Ikulu wataruhusiwa?
Inaelekea chama bado kimeshika UTAMU ............ sorry, HATAMU!!
 
Hahaha yaani tuna shiida upstairs!! Hivi kwa kuwa CCM ni chama tawala mnaweza kufanyia hata kwenye kumbi za mahakama??
CCM inatawala na kila kitu ni chao hata wakiamua kufanyia bungeni hakuna mahakama ambayo haiko chini ya serekali ya chama cha Mapinduzi pia
 
Dunia ya wapumbavu tuu ndo inaweza kufanya huo uzwazwa unaoutetea
United Russia wanakutana Kremlin na Putin tumeona, Republican wakikutana White house Jubilee wakikutana na Kenyata Ikulu sasa wewe unataka Rais akakutane na watu wake ddc kariakoo au vipi
 
Askofu ama padri hawezi kufanyia vikao vya ukoo ama famlya yake kanisani
Hivyo hivyo rais magufuli hawezi kufanyia vikao vya ccm ikulu
Waumini wa kanisa wanaruhusiwa kwenda kusali kanisani kila wakihitaji,lkn waumini wa kanisa hawawezi kwenda kufanyanyia ufusuka kanisani
Hivyo hivyo watanzania wanaruhusiwa kwenda ikulu kumuona rais wetu,lkn ccm kama chama hakiruhusiwi kufanyia vikao vyake ikulu
Ccm kufanyia vikao vyake ikulu ni sawa na kushusha hadhi ya ikulu yetu
 
Huyu anateswa na albadir..... Bado haijashika kasi ndo imeanza.
 
Utaratibu tumejiwekea wenyewe,alfu rais anavunja utaratibu huo kwa kutumia mabuvu ya vyombo vya wananchi
 
Askofu ama padri hawezi kufanyia vikao vya ukoo ama famlya yake kanisani
Hivyo hivyo rais magufuli hawezi kufanyia vikao vya ccm ikulu
Waumini wa kanisa wanaruhusiwa kwenda kusali kanisani kila wakihitaji,lkn waumini wa kanisa hawawezi kwenda kufanyanyia ufusuka kanisani
Hivyo hivyo watanzania wanaruhusiwa kwenda ikulu kumuona rais wetu,lkn ccm kama chama hakiruhusiwi kufanyia vikao vyake ikulu
Ccm kufanyia vikao vyake ikulu ni sawa na kushusha hadhi ya ikulu yetu
Tundu Lissu ana vyeo vingapi, ?? Huwa anatofautishaje maneno na vyeo vyake kwenye press conference
 
Nimesoma gazeti la Tanzania Daima ambapo mwandishi analalamikia tukio la kikao cha CCM kufanyikia katika ukumbi wa ikulu. Napenda kutoa angalizo tu kwamba kimantiki kuna tofauti baina ya mkutano kufanyikia katika ukumbi wa ikulu NA mkutano kufanyika ikulu. Rais mstaafu alipowaalika viongozi wa Chadema kwa mfano, mkutano ule ulifanyika Ikulu kwa maana uliitishwa na Rais na itifaki yote ilizingatiwa lakini Mwenyekiti mstaafu wa CCM alipoitisha kikao cha kamati kuu ya CCM kwa mfano, mkutano ule ulifanyika katika ukumbi wa ikulu na taratibu za chama zilizingatiwa ikiwemo kuvaa sare ya chama. So hakuna ubaya kwa chama kutumia ukumbi wa ikulu, nimemsikia hata Rais wa sasa kupitia Clouds 360 akisema hata wapinzani wanaruhusiwa kutumia ukumbi ule ilimradi tu waeleze ajenda za mkutano tarajiwa. Tumeelewana?!
 
Siamini kama ccm hawajui sheria ya maadili ya umma inayokataza vikao vya vyama vya siasa kufanyika kwenye ofisi za umma

Kwa nini kamati ya maadili imeshindwa kuwazuia ccm kuvunja sheria? je nikuogopa kutumbuliwa? hivi nini kimetokea nchini watu kushindwa kusema ukweli?
 
Back
Top Bottom