Mkuu, naomba nikiwa nikufahamishe kuwa sina personal issue na mtu yeyote, na uandishi wangu hautawaliwi na hizo. Kama umesoma vizuri nimeuliza swali la kimsingi kuhusu kufanyia vikao vya chama tawala ikulu. Nakumbuka kuanzia enzi za TANU (ndiyo, nakumbuka vizuri sana) vikao vya chama vilifanyika katika ofisi za chama, hata wakati wa Chama kiliposhika hatamu, ndio kwanza makao makuu ya CCM Lumumba street, yakapata hadhi zaidi. Je kumekuwa na mabadiliko rasmi mapya yaliyotokea ambapo chama tawala kimeshika hatamu tena
Mkuu sio kweli kwamba tokea zamani vilikuwa vinafanyika kwenye makao ya ccm,Kuanzia wakati wa Mwalimu Nyerere,Wakati wa Mwinyi,Wakati wa Mkapa,Wakati wa Kikwete mpaka utawala huu wa awamu ya tano,wote wamefanyia vikao,vya chama kinachotawala ikulu.
Hata kwa rais Magufuli hii si mara ya kwanza,Mwaka 2016 My 05,ccm walifanya kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu,Ikulu ya Chamwino,lakini hukuuliza kwa nini,au ilikuwa ni sahihi kufanya vile.13-december,2016 kamati kuu ya ccm walifanyia kikao,pale ikulu ya magogoni,hukuona.
Tarehe,02-03-2015,ccm central committee walifanyia kikao cha ikulu,chini ya rais Kikwete,hukuona wala hukuoji,
Tarehe 28-02-2015 ccm central committe walifanya kikao ikulu ya magogoni,lakini hukuona
Tarehe 22-05-2010 ccm central committee walifanya kikao ikulu ya magogoni.
Chama tawala kwa kawaida kiongozi wake wakati mwingine huitisha kikao kama hicho ikulu,ili aweze kufanya majukumu yake kama rais au mwenyeketi.
Rejea mwezi April au May,wakati rais Trump alipotakakubadilisha sheria ya Obamacare,aliwaita senetors wote wa republican ikulu ya white house,kwenda kuweka mikakati ya pamoja kuweza ku-repeal Obamacare.